Wednesday, August 29, 2012

Magazeti Leo Jumatano Tarehe 29.08.2012















Labels: ,

Friday, August 24, 2012

Magazeti Leo Jumamosi Tarehe 25.08.2012












Labels: ,

Tuesday, August 21, 2012

BI KIDUDE (FATMA BINTI BARAKA) ANA HALI MBAYA


 



Taarifa kutoka Zanzibar zinadai kuwa mwanamuziki mkongwe wa Taarab nchini Bi. Kidude anaumwa na hana msaada wowote.
Inadaiwa kuwa mjukuu wake alizungumza na televisheni ya Zanzibar na kulalamika kuwa bibi yake hana msaada na hivyo kumuuguza kwa shida.
Taarifa zaidi zinasema Bi. Kidude anaumwa tangu wiki iliyopita.na hana mdau hata mmoja wa muziki aliyejitokeza kumsaidia hivyo natoa wito kwa wadau wenye uwezo wajitokeze kumsaidia bi kidude ili apate matibabu na arejee katika hali yake ya kawaida.

Labels: ,

DR KAFUMU (CCM) AVULIWA UBUNGE NA MAHAKAMA IGUNGA




MAHAKAMA KUU ya Kanda ya Tabora leo imemvua rasmi ubunge, Dk Peter Kafumu, aliyekuwa Mbunge wa Igunga kupitia Tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya mlalamikaji Joseph Kashindye aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Tiketi ya Chadema kufungua kesi dhidi ya Peter Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.
Katika shauri hilo, hoja 15  ziliwasilishwa na wakili wa upande wa mlalamikaji Profesa  Abdalla Safari ikiwamo anayodai kwamba Waziri wa Ujenzi  John Magufuli alifanya mkutano wa kampeni Kata ya Igulubi wilayani Igunga kutumia madaraka yake kuahidi ujenzi wa Daraja la Mbutu kama wananchi hao watampigia kura mgombea wa chama mapinduzi.

Pia Safari anadai waziri huyo aliwatisha wananchi wa kata hiyo kwamba wasipo ichagua CCM daraja hilo halitajengwa na kwamba pia aliwatisha wananchi hao kuwa wasipomchagua Dk Kafumu watashughulikiwa.
Profesa Safari alidai  Baraza la Waislamu (Bakwata) Wilaya ya Igunga liliwakataza waumini wasiipigie kura Chadema  na kwamba naye Rais mstaafu, Benjamini Mkapa alitoa ahadi ya kugawa mahindi kwa wananchi wa Igunga siku moja kabla uchaguzi ili waichague CCM.

Labels: ,

Monday, August 20, 2012

MTOTO WA AJABU AZALIWA TANZANIA..





Habari Leo jumatatu wapendwa wa blog yetu ya bongomixx.
MAAJABU yametokea kwa msichana mkazi wa kijiji cha Mpasa mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi mkoani Rukwa, kujifungua mtoto asiye wa kawaida baada ya ujauzito wa zaidi ya miaka mitatu

Mtoto aliyekuwa kivutio na gumzo kijijini hapo na kwingineko, alizaliwa Agosti mosi, akiwa na meno 32 ambayo ni idadi ya mtu mzima na nywele zenye mvi utosini huku mzazi Lucia Sabastiano (18) akidai kuwa hakuwahi kukutana kimwili na mwanamume yeyote maishani mwake.

Mtoto huyo ambaye alifariki dunia baada ya siku mbili, alikuwa wa kiume, huku pia akiwa na sehemu za siri zilizokomaa kama za mtu mzima ambazo zilikuwa na nywele ndefu sehemu hizo.
Maumbile mengine ambayo yalionekana kuwa ya ajabu ni pamoja na midomo kuwa myekundu, mikono na miguu yenye kucha ndefu na viungo vingine vikionekana sawa na vya mtu mzima.
Akizungumzia tukio hilo jana, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mpasa, Privatous Maliyatabu alisema msichana huyo ambaye alipata ujauzito huo akiwa mwanafunzi wa darasa la tano, alijifungua saa 10 alasiri nyumbani kwa mjomba wake aliyetajwa kwa jina moja la Mwelela.
Maliyatabu alisema Lucia alijifungua kwa msaada wa mkunga wa jadi aliyejulikana pia kwa jina moja la Mama Pashaa, baada ya kupewa dawa ya kunywa na mganga wa jadi, Maneti Mazimba.
Kwa mujibu wa Lucia, licha ya kupata ujauzito huo, bila kukutana kimwili na mwanamume maishani mwake, alidai kutojua jinsi alivyopata ujauzito huo na kudumu nao miaka mitatu.
“Nakumbuka siku moja nilisimama mlangoni mwa nyumba yetu na ghafla nikaona kama mwujiza, mwanga mkali mbele yangu na kisha kujitokeza sura ya mwanaume ambaye siwezi kuhadithia umbile lake na akatoweka na tangu hapo, nilianza kuhisi tumbo kujaa na kuhisi kiumbe kikicheza,” alidai Lucia.
Baadaye aliwaeleza wazazi wake ambao walimpeleka hospitali baada ya kuona tumbo lake linaongezeka siku hadi siku, lakini kwa nyakati tofauti Lucia alipimwa katika hospitali tofauti na kuambiwa hakuwa na ujauzito.
Alisema:“Kila waliponipima waliniambia kuwa sina mimba, lakini miye nilikuwa nikihisi kitu kama mtoto kinacheza tumboni kwa kipindi chote cha miaka mitatu, hali hiyo ilizidi kunishangaza.
Mmoja wa ndugu wa Lucia ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema wana uhakika ndugu yao hajawahi kukutana na mwanamume maishani mwake na familia nzima ilishangazwa na ujauzito wake.
“Lucia ni miongoni mwa watoto watatu katika tumbo la mama yetu, na amekuwa akitushangaza kwa yaliyokuwa yakimtokea tangu apate ujauzito huu, kwani mara nyingi usiku amekuwa akiweweseka, hali iliyofanya tuanze kuhangaika naye kwa waganga wa jadi baada ya hospitali kutueleza kuwa hana kitu tumboni,” alisema mwanandugu huyo aliyejitambulisha kuwa ni dada yake.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk Emmanuel Mtika alisema kitaalamu ujauzito unatakiwa kuwa kati ya wiki 38 na 40 na ikizidi sana wiki 42 hadi kujifungua na kuongeza kuwa hakuna ujauzito wa miaka mitatu.
“Inawezekana huyu mwanamke alikuwa na matatizo ya uvimbe tumboni kwa muda mrefu na akapata ujauzito wa muda wa kawaida ihali yeye akiamini kuwa alikuwa mjamzito kwa kipindi kirefu kumbe sivyo,” alisema Dk Mtika.
Alisema kinachoshangaza ni maelezo ya kudai kuwa mjamzito bila kukutana na mwanamume, kwani hakuna mwanamke anayeweza kupata ujauzito kwa hali hiyo.
“Inawezekana kuna mwanamume alitaka kufanya naye mapenzi kwa nguvu, lakini hakufikia sehemu mwafaka na labda mbegu za kiume zilimwagika karibu na sehemu zake za siri na kumwingia, hapo uwezekano wa kupata ujauzito upo,” alisema Daktari.
Hata hivyo, Dk Mtika alisema mwanamke huyo hakwenda hospitali kubwa kupata vipimo ili kubaini tatizo lililokuwa likimsumbua kwa kipindi chote hicho.

