Saturday, August 18, 2012

SIMBA BINGWA BANC ABC SUP8R CUP 2012



TIMU ya Vijana ya Simba ‘Simba B’  leo imedhihirisha ubora wake baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kwanza ya Banc ABC Sup8r  baada ya kuibamiza Mtibwa Sugar mabao 4-3. 
Katika mchezo huo wa fainali uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ilionekana kutawala kila idara katika mchezo huo ambapo vijana hao waliwahenyesha wapinzani waoMtibwa. 
Edward  Christopher ndiye alianza kuiandikia Simba bao la kwanza katika dakika ya 12 alipoitendea haki pasi ya Haruna Athuman  na kumuuza kipa wa Mtwiba, Shaban Kado langoni mwake. 
Dakika ya 32 Shaban Kisiga aliisawazishia  Mtibwa kwa bao la mkwaju wa penalty  ambapo mwamuzi Hashim Abdallah kuamuru hivyo kutokana na mchezaji wa Simba  Omary Salum kumchezea vibaya Jamal Mnyate wa Mtibwa.Bao hilo lilidumu hadi timu hizo zibnakwenda mapumziko. 
Kipindi cha pili kilianza kwa timu kucheza kwa umakini huku   Simba wakicheza mpira wa akili na kuwachosha wakata miwa hao wa Mtibwa na kuwafanya  kucheza mpira wa kutumia nguvu. 
Christopher aliiandikia tena Simba bao la pili katika dakika ya 52, akimalizia krosi ya Rashid Ismail, kabla ya Mtibwa kusawazisha katika dakika ya 56 kupitia Kisiga aliyepiga shuti kali nje ya 18 na kumshinda kipa wa Simba. 
Simba ilipachika bao la tatu katika dakika ya 66 likipachikwa na Haruna Athuman mara baada ya kuwatoka mabeki  wa Mtibwa, kabla  Hassan Seif kuitumia safu faulo na kusawasazisha katika dakika ya 73. 
Dakika 90 za mchezo huo ambao ulishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dh.Fenella Mukangara ambaye alikuwa mgeni rasmi,zilimazika kwa timu hiyo kwenda sare ya mabao 3-3 hivyo mwamuzi kuongeza dakika 30. 
Alikuwa ni Christopher tena ambaye aliifungia Simba bao la ushindi katika dakina ya 102 alipomalizia kazi safi ya ia  kazi safi ya Frank Sekule na kufanya bao hilo lidumu hadi dakika ya 120 na kuifanya Simba kushinda kwa mabao 4-3. 
Kwa ushindi huo, Simba imepata milioni 40 pamoja na medali , huku Mtibwa ikiondoka na shilingi mil 20 pamoja na medali. 
Aidha, shujaa wa Simba Christopher alizawadiwa sh milioni mbili kwa kuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao 7, huku kipa wa Simba Abuu Hashim alizawadiwa sh milioni 2.5 kwa kuwa mchezaji bora. 
Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi Agosti 8 na kuzishirikisha pia timu za Simba, Mtibwa Sugar, Azam Fc,Polisi Morogoro kwa upande wa Bara, huku Visiwani iliwakilishwa na  Mafunzo ,Zimamoto, Mtende na  Super Falcon. 
Simba:Abuu Hashim, William Lucian, Omary Salum, Hassan Isihaka, Hassan Hatibu, Said Ndemla, Haruna Athuman, Abdallah Seseme, Rashid Ismail, Edward Christopher na Ramadhan Singano/Fank Sekule. 
Mtibwa Sugar:Shaban Kado, Malika Ndeule, Yusuf Mguya, Salum Swedy, Salvatory Ntebe, Babu Ally, Jamal Mnyate, Awadh Juma, Juma Javu, Shaban Kisiga/Hassan Seif na Vicent Barnabas.
source; mitandao..

Labels: ,

Sunday, August 12, 2012

LEO NDIO LEO LIGI KUU UINGEREZA..

