Emanuel Okwi mchezaji halali wa Simba kisheria...
MCHEZAJI EMMANUEL OKWI NI MCHEZAJI WA SIMBA KISHERIA
Makamu mwenyekiti wa timu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu akizungumza
na mchezaji wake Emmanuel Okwi kwa njia ya simu kutoka nchini Uganda
huku waandishi wa habari wakifuatilia mazungumza hayo.
Makamu mwenyekiti wa timu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu akionyesha
mktataba wa timu ya Simba na mchezaji Emmanuel Okwi mbele ya waandishi
wa habari
WAKATI Mshambuliaji Emmanuel Okwi amekanusha kusaini Yanga, uongozi wa klabu yake, Simba umesikitishwa na habari
zilizovumishwa kwenye vyombo vya habari kuhusu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda kujiunga na wapinzani wa jadi, Yanga SC.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makamo
makuu ya klabu Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Simba,
Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema kwamba habari hizo hazina ukweli wowote, ni
kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na zina lengo la kupotosha
ukweli na kuwanyima raha wale wote wenye mapenzi mema na Simba.
“Gazeti kama la Spoti STAREHE limekwenda mbali zaidi kwa
hatua yake ya kutaka kuufitinisha uongozi na wapenzi na wanachama wake kwa
kudai kuwa uongozi unafikiria tu kumuuza Okwi bila ya kuangalia mkataba wake.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, mkataba wa Okwi umemalizika leo
na ndiyo maana ameamua kusaini Yanga akiwa mchezaji huru,”alisema Kaburu na
kuongeza;.
“Ukweli ulivyo. Emmanuel Okwi alisaini mkataba mpya wa
kuichezea Simba mnamo mwaka jana na mkataba huo unamfanya kuwa mchezaji halali
wa klabu yetu hadi mwaka 2013. Baada ya mkutano huu, nitawaonyesha waandishi
nakala ya mkataba wa Okwi na Simba. Hivyo taarifa kwamba mchezaji huyo hana
mkataba na Simba ni za uongo, uongo mtupu,”alisema.
“Hivi ninavyozungumza nanyi, Okwi yuko kwao nchini Uganda
akishughulikia viza ya kwenda nchini Italia ambako anatarajiwa kufanya
majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika moja ya vilabu vya Ligi Kuu ya
Italia (Serie A),”alisema Kaburu.
Labels: michezo
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home