Labels: ,

Saturday, August 18, 2012

SIMBA BINGWA BANC ABC SUP8R CUP 2012



TIMU ya Vijana ya Simba ‘Simba B’  leo imedhihirisha ubora wake baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kwanza ya Banc ABC Sup8r  baada ya kuibamiza Mtibwa Sugar mabao 4-3. 
Katika mchezo huo wa fainali uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ilionekana kutawala kila idara katika mchezo huo ambapo vijana hao waliwahenyesha wapinzani waoMtibwa. 
Edward  Christopher ndiye alianza kuiandikia Simba bao la kwanza katika dakika ya 12 alipoitendea haki pasi ya Haruna Athuman  na kumuuza kipa wa Mtwiba, Shaban Kado langoni mwake. 
Dakika ya 32 Shaban Kisiga aliisawazishia  Mtibwa kwa bao la mkwaju wa penalty  ambapo mwamuzi Hashim Abdallah kuamuru hivyo kutokana na mchezaji wa Simba  Omary Salum kumchezea vibaya Jamal Mnyate wa Mtibwa.Bao hilo lilidumu hadi timu hizo zibnakwenda mapumziko. 
Kipindi cha pili kilianza kwa timu kucheza kwa umakini huku   Simba wakicheza mpira wa akili na kuwachosha wakata miwa hao wa Mtibwa na kuwafanya  kucheza mpira wa kutumia nguvu. 
Christopher aliiandikia tena Simba bao la pili katika dakika ya 52, akimalizia krosi ya Rashid Ismail, kabla ya Mtibwa kusawazisha katika dakika ya 56 kupitia Kisiga aliyepiga shuti kali nje ya 18 na kumshinda kipa wa Simba. 
Simba ilipachika bao la tatu katika dakika ya 66 likipachikwa na Haruna Athuman mara baada ya kuwatoka mabeki  wa Mtibwa, kabla  Hassan Seif kuitumia safu faulo na kusawasazisha katika dakika ya 73. 
Dakika 90 za mchezo huo ambao ulishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dh.Fenella Mukangara ambaye alikuwa mgeni rasmi,zilimazika kwa timu hiyo kwenda sare ya mabao 3-3 hivyo mwamuzi kuongeza dakika 30. 
Alikuwa ni Christopher tena ambaye aliifungia Simba bao la ushindi katika dakina ya 102 alipomalizia kazi safi ya ia  kazi safi ya Frank Sekule na kufanya bao hilo lidumu hadi dakika ya 120 na kuifanya Simba kushinda kwa mabao 4-3. 
Kwa ushindi huo, Simba imepata milioni 40 pamoja na medali , huku Mtibwa ikiondoka na shilingi mil 20 pamoja na medali. 
Aidha, shujaa wa Simba Christopher alizawadiwa sh milioni mbili kwa kuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao 7, huku kipa wa Simba Abuu Hashim alizawadiwa sh milioni 2.5 kwa kuwa mchezaji bora. 
Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi Agosti 8 na kuzishirikisha pia timu za Simba, Mtibwa Sugar, Azam Fc,Polisi Morogoro kwa upande wa Bara, huku Visiwani iliwakilishwa na  Mafunzo ,Zimamoto, Mtende na  Super Falcon. 
Simba:Abuu Hashim, William Lucian, Omary Salum, Hassan Isihaka, Hassan Hatibu, Said Ndemla, Haruna Athuman, Abdallah Seseme, Rashid Ismail, Edward Christopher na Ramadhan Singano/Fank Sekule. 
Mtibwa Sugar:Shaban Kado, Malika Ndeule, Yusuf Mguya, Salum Swedy, Salvatory Ntebe, Babu Ally, Jamal Mnyate, Awadh Juma, Juma Javu, Shaban Kisiga/Hassan Seif na Vicent Barnabas.
source; mitandao..