MSIMU mpya wa Ligi Kuu England, unaanza leo kwa mechi ya Ngao ya Jamii, kati ya mabingwa Manchester City dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Villa Park.Mara nyingi, mashabiki husema timu inayoibuka na ushindi kwenye mchezo huo wa Ngao ya Jamii, ndiyo ambayo huja kuwa bingwa wa Ligi Kuu.
Lakini msimu uliopita hali ilikuwa tofauti, kwani Manchester United pamoja na kushinda dhidi ya Manchester City, walishuhudia taji la Ligi Kuu likiwaponyoka siku ya mwisho na kwenda City.
United ilitwaa taji la mechi hiyo ya ufunguzi wa ligi baada ya kuwa nyuma kwa mabao mawili dhidi ya City kabla ya kuibuka na ushindi.
Makocha wa timu zote mbili, leo wanatarajia kupanga vikosi kamili ili kutengeneza mazingira mazuri ya mwanzo wa ligi inayotarajia kuanza Agosti 18 mwaka huu.

Labels: ,

Friday, August 3, 2012

HATIMAYE MRISHO NGASSA AKABIDHIWA JEZI NAMBA 16 NAKUANZA MAZOEZI LEO..

Mchezaji mpya wa timu ya Simba, Mrisho Khalfan Ngassa hivi leo asubuhi ameonekana akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa timu ya Simba.
Bongomixx ilimfuatilia kwa ukaribu nakugundua kuwa, mrisho Ngassa akiwasili na Gari yake ambayo alipewa kama aina mojawapo ya uhamisho kutoka timu ya Azam ambayo alikuwa akiichezea hapo awali.
Mchezaji mpya wa timu ya Simba, Mrisho Ngassa (kushoto) akitoka mazoezini hivi leo asubuhi.



Mrisho Ngassa akiwa ndani ya gari yake aliyokabidhiwa na timu ya Simba.
                                                                       
                                                                    

Labels: ,

Thursday, August 2, 2012

EMMANUEL OKWI HATIMAYE AMEFUZU KUCHEZA ULAYA..

Aliyekuwa mchezaji hatari wa timu ya Simba, Emmanuel Okwi.
      
Bongomixx imefanikiwa kupata taarifa juu ya aliyekuwa mchezaji hatari wa timu ya Simba sports club  Emmanuel Okwi kuwa amefuzu majaribio yake ya kucheza mpira katika timu ya FC Red Bull Salzburg ya Austria na inasubiriwa majadiliano ya uhamisho wake na Klabu yake ya sasa Simba Sports Club. Bado haijajulikana Simba watavuta dau gani kutokana na kumuuza Okwi tutakujulisha habari zaidi zikipatikana..

Labels:

Wednesday, August 1, 2012

AZAM WAMTIMUA KOCHA WAO..

Aliyekuwa kocha wa timu ya Azam Fc Stewart Hall




                                                                                     

Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa kuwa mkataba wake na kocha Stewart John Hall kutoka nchini uingereza ulisitishwa rasmi jana Tarehe 31/07/2012 kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Klabu ya Azam FC inajivunia mafanikio ya kocha Stewart Hall, na inampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya katika muda wote aliofanya kazi kama kocha mkuu na mkurugenzi wa ufundi.
Chini ya Stewart Hall, Azam FC ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi Cup, Kushika nafasi ya pili katika ligi kuu, Mashindano ya Urafiki na Kombe la kagame. Haya ni mafaniko ambayo hayajawahi kufikiwa na makocha wote waliotangulia na ni mafaniko ya kihistoria katika klabu ya Azam FC.
Azam FC inamtakia kocha Stewart Hall kila la heri, na inatarajia kuwa ipo siku katika siku za usoni kocha Stewart atarudi tena kufanya kazi na Azam FC.
Stewart Hall anaacha changamoto kubwa sana kwa mrithi wake ambaye atatangazwa hapo baadaye lakini kizuri ni kuwa, mrithi wa Stewart Hall atakuwa ni mwalimu anayefuata mfumo ule ule wa uchezaji ulioachwa na Stewart Hall kwani hiyo ndiyo (Playing Philosophy ya Azam FC)
Kwa sasa timu itakuwa chini ya Vivek Nagul na Kally Ongala
Imetolewa na Utawala
Azam FC

                                      

Labels:

Monday, July 30, 2012

AZAM WATOA TAMKO... WAMUACHIA NGASSA KWENDA SIMBA!!!