Labels: ,

Friday, August 17, 2012

Rufaa Ya Lema Tarehe 20 Sept



RUFAA ya kupinga kuvuliwa ubunge ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), imepangwa kusikilizwa Septemba 20, mwaka huu, mbele ya majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa; Natalia Kimaro, Mbarouk Salim Mbarouk na Salumu Massati.
Kwa mujibu taarifa za kikao cha Mahakama ya Rufaa cha Arusha, rufaa hiyo iliyofunguliwa na Lema akipinga uamuzi uliotengua ubunge wake kufuatia shauri lililofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, inatarajiwa kusikilizwa kwa siku moja ambapo baada ya hapo itapangwa tarehe kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.

Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.

Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Katika madai mengine, Lema anamlalamikia, Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa, alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Lema anadai kuwa, Jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

Kesi hiyo iliyotengua ubunge wa Lema, ilifunguliwa na wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, wakidai kuwa wakati wa kampeni mbunge huyo alimdhalilisha mgombea mwezake, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.

ANGALIZO
Jaji Mbarouk Salim Mbarouk ni yule aliyeonekana kutajwa kwa namna isiyo nzuri kwenye utetezi wa Tundu Lisu au ni mwingine? na kama ni yeye hiyo haitaleta tena kutoridhika iwapo maamuzi hayatakuwa upande wa Lema na Chadema? nini mawazo yenu katika hili? 
Bush Lawayer

Labels: ,

Thursday, August 16, 2012

EXCLUSIVE: "KAMA BUSHOKE AKINIZUNGUA, BASI NAITOA HII MIMBA" - JINI KABULA

Siku chache baada ya kuripotiwa amenasa mimba, mwigizaji anayewakilisha kundi la Scorpion Girls, Mariam Julwa aka JINI Kabula amemtaja mwanaume aitwae Bushoke kama ndio baba wa mtoto wake.

"Hii ni mimba ya miezi minne sasa, kama Bushoke hatakuwa na usumbufu wowote basi nitamzalia mtoto mzuri ambaye atatamba nae mitaani, lakini akinizingua, wakati wowote sikawii kubadilisha mawazo na kuichoropoa"

Labels: ,

Sunday, August 12, 2012

MNYIKA : CCM WANA UZUSHI WA KIJINGA KUWA CHADEMA IMEPEWA MABILIONI NA NCHI ZA NJE..


                                                            Mh. John Mnyika, mbunge wa Ubungo.                                                                          

Kauli ya awali kufuatia madai ya kizushi na kijinga ya CCM kuwa CHADEMA imepewa mabilioni na nchi za nje

Katika mitandao ya kijamii kumesambazwa habari zikimnukuu msemaji wa CCM kutoa madai mbalimbali ya uzushi katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu CHADEMA baada ya CHADEMA kuendelea kutekeleza mikakati na mipango yake ya kuwaunganisha watanzania kupitia falsafa ya ‘nguvu ya umma’ katika kuchangia vuguvugu la mabadiliko (M4C) katika maeneo mbalimbali nchini. Nitatoa tamko kamili na kueleza hatua za ziada baada ya kupata taarifa iliyotolewa kwa ukamilifu, hata hivyo kuhusu madai yaliyokwisha sambazwa kwenye mitandao ya kijamii na CCM nachukua fursa hii kutoa kauli ya awali kama ifuatavyo:


Kuibuka huku kwa CCM na kufanya propaganda chafu ni ishara ya kwamba CCM inaumizwa na namna ambavyo watanzania wanajitokeza kuunga mkono CHADEMA kwa hali na mali hivyo CCM sasa inatapatapa kujaribu kudhibiti wimbi la mabadiliko kwa kutumia siasa chafu. Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete anapaswa kueleza watanzania iwapo mikakati hiyo michafu ina baraka zake na za serikali anayoiongoza kwa kurejea pia madai yaliyotolewa na Waziri wa Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Steven Wassira kuwa CHADEMA itasambaratishwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa mbinu mbalimbali.

CCM kwa kuwa imekuwa na kawaida ya kufanya usanii kuhalalisha fedha haramu kama ilivyofanya kwenye chaguzi zilizopita baada ya viongozi waandamizi wa CCM na makada wake kuchota fedha za chafu kifisadi kama zile za kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na vyanzo vingine vichafu na kuzisafisha kupitia harambee za hadaa zilizofanywa na CCM kwa nyakati mbalimbali; inataka kuichafua CHADEMA inayopata fedha kutoka vyanzo halali kwa njia za wazi ili kukatisha tamaa umma wa watanzania unaochangia vuguvugu la mabadiliko.

Viongozi wa CCM wameamua kujidanganya, kuidanganya Serikali yao na kujaribu kuwapotosha watanzania lakini CHADEMA inatambua kwamba watu wachache wanaweza kudanganyika kwa muda mchache lakini si watu wote wakati wote; na kwamba watanzania wa leo kwa uwingi wao hawawezi kudanganyika na uzushi wa kijinga wa CCM.

Ni ukweli ulio wazi kwamba CHADEMA imekuwa ikifanya harambee kwa uwazi kwa nyakati mbalimbali katika kumbi na katika mikutano ya hadhara ikiwemo ya vijijini ambapo michango hutolewa kwa uwazi, aidha michango kwa njia ya simu inaweza kufuatiliwa na kuthibitisha bila shaka yoyote kwamba watanzania wameamua kuchangia mabadiliko ya kweli.

Madai ya CCM kuwa CHADEMA imepokea au itapokea mabilioni ya shilingi kutoka mataifa ya nje ni ya uzushi na narudia kwa mara nyingine tena kuitaka CCM itaje majina ya serikali, taasisi ama makampuni ya nje ambayo CCM inadai kwamba CHADEMA imepokea mabilioni ya shilingi katika siku za karibuni au inatarajia kupokea.

Badala ya CCM kuisingizia CHADEMA ilipaswa CCM ieleze watanzania orodha ya vigogo wa Serikali inayoongozwa na wanachama waandamizi wa CCM ambao wanaelezwa kuwa na akaunti nchini Uswisi na nchi zingine wakituhumiwa kupewa fedha za kifisadi kutoka kwa makampuni ya utafutaji wa mafuta, gesi asili pamoja na uchimbaji wa madini.

CCM ilipaswa ieleze watanzania sababu za kuendelea kusuasua kujivua magamba ya ufisadi kinyume na maazimio ya CCM yaliyofikiwa baada ya msukumo wa CHADEMA kutaja orodha ya mafisadi kwa kuwa kati ya mafisadi hao ni pamoja na viongozi wa CCM walioiingiza nchi katika mikataba mibovu.

Ikumbukwe kwamba madai haya si mapya kutolewa na CCM, yaliwahi kutolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Sophia Simba mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 akidai kuwa CHADEMA imepokea fedha kutoka mataifa ya ulaya kwa ajili ya kufanya maandamano ya kuiondoa CCM madarakani.

Itakumbukwa kwamba wakati huo nilimtaka ataje nchi hizo na kueleza kusudio la kumchukulia hatua zaidi na kwa upande mwingine niliyataka mataifa hayo ya Ulaya yatoe kauli kuhusu madai hayo. Izingatiwe kwamba mataifa hayo yalikanusha madai hayo ya CCM na Sophia Simba mwenyewe alikana kuwa hakuna madai hayo dhidi ya CHADEMA.

Nimeelezwa kuwa CCM imetoa madai mengine ya uzushi kuwa CHADEMA inapewa mabilioni toka nje kwa kuwa nchi imegundua rasilimali za mafuta na gesi na kudai kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kuiweka nchi rehani.

Madai haya yaliwahi kutolewa pia na Katibu wa CCM wa Fedha na Uchumi Mwigulu Nchemba na nikamtaka Waziri wa Mambo ya Nje Benard Membe kutaja nchi hizo na mikataba hiyo hata hivyo mpaka sasa hakuna kiongozi yoyote wa CCM na Serikali aliyejitokeza kutaja CHADEMA imepokea au itapokea mabilioni kutoka nchi gani na kwa mikataba gani.

CCM inatoa madai hayo kuhamisha mjadala baada ya CHADEMA wa uongozi bora, sera makini, mikakati sahihi na oganizesheni thabiti kuwa mstari wa mbele katika kutetea rasilimali za taifa na watanzania kutambua kwamba taifa letu litaepushwa kutumbukia kwenye laana ya rasilimali kwa kuiondoa CCM madarakani katika chaguzi za mwaka 2014 na 2015 na kuichagua CHADEMA.

CCM na Serikali yake ndiyo imekuwa kinara wa kupokea fedha kutoka nje kwa kisingizio cha misaada na kuingia mikataba mibovu na mataifa ya nje pamoja na makampuni ya kigeni na kuachia mianya ya uporaji wa rasilimali za nchi na CHADEMA imeanika hali hii kwenye orodha ya mafisadi kwa kutaja majina ya viongozi waliohusika kwenye mikataba ya madini na tutaendelea kufanya hivyo hata katika masuala ya mafuta na gesi ambayo tayari vigogo wa Serikali inayoongozwa na CCM wameshaanza kuingia mikataba mibovu na kuingiziwa fedha katika akaunti zao za nje ya nchi.

Hivyo, badala ya CCM kutoa madai ya uzushi kuhusu CHADEMA kuingia mikataba na serikali au makampuni ya nje, CCM ieleze watanzania imechukua hatua gani mpaka sasa juu ya viongozi na wanachama wake waliongia mikataba mibovu kwenye rasilimali muhimu nchini ikiwemo madini, mafuta, gesi na maliasili zingine za taifa letu na kutoa mikataba hiyo hadharani ili watanzania waweze kuchukua hatua za kufanya mabadiliko ya kweli.

Hivi karibuni Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM alisema kwamba serikali inayoongozwa na CCM haitarudia makosa ya kuachia mianya ya ufisadi kwenye gesi; hivyo CCM ilipaswa wakati huu kuwaomba radhi watanzania kwa ufisadi uliofanyika kwenye madini na rasilimali nyingine na kuishukuru CHADEMA kwa kuendelea kuwaunganisha watanzania wakati wote kusimamia mabadiliko ya kweli.

CCM badala ya kutishia kuwa ina mikataba inayoihusu CHADEMA ingetoa mikataba hiyo na hali hii ya CCM inayoongoza Serikali kudai CHADEMA kufanya mikakati, mipango na shughuli iliyo kinyume cha sheria bila vyombo vya dola kuchukua hatua ni ishara ya CCM kukiri wazi kuwa chama legelege chenye serikali legelege kimeshindwa kuongoza nchi na badala yake kimejikita katika propaganda chafu.

CHADEMA tangu kuanzishwa kwake imekuwa na makubaliano ya ushirikiano (MOU) bila masharti yoyote na vyama rafiki vya ndani ya Afrika na duniani na makubaliano hayo yamekuwa yakifikiwa kwa uwazi ikiwa ni sehemu ya CHADEMA kuwa na mtandao wa kimataifa na hayajawahi kuhusisha wala hayatawahi kuhusisha CHADEMA kusaidiwa mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kufanya kazi zake kama inavyodaiwa na CCM.

CHADEMA kimekuwa chama kiongozi kwa nyakati mbalimbali kueleza viwango cha matumizi yake ya fedha na vyanzo vya fedha husika huku kikitegemea kwa kiwango kikubwa michango ya wanachama na wapenzi wa chama hapa nchini pamoja na kutumia kwa ufanisi ruzuku inayotolewa kwa vyama vya siasa.