Bongomixx imelipata tamko rasmi la azam kuhusiana na sakata la mchezaji wao anayeonesha mapenzi ya wazi na yanga ambayo ndio mabingwa wa kagame cup
Club ya azam yatoa tamko kuhusu ngasa kupitia ukurasa wao wa facebook "Azam FC
Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa rasmi kuwa baada ya baada ya mchezaji wetu Mrisho Ngasa kuonesha wazi kuwa na mapenzi na Yanga kwa kuivaa na kuipiga busu Logo ya Yanga, tuliwapa Yanga nafasi ya upedeleo ya kumnunua lakini hadi leo hakuna ofa iliyokuja toka Yanga. simba wametoa ofa na uongozi unatafakari ofa ya Simba
Yanga.... Ngasa anauzwa $50,000 wadau wa Yanga tunajua mnampenda sana Ngasa... fikisheni ujumbe kwa uongozi wenu...."
SOMA HAPA UONE MATUKIO YANAYOMHUSISHA NGASSA NA KURUDI YANGA...

                                                          

Labels:

Thursday, July 26, 2012

HAMIS KIIZA AIPELEKA YANGA FAINALI..

Photo: Wanajeshi wa APR ya Rwanda kwa mara ya pili mfululizo wameshindwa kucheza kwata Jangwani baada goli pekee la Hamis Kiiza lililofungwa dakika za nyongeza kuipeleka Yanga fainali ya kombe la Kagame. Hongera sana Wanajangwani.

Labels:

Tuesday, July 24, 2012

PICHA MBALIMBALI SIMBA ILIVYOPIGWA BAO 3 NA AZAM..NAZI ILIYOVUNJWA NA SIMBA HII HAPA


Shujaa wa leo, John Bocco 'Adebayor''

Na Andy Ryn 
AZAM imefuzu kuingia Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada ya kuifunga Simba SC mabao 3-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii na sasa itamenyana na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) keshokutwa.
Shujaa wa Azam leo alikuwa John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyefunga mabao yote hayo, moja kipindi cha kwanza na mengine kipindi cha pili.
Lakini japokuwa Bocco aliondoka na mpira leo, lakini nyota wa mchezo anastahili kuwa Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr’, ambaye alitawala sehemu ya kiungo na kuiongoza vema timu yake hata ikapata ushindi huo mnono.
Bocco, mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, alifunga bao la kwanza dakika ya 17, akiunganisha krosi ya nyota kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tcheche, wakati bao la pili alifunga dakika ya 46, baada ya kupewa pasi na Sure Boy na la tatu alifunga dakika ya 73.
Kabla ya Bocco kufunga bao la kuununua mpira uliotumika katika mechi ya leo, Shomari Kapombe kwa juhudi zake binafsi aliifungia Simba bao la kufutia machozi dakika ya 53.
Ikumbukwe jana APR na Yanga zilikuwa za kwanza kujikatia tiketi ya Nusu Fainali, baada ya kuzitoa Mafunzo na URA.
Katika Robo Fainali ya tatu leo, AS Vita imeingia Nusu Fainali, baada ya kuifunga Atletico kwa mabao 2-1. Taddy Etekiama aliifungia Vita dakika ya sita na Pierre Kwizera akasawazisha dakika ya 48, kabla ya Basilua Makola kufunga la ushindi dakika ya 90+2.
Sasa Nusu Fainali zote zitafanyika keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Azam wakianza na Vita na baadaye Yanga na APR saa 10:00 jioni.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Azam kilikuwa; Deo Munishi, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Michael Balou/Ramadhan Chombo, Kipre Herman Tcheche/George Odhiambo ‘Blackberry’, Salum Abubakar, John Bocco, Ibrahim Mwaipopo na Khamis Mcha ‘Vialli’/Jabir Aziz.
Simba SC; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Shomary Kapombe, Lino Masombo, Juma Nyosso, Mussa Mudde, Uhuru Suleiman/Kiggi Makassy, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Jonas Mkude/A

Bocco akishangilia bao lake

Shangwe za bao

Bocco anadeka baada ya kufunga

Kikosi cha Simba kilichoanza



Kikosi cha Azam kilichoanza

Simba wamevunja nazi hii
ROBO Fainali ya mwisho ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, kati ya Simba SC na Azam FC ndio hivi sasa ni mapumziko, Azam FC inaongoza 1-0, lililofungwa na John Bocco ‘Adebayor’ kwa kichwa akiunganisha krosi ya Kipre Tcheche dakika ya 17.
Katika Robo Fainali ya tatu leo, AS Vita imeingia Nusu Fainali, baada ya kuifunga Atletico kwa mabao 2-1. Taddy Etekiama aliifungia Vita dakika ya sita na Pierre Kwizera akasawazisha dakika ya 48, kabla ya Basilua Makola dakika ya 90+2.
Angalia vikosi vya Simba na Azam.
Azam FC; Deo Munishi, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Michael Balou, Kipre Herman Tcheche, Salum Abubakar, John Bocco, Ibrahim Mwaipopo na Khamis Mcha ‘Vialli’.
Benchi; Mwadini Ally, Waziri Salum, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, George Odhiambo, Mrisho Ngassa, Jabir Aziz, Gaudence Mwaikimba, Joseph Owino na Samir Hajji Nuhu.
Kocha Stewart Hall (Uingereza)
*********
Simba SC; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Shomary Kapombe, Lino Masombo, Juma Nyosso, Mussa Mudde, Uhuru Suleiman, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Jonas Mkude.
Benchi; Hamadi Waziri, Obadia Mungusa, Danny Mrwanda, Salum Kinje, Amri Kiemba, Kiggi Makassy, Amir Maftah, Abdallah Juma na Kanu Mbivayanga.
Kocha; Milovan Cirkovick (Serbia).

MECHI YA KWANZA;
AS Vita; Lukong Nelson, Ilongo Ilifo, Issama Mpeko, Ebunga Simbi, Mapuya Lema, Mfongang Alfred, Ngudikama Emmanuel, Magola Mapanda, Mutombo Kazadi, Lema Mubidi na Etikiama Taddy.
Benchi; Matadi Mankutima, Tshimanga Mutamba, Ngoyi Emomo, Kasereka Thierry, Basilua Makola, Niemba Nkanu, Pambani Makiadi, Romaric Rogombe na Tchomba Musikila.
Kocha; Raoul Shungu
Etikiama Taddy, anayeongoza kwa mabao sasa (6)
**************
Atletico; Said Ndikumana, Francis Nongwe, Etienne Karekezi, Hassan Hakizimana, Emery Nimubona, Pierre Kwizera, Gael Duhayindavyi, Claude Nahimana, Henry Mbazumutima, Didier Kavumbagu na Chalstone Ndayishimye.
Benchi; Innocent Mbonihanuvye, Olivier Nduwimana, FredrcikNsabiyumva, Kevin Ndayisenga, Hussein Ciza, Divin Gateretse, Chrsitian Mbirizi, Sadik Majaliwa na Tressor A Ndiyonkuru.
Kocha; Kaze Cedrick.

Labels:

Thursday, July 19, 2012

Liverpool waafikiana kutoa £10M kupata saini ya Dempsey






Liverpool wanakaribia kuafikiana na Fulham FC juu ya usajili wa mchezaji wa kimataifa wa marekani Clint Dempsey.
Mchezaji huyo ana rekodi nzuri ya ufungaji katika klabu yake ya Fulham na timu ya taifa ya MArekani na aliwahi kufunga Goli lililoipatia droo Marekani dhidi ya Engaland katika fainali za kombe la Dunia.
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anataka kuongeza nguvu ya kikosi chake hasa katika nafasi ya ushambuliaji kutokana na Suarez kutokuwa na msaidizi na Carroll kushuka kiwango.
Dempsey mwenye miaka 29 karibuni anataegemewa kuonekana Merseyside karibuni kukamilisha taratibu za uhamisho.

Labels: ,

AmaZulu 0 -1 Man United

Dimitar Berbatov with Shinji Kagawa after the match in South Africa on Wednesday
Wachezaji wa timu ya manchester united, kushoto ni Berbatov na kulia ni Kagawa


Manchester United wameibuka na ushindi wa goli moja tu katika mchezo wa kirafiki uliochezwa huko Afrika ya Kusini.Mechi hiyo ilichezwa pia kwa kusheherekea siku ya kuzaliwa Nelson Mandela.
Goli hilo pekee la Man United lilifungwa na mchezaji aliesahaulika kikosini hapo Dimitar Berbatov katika dakika ya 20 kipindi cha kwanza.
Kikosi cha United: Lindegaard; Veseli (Vermijl 46), Wootton, Ferdinand, Brady (Blackett 58); Carrick, Scholes (Tunnicliffe 70), Lingard (Petrucci 70); Hernandez (Kagawa 89), Berbatov, Macheda (Anderson 58).