CCM imekuwa na kawaida ya kutoa madai ya uzushi wakati mwingine yakiambatana na kutoa nyaraka za kughushi inazodai kuwa ni za CHADEMA. Ikumbukwe kwamba wakati wa uchaguzi wa mdogo wa Igunga, CCM ilitoa madai ya uzushi kuwa CHADEMA inafadhiliwa na nchi za nje ikiwemo kupewa mafunzo ya ugaidi na kudai kuwa tayari magaidi wameingizwa na CHADEMA toka nje katika uchaguzi huo; hata hivyo katika mwenendo wa kesi ya uchaguzi ya Igunga Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama aliyetoa madai hayo alitoa ushahidi mahakamani kwamba CHADEMA haijawahi kuleta magaidi bali kauli hizo za CCM zilikuwa ni za siasa za uchaguzi.

Hivi karibuni, CCM imeghushi waraka mwingine na kuusambaza kile ilichodai kuwa ni maazimio ya kamati kuu ya CHADEMA ya kupanga migomo ya walimu, madaktari na mipango mingine ya kuhujumu serikali; hata hivyo waraka huo ulidhihirika wazi kuwa ni wa kughushi.

Mikakati yote hiyo michafu hupangwa na CCM mara kwa mara wakati ambapo CHADEMA inaanza operesheni Sangara na mikakati mingine ya kuleta mabadiliko nchini na kujipanga kuiondoa CCM madarakani kama ilivyo sasa ambapo CHADEMA inaendelea na operesheni katika mkoa wa Morogoro hivyo watanzania wanapaswa kuipuuza CCM na kuendelea kujiunga CHADEMA na kuchangia mabadiliko kwa hali na mali mpaka kieleweke.

John Mnyika (Mb)

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

source; mnyika.blogspot.com

Labels: ,

LEO NDIO LEO LIGI KUU UINGEREZA..

MSIMU mpya wa Ligi Kuu England, unaanza leo kwa mechi ya Ngao ya Jamii, kati ya mabingwa Manchester City dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Villa Park.Mara nyingi, mashabiki husema timu inayoibuka na ushindi kwenye mchezo huo wa Ngao ya Jamii, ndiyo ambayo huja kuwa bingwa wa Ligi Kuu.
Lakini msimu uliopita hali ilikuwa tofauti, kwani Manchester United pamoja na kushinda dhidi ya Manchester City, walishuhudia taji la Ligi Kuu likiwaponyoka siku ya mwisho na kwenda City.
United ilitwaa taji la mechi hiyo ya ufunguzi wa ligi baada ya kuwa nyuma kwa mabao mawili dhidi ya City kabla ya kuibuka na ushindi.
Makocha wa timu zote mbili, leo wanatarajia kupanga vikosi kamili ili kutengeneza mazingira mazuri ya mwanzo wa ligi inayotarajia kuanza Agosti 18 mwaka huu.

Labels: ,

Rungu la Dk Mwakyembe latua kwa meneja Tazara

                                                                     

WAZIRI  wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema atamtimua kazi Meneja Mkuu wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara), Abdallah Shekimweri, iwapo atashindwa kusimamia majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuwapa vitendea kazi na posho wafanyakazi wa shirika hilo.
Rungu la waziri huyo lilianza Juni 5, mwaka huu baada ya kutengua uteuzi wa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi na kumteua rubani wa muda mrefu, Kapteni Lusajo Lazaro kukaimu nafasi hiyo.
Mbali na uteuzi huo pia alitangaza kuwasimamisha kazi vigogo wengine wanne wa shirika hilo ambapo baada ya siku chache alianika ufisadi unaodaiwa kufanywa na kigogo huyo.
Lakini jana wakati akiwa katika ziara yake ya kushtukiza katika karakana za Tazara, Dk Mwakyembe alisema kuwa haridhishwi na utendaji kazi wa Shekimweri.
Mbali na kutembelea Tazara, pia alifanya ziara  bandarini na katika ofisi za Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).
Akiwa katika ziara hiyo aliahidi kukutana na uongozi mzima wa Tazara ili kujadili matatizo yaliyopo katika shirika hilo ikiwa ni pamoja na ubovu wa reli, lengo likiwa ni kuyapatia ufumbuzi.
Mmoja wa wasaidizi wake ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini licha ya kuwa alikuwa amembatana na waziri huyo katika ziara hiyo alisema kuwa suala la kumtimua kazi Shekimweri siyo jambo la utani.
“Dk Mwakyembe ameshatuma barua kwa uongozi wa Tazara nchini Zambia, amewaeleza wazi kuwa haridhishwi na utendaji kazi wa (Shekimweri) na yupo tayari kutoa uamuzi, itakuwa kabla ya Oktoba mwaka huu,” alisema  msaidizi huyo na kuongeza;
“Si unajua hili shirika linaendeshwa kwa ubia wa Tanzania na Zambia, hivyo kama unataka kuchukua uamuzi ni lazima upande mwingine uwe na taarifa.”
Dk Mwakyembe alisema haridhishwi na ufanyaji kazi unavyoendelea katika Karakana ya Tazara na kumtaka Shekimweri kuwapa vifaa wafanyakazi hao na iwapo atashindwa kufanya hivyo atalazimika kumfukuza kazi. “Tutafukuzana hapa, watu wapo tayari kufanya kazi ila  wanakwamishwa, mwambieni Shekimweri kuwa nitamfukuza kazi na nitarudi tena Jumatatu (kesho),” alisema Dk Mwakyembe.
 Alisema kuwa ni jambo la ajabu kwa menejimenti ya Tazara kushindwa kutoa fedha kwa watumishi wake wakati Serikali imeshatoa fedha za ukarabati wa mabehewa ya treni yanayotakiwa kuanza kutoa huduma ya usafiri kuanzia Oktoba mwaka huu.
 Dk Mwakyembe alihoji sababu ya menejimenti hiyo kukalia fedha hizo wakati zinapaswa kulipwa kwa wafanyakazi hao wanaoendelea kukimbizana na muda ili kumaliza ukarabati huo. “Fedha mnaziweka makao makuu kwani ni maua hayo? Walipeni watu fedha zao na mnunue vifaa, tutafukuzana hapa na hakuna wa kunilaumu,” alisema Dk Mwakyembe.
Aliitaka menejimenti ya Tazara kukamilisha ukarabati wa mabehewa 14 ambayo aliagiza yafanyiwe ukarabati kwa kuwa mpaka sasa ni mabehewa manne tu ndiyo yanayoonekana kukarabatiwa.
Baadhi ya wafanyakazi waliokuwapo katika maeneo yao ya kazi walimweleza, Dk Mwakyembe kwamba shirika hilo haliwawekei fedha zao za mifuko ya hifadhi ya jamii, suala ambalo waziri huyo aliahidi kulifuatilia kwa ukaribu.
Akiwa katika Karakana ya TRL, Dk Mwakyembe aliridhishwa na utendaji kazi na kusema kuwa mpaka Oktoba mwaka huu treni ya Reli ya Kati itaanza kutoa huduma zake kama ilivyotangazwa.
Katika hatua nyingine, Dk Mwakyembe alisema mashine ya kushusha na kupakia mizigo katika meli karibu itafungwa kwa kuwa ujenzi wa reli kwa ajili ya kusimamisha mashine hiyo unaendelea vizuri.
source: Mwananchi, Jumapili.

Labels: ,

Friday, August 10, 2012

BREAKING NEWS: AJALI TENA..

WATU zaidi ya 11 WAHOFIWA KUFA KATIKA AJALI iliotokea daraja la mto wami alfajili ya jana tarehe 10.
Watu zaidi ya 11 wanahofiwa kufa kufuatia ajali ya mabasi mawili ya abiria yaliyokuwa yakitokea Nairobi nchini Kenya kuja Dar es Salaam.Ajali hiyo inaelezwa kuwa imetokea maeneo ya Daraja la mto Wami alfajiri ya jana Mkoani Pwani. Wadau tunazidi kuzifuatilia taarifa hizi kwa ukaribu,tutazidi kutaarifiana kadiri ya taarifa zitakavyokuwa zinapatika,lakini pia si vibaya kwa mwenye taarifa kamili akatujuza hapa hapa bongomixx.

Labels:

MASTAA BONGO MOVIE WADAIWA KUJIUZA BBM



                                                                                                

BAADHI ya mastaa Bongo wanadaiwa kuwa na tabia ya kutumia mtandao wa simu wa BlackBerry Messenger ‘BBM’ vibaya ikiwa ni pamoja na kujiuza kwa wanaume, Ijumaa limebaini.
Utafiti uliofanywa na mapaparazi wetu umeonesha kuwa, wapo ambao wawapo vyumbani kwao hujipiga picha za utupu na kuzitupia kwenye mtandao huo kisha baada ya muda huzitoa.
Wakizungumzia tabia hiyo, baadhi ya wanaume wanaotumia BBM walikiri kukumbana na picha hizo za ajabu za mastaa huku zikiambatana na maneno ya kujitongozesha kwao.
“Huyu …(anataja jina la staa maarufu Bongo), juzi usiku mishale ya saa nane alianza kunitumia ‘sms’ kuniuliza kama niko macho. Nilipomjibu akaniambia kuna zawadi anataka kunipa, nilivyomkubalia akatupia picha yake akiwa kitandani mtupu.
“Hazikupita hata sekunde nyingi, kabla ‘sijai-download’ akaitoa kisha akaniuliza nimejisikiaje kumuona alivyo. Nilishangaa lakini nikamjibu kwa kifupi kuwa ana mvuto, basi kuanzia siku hiyo akawa ameniganda,” anasema kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Sule ambaye ni mfanyabiashara jijini Dar.
Msanii mwingine wa kiume aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema:
“Mbona huo ndiyo mchezo wao, yaani ukishamkubalia kuwa rafiki yao basi subiri vituko, kwa kifupi sasa hivi wengi wanajiuza kupitia BBM.”
Katika kupata ukweli juu ya habari hiyo, waandishi wetu walizungumza na baadhi ya mastaa wa Kibongo wanaotumia mtandao huo ambapo walikuwa na haya ya kusema:

JACQUELINE PATRICK
Modo huyo mwenye jina kubwa Bongo alifunguka: “Kwa upande wangu siwezi kukataa kuwa sijawahi kuweka picha kama hizo, mimi ni mpenzi sana wa picha na ninaupenda sana mwili wangu hivyo nikipiga picha ya aina yoyote lazima niitupie kwani ‘fansi’ wangu ndiyo wanaoweza kuniambia kama nimenenepa au nimekonda au kunisifia
“Suala la kutongoza wanaume naweza nikasema kuwa mimi siweki kwa sababu hiyo kwani marafiki zangu wote kwenye BBM wana wapenzi wao.”

ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
Mwigizaji huyo ambaye pia ni mwanamuziki alisema: “Mimi sijawahi kumtongoza mwanaume na siwezi kwa sababu mila za kwetu zinasema mwanaume ndiye anatakiwa kumtongoza mwanamke hivyo mwanamke anayemtongoza mwanaume anakosea kwani ataonekana wa bei rahisi sana.
Labda wenzangu wanaweza kufanya hivyo kupitia njia hiyo.”

MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
Mwigizaji huyo alifunguka: “Mimi nina mume wangu, nampenda sana na mara nyingi siingii BBM ila ninauzisha tu picha zangu kule lakini kuchati na watu siyo kivile na siwezi kumtongoza mwanaume kwa sababu wanaume wanaopatikana kwa njia hiyo siyo kabisa labda mastaa wenzangu, lakini mimi sijawahi kumtongoza mwanaume.”

RACHEL HAULE ‘RECHO’
Staa huyo wa filamu alisema: “Sijawahi kumtongoza mwanaume ila suala la kutongozwa na wanaume kwenye BBM ni la kawaida, inategemea na msimamo wa mtu. Najua BBM tumejiunga kwa ajili ya kujua matukio yanayotokea kwa haraka zaidi na siyo kwa ajili ya kujiuza.”

ISABELA MPANDA
Mwigizaji huyo alitiririka: “Katika orodha ya hao wanaojiuza kupitia mtandano huo, mimi simo. Nipo BBM ila sijawahi kumtongoza mtu wala kutupia za utupu.”
RUTH SUKA ‘MAINDA’
Mwigizaji huyo mkongwe alisema: “Ni kweli nimejiunga BBM lakini kwa sasa nipo ‘shouting’ nicheki baadaye.
Mastaa wengine waliotajwa kuwepo BBM nja na waigizaji Aunt Ezekiel, Irene Uwoya, Agnes Gerard ‘Masogange’ na wengineo.

Source: Global publishers

Labels: ,

TAFF YATOA TAMKO JUU YA MAHARAMIA WA FILAMU


                                                                                       


                                                                                
SHIRIKISHO la Filamu nchini(TAFF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) pamoja Kampuni za usambazaji wa filamu na kazi za wasanii ‘wameapa’ kupambana na maharamia wote wa kazi hizo ili kulinda maslahi ya wasanii. Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana, umoja huo kwa pamoja ulisema umefika wakati tatizo la wizi wa kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo ni kero kwa muda mrefu. Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo. “Umefika wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi zao” “Tuna imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri, tutaweza kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu wachache ndiyo wananufaika nayo” alisema Mwakifwamba. Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii. Alisema Serikali inapswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa nchini walioamua kujitoa mughanga kufanya kazi zao.
Kwa upande wake Meneja usimamizi kutoka TRA Msafiri Ndimbo alisema Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia Bunge lake kukubaliana kuweka mikakati ya kupamba na suala hilo.
Ambapo wasanii na wasambazaji wa kazi zao wameungana pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao zinakwenda kwa haki ili wasanii na kazi zao

Labels: ,

HATIMAYE MALAWI YASALIMU AMRI KWA TANZANIA..

Siku chache baada ya Serikali ya Tanzania kupitia kwa waziri wake wa mambo ya nje Mh. Bernad Membe kuitaka Serikali ya Malawi kuondoa majeshi na kampuni zinazofanya utafiti wa gesi kwenye ziwa Nyasa ukanda wa Tanzania wakidai kuwa ziwa hilo ni la kwao lote wameanza kufanya hivyo na kuondoka taratibu ukanda huo. Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro alisema kuwa kwa sasa eneo hilo hali ni shwari kwani

makampuni, ndege na askari wa malawi waliokuwa wakiendesha shughuli zao kwenye eneo la Tanzania wametii amri na kuondoka kwenye eneo hilo hivyo wananchi wasiwe na shaka bali waendelee na kazi zao za kila siku kwenye ziwa hilo, Mbali na Waziri Membe, viongozi wengine waliozungumzia mgogoro huo na

kuitaka Malawi iache uchokozi ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika

Mashariki, Samuel Sitta na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya

Nje, Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa.

Labels: ,

Wednesday, August 8, 2012

KAMPUNI YA STEPS, WASANII, WAKAMATA WEZI WA KAZI ZAO DAR ES SALAAM



Baadhi ya wasanii pamoja na askari polis wakiwa wamerizingira duka lililokuwa linauza kazi za wasanii feki 
BAADHI YA MIZIGO YA DVD MPYA KABISA ZILIZO FEKI ZIKIWA ZIMEKAMATWA LEO JANA JIJINI DAR ES SALAAM
Msanii wa filamu nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto na Jacob Stevin 'JB' wakiwa katika duka ambalo lilikuwa linauza kazi zao ambazo ni feki ambapo walikamatwa kwa kushilikiana na Kampuni ya usambazaji ya Steps Entantainment ya jijini Dar es salaam
MSANII WA MUZIKI WA TAARABU, MZEE YUSUFU KUSHOTO, AKIANGALIA MOJA YA KAZI YAKE ILIYOKUWA FEKI ZILIZOKAMATWA NA WASANII WENYEWE KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTANTAINMENT YA JIJINI DAR ES SALAAM JANA
MSANII MOHAMED NICE 'MTUNISI' AKIZUNGUMZA JINSI WALIVYOKAMATA MZIGO FEKI WA KAZI ZA WASANII MBALIMBALI KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTATAINMET YA JIJINI DAR ES SALAAM INAYOSAMBAZA KAZI ZA WASANII NCHINI
Moja ya gari lililokuwa limejaa kazi feki za wasanii mbalimbali nchini zinazouzwa baada ya kurudufiwa kinyume cha sheria na kukosesha wasanii mapato mazuri.
MSANII KAPTEN RADO AKIKAGUA KAZI ZAKE MPYA AMBAPO KAZI YAKE IJULIKANAYO KAMA 'HATIANI' ILIYOINGIA MTAANI JANA ILIKUWA IMESHACHAKACHULIWA NA KUINGIZWA SOKONI
MSANII MOHAMED 'NICE' AKILIA KWA UCHUNGU BAADA YA KUKUTA KAZI ZAO ZILIZOKUWA ZIKIUZWA KATIKA MOJA YA DUKA MTAA WA MAGILA NA LIKOMA JANA

Labels: ,

NDOA YA WAKE WATATU YAIBUA MENGI..

Mwananume anayedaiwa kuwaoa wake watatu kwa mpiga.
                                                                             
Mwanamme mmoja huko jamhuri ya kidemokrasia ya kongo kafunga ndoa na wanawake watatu kwa mpigo siku moja kanisani. Tukio hilo limetokea wiki iliyopita ambapo pedeshee huyo aliamua kuwapeleka wake waote  watatu kwa mpigo kanisani na kuwafungisha ndoa kwa nia ya kuishi nao pamoja.

Labels:

NAIBU WAZIRI ABUDULLAH JUMA APATA AJALI MBAYA


Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Mhe. Abdullah J Abdallah, amenusuirika katika ajali ya gari leo jioni katika maeneo ya Tumbi – Kibaha wakati akitokea Bungeni Dodoma akielekea Dar.
Ndani ya gari alikuwa pamoja na mkewe na watoto wake ambao wote wamepata majeraha madogo, dereva wake ameumia zaidi na hivyo kulazimika kukimbizwa katika hospitali ya Tumbi.

Labels: ,

EDWARD LOWASSA: TUPO TAYARI KUINGIA VITANI NA MALAWI NA TUMEJIPANGA VIZURI


KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imesema Tanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.

Akizungumza mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Edward Lowassa alisema kamati yake imeridhishwa na maandalizi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

“Tumepewa maelezo na jeshi letu na tumeridhika kuwa ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na limejipanga vizuri sana kwa uhakika, kiakili na kivifaa,” alisema Lowassa.

Kabla ya Lowassa kuzungumza na waandishi wa habari, alifanya kikao cha faragha kilichohusisha pia wajumbe wa kamati hiyo na makamanda wa JWTZ walipofika bungeni kutoa taarifa kwa kamati hiyo.

 
Hata hivyo, katika tamko hilo Lowassa alisema Tanzania inatarajia mgogoro huo utamalizika kwa njia za kidiplomasia kwa sababu Watanzania na Wamalawi ni ndugu wa muda mrefu.

“Ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na kama ilivyo ahadi yao (JWTZ), wako tayari kulinda mipaka ya nchi yetu hadi tone la mwisho. Tunasali sana tusifike hapo,” alisema Lowassa na kuongeza: “Tunategemea hatutafika huko, lakini kwa heshima ya nchi yetu kama ikibidi kufika huko (vitani) tutafika kulinda mipaka yetu”.

Mwenyekiti huyo ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu, alisema kama Tanzania itafikishwa mahali itabidi damu ya Watanzania imwagike, nchi iko tayari kulinda mipaka yake kwa nguvu.


Alisema kama itabidi kuingia vitani, itatumia umoja na mshikamano wa Watanzania wa mwaka 1978 wakati wa Vita na Uganda kulinda mipaka ili kulinda heshima ya nchi.

Alisema mwaka 1978 wakati Rais wa Uganda, Idd Amin na majeshi yake walipochukua sehemu ya Tanzania na kujitangazia ni mali yake, ilichukua hatua kumfukuza Amin.

“Alijitangazia sehemu ile ni mali ya Uganda hutegemei nchi ikae kimya, hutegemei Watanzania wanyamaze wakati nchi yao imetekwa, tulichukua hatua tukamfukuza hadi nchini kwake.”

 
Lowassa alisema Kamati ya Bunge inajua madhara ya kiuchumi yaliyotokana na Vita ya Idd Amin na kwamba vita yoyote ikipiganwa lazima kunakuwa na madhara ya kiuchumi.

Hata hivyo, alisema anaamini mgogoro huo hautafika huko na kusisitiza kuwa, lakini ikibidi JWTZ ni moja kati ya majeshi bora duniani na ni jeshi lililojiandaa vizuri kwa lolote.

 
“Wako tayari sisi ni moja kati ya jeshi lililojiandaa vizuri na jeshi bora duniani na la kujivunia. Tuko imara kiakili na kivifaa tena vya kisasa,” alisema Lowassa.

Alisema kamati yake inaunga mkono msimamo ulitolewa bungeni juzi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuhusu mgogoro huo na kwamba ndiyo kauli rasmi ya Serikali.

 
Juzi, Waziri Membe alizionya kampuni za kigeni za Malawi zilizoingia katika ardhi ya Tanzania eneo la Ziwa Nyasa kutafiti mafuta na gesi kusitisha mara moja.

Akiwasilisha makadirio ya wizara yake, Membe alisema upo ushahidi kuwa ndege tano za utafiti za Malawi ziliruka anga la Tanzania na kutua katika Ziwa Nyasa upande wa Tanzania.Membe alisema pamoja JWTZ kutoruhusu ndege hizo za Malawi kuingia na kutua eneo hilo la Ziwa Nyasa, bado ziliingia na kutua kinyume kabisa cha sheria za kimataifa.

“Wenzetu wa Malawi wanadai Ziwa Nyasa lote lipo Malawi na msingi wa madai yao ni mkataba wa Heligoland wa mwaka 1890 na sisi tunasema mpaka uko katikati ya Ziwa.”

Membe alisema hata mgogoro wa mpaka kati ya Cameroon na Nigeria ulitatuliwa na Mahakama Kuu ya Dunia kuwa mpaka baina ya nchi hizo mbili upite katikati ya Ziwa Chad.

Juzi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Patrick Kabambe alikaririwa na Redio Sauti ya Ujerumani akisema wataendelea na utafutaji mafuta licha ya onyo hilo la Tanzania.

Waziri huyo alisema ziwa hilo linaitwa Malawi na siyo Ziwa Nyasa na kwamba utafutaji wa mafuta na gesi utaendelea na hakuna wa kuwasimamisha. Alihoji, iweje Tanzania ishtuke sasa

Labels: ,