Labels: ,

KOCHA APR AZIPONDA SIMBA NA YANGA

Kocha wa timu ya APR  Ernest Brandits
Kocha wa APR, Ernest Brandits ameziponda Simba na Yanga kwa kusema si lolote kama alivyokuwa anazisikia. Alisema kuwa awali walikuwa wanazihofia sana timu hizo kuwa zitakwamisha harakati zao za kutwaa ubingwa lakini baada ya kuziona wamegundua kuwa zinaudhaifu.
Alianza kuzichambua timu hizo kwa kuanza na Simba akisema, inacheza vizuri lakini washambuliaji wao hawana uwezo wa kufunga magoli.
Kwa upande wa Yanga amesema wanachoka haraka hasa kipindi cha pili, ambacho ni kikwazo kitakachowafanya washindwe kutetea ubingwa wao.
APR ilianza michuano hii kwa kishindo kwa kuibamiza Wau mabao 7-0, na mchezo unaofuata ikatoka sare (0-0) na Atletico. Ipo katikka kundi C pamoja na Yanga SC.
Yanga itaivaa timu ya APR tarehe 20 katika uwanja wa Taifa.

Labels: ,

Sunday, July 8, 2012

KASEBA APEWA USHINDI, CHEKA AGOMA KUPIGANA..

Lile pambano la kukata na shoka kati ya bondia maarufu na mkali hapa bongo Japhet Kaseba na mkali mwingine kutoka Morogoro Francis Cheka jana halikufanyika baada ya Francis Cheka kukataa kuingia ndani ya uwanja kupigana na kumwamulu refarii ampe ushindi Kaseba.




Bondia Francis Cheka akitoka nje ya ulingo baada ya kugoma kupigana jana.


Labels:

Saturday, July 7, 2012

Emanuel Okwi mchezaji halali wa Simba kisheria...


MCHEZAJI EMMANUEL OKWI NI MCHEZAJI WA SIMBA KISHERIA


 Makamu mwenyekiti wa timu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu akizungumza na mchezaji wake Emmanuel Okwi kwa njia ya simu  kutoka  nchini Uganda huku waandishi wa habari wakifuatilia mazungumza hayo.
Makamu mwenyekiti wa timu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu akionyesha mktataba wa timu ya Simba na mchezaji Emmanuel Okwi mbele ya waandishi wa habari
WAKATI Mshambuliaji Emmanuel Okwi amekanusha kusaini Yanga, uongozi wa klabu yake, Simba umesikitishwa na habari zilizovumishwa kwenye vyombo vya habari kuhusu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda kujiunga na wapinzani wa jadi, Yanga SC.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makamo makuu ya klabu Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema kwamba habari hizo hazina ukweli wowote, ni kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na zina lengo la kupotosha ukweli na kuwanyima raha wale wote wenye mapenzi mema na Simba.
“Gazeti kama la Spoti STAREHE limekwenda mbali zaidi kwa hatua yake ya kutaka kuufitinisha uongozi na wapenzi na wanachama wake kwa kudai kuwa uongozi unafikiria tu kumuuza Okwi bila ya kuangalia mkataba wake.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, mkataba wa Okwi umemalizika leo na ndiyo maana ameamua kusaini Yanga akiwa mchezaji huru,”alisema Kaburu na kuongeza;.
“Ukweli ulivyo. Emmanuel Okwi alisaini mkataba mpya wa kuichezea Simba mnamo mwaka jana na mkataba huo unamfanya kuwa mchezaji halali wa klabu yetu hadi mwaka 2013. Baada ya mkutano huu, nitawaonyesha waandishi nakala ya mkataba wa Okwi na Simba. Hivyo taarifa kwamba mchezaji huyo hana mkataba na Simba ni za uongo, uongo mtupu,”alisema.
“Hivi ninavyozungumza nanyi, Okwi yuko kwao nchini Uganda akishughulikia viza ya kwenda nchini Italia ambako anatarajiwa kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika moja ya vilabu vya Ligi Kuu ya Italia (Serie A),”alisema Kaburu.

Labels: