Saturday, August 18, 2012

Roma Mkatoliki,TMK Wanaume Family Jukwaa moja Idd Pili



KWA sasa mambo yanazidi kunoga wakati sikukuu ya Idd El Fitr ikiwa inakaribia, pale kulipoandaliwa burudani ya kufa mtu katika fukwe ya Coco iliyopo Oysterbay, Dar es Salaam siku ya Idd Pili.

Katika burudani hiyo inayoletwa na vinywaji vya Grand Malt na Vita Malt ambavyo havina kilevi, huku wasanii kadhaa wenye majina wakitarajiwa kufanya kweli zaidi.

Kwa mujibu wa Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam alisema, wameamua kuleta burudani hiyo ambayo itakuwa bure kwa kila atakayeshiriki, huku kukiwa na michezo kibao ya kuvutia.

Consolata alisema, wasanii watakaoshiriki katika burudani hiyo ya kufa mtu siku hiyo ni pamoja na Roma Mkatoliki pamoja na kundi za la TMK Wanaume.
Kundi hilo linajulikana kwa jinsi lilivyo na wasanii wakali kama Mheshimiwa Temba, Chege, Aslay, Bibi Cheka na wakali wengine kibao, ambao wote wameapa kutoa burudani ya kufa mtu.

“Unajua vinywaji hivi havina kilevi, hivyo ni vema mtu ukaja na familia yako kwani kutakuwa na michezo ya kila aina pamoja na zawadi kibao,” alisema.

Consolata alisema, burudani hizo za bure zitaanza saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni katika siku hiyo ya Idd Pili.

Labels:

Namna ya kupanga malengo maishani


                                                                                        
Baada ya kuanza kujiuliza na kuyatambua malengo yako huku ukiandika kila wazo linalokujia akilini, fuata hatua zifuatazo:

1. JENGA PICHA AKILINI MWAKO
Jenga taswira ya kitu unachokitaka akilini mwako. Picha unayoijenga lazima iwe kubwa. Fikiria jinsi utakavyokuwa na mafanikio makubwa maishani katika kile ulichochagua kukifanya. Jione tayari ukiwa katika mafanikio ambayo ulikuwa ukiyatamani kwa siku nyingi.

Jitazame furaha utakayokuwa nayo na jinsi utakavyoyamudu maisha ya mafanikio. Panga malengo ya muda mrefu. Usifikirie kuwa ulichokiwaza kitatokea kesho, jipe muda hata wa miaka kumi au zaidi, usiogope kufikiria mambo makubwa yanayohitaji muda mrefu kukamilika. Kuanzia hapo, endelea na hatua ya pili.

2. YARAHISISHE MALENGO YAKO
Yawezekana malengo yako ni makubwa sana kiasi cha kukuzidi. Hiyo isikutishe, yarahisishe malengo yako. Kivipi? Kama malengo yako ni kuwa na mafanikio makubwa maishani baada ya miaka kumi, ugawanye muda wako katika sehemu ndogondogo.

Kwa mfano unaweza kuanza kugawanya miaka kumi kwa mbili, yaani baada ya miaka mitano uwe angalau umefikia nusu ya kile ulichokiwaza awali. Baada ya hapo igawanye miaka mitano kupata mwaka mmoja mmoja.

Jiulize kwa kila mwaka utafanya nini ili kuyakaribia mafanikio. Weka ratiba na mipango yako kwa maandishi. Ugawanye mwaka kupata miezi, jiulize utafanya nini mwezi wa kwanza, wa pili hadi mwaka uishe. Hakikisha unaandika kila kinachokujia akilini.

Endelea kurahisisha malengo yako kwa kujiuliza ndani ya miezi sita utakuwa tayari umefanya nini, shuka mpaka miezi mitatu kisha malizia kwa kila mwezi mmoja. Utaona kwamba lengo unalotarajia kulifanikisha kwa kipindi cha miaka kumi umelirahisisha mpaka kwenye mwezi mmoja.

Usiishie hapo, mwezi ugawanye kwenye wiki, kisha malizia kwenye siku. Jiulize kila siku utafanya nini ili kuelekea kwenye lengo lako kubwa unalotaka litimie baada ya miaka kumi. Hapo utaanza kuona umuhimu wa kutumia muda wako vizuri, hakuna muda wa kupoteza.

3. ANZA UTEKELEZAJI
Anza utekelezaji wa malengo yako mara moja. Hakikisha kila saa inayopita umefanya jambo ili kupalilia malengo yako. Hakikisha unafuata ratiba uliyojipangia, usisubiri mtu mwingine aje kukukumbusha kuhusu malengo uliyoyapanga. Tembea na karatasi au kitabu ulichoandika malengo yako na endelea kujikumbusha kila siku juu ya kile unachotaka kitokee.

Mwanasaikolojia mmoja mashuhuri aliwahi kuandika kuwa: Mafanikio siyo tukio unaloweza kulisubiri litokee bali ni hatua unayochukua kuyafikia. Ukianza kufikiria mafanikio, tayari umeanza kufanikiwa, ukiweza kupanga malengo na kuanza kuyafanyia kazi, tayari umo ndani ya mafanikio.

Usisubiri itokee siku ambayo utalala halafu ukiamka asubuhi ukute yale uliyokuwa unayataka yametokea. Malengo yako lazima yakutese usiku na mchana. Watu wote waliofanikiwa hawakufika hapo kwa bahati, walipanga malengo na wakayafanyia kazi.

MAMBO YA KUZINGATIA KUELEKEA MAFANIKIO
Kwa kuwa maisha ni kama safari na malengo ndiyo dira, ukianza kuyafanyia kazi malengo yako utagundua unatakiwa kufanya nini ili safari yako ya maisha iwe rahisi. Lazima ufahamu mambo muhimu yatakayokusaidia kurahisisha safari yako kuelekea mafanikio.

Labels: ,

SIMBA BINGWA BANC ABC SUP8R CUP 2012



TIMU ya Vijana ya Simba ‘Simba B’  leo imedhihirisha ubora wake baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kwanza ya Banc ABC Sup8r  baada ya kuibamiza Mtibwa Sugar mabao 4-3. 
Katika mchezo huo wa fainali uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ilionekana kutawala kila idara katika mchezo huo ambapo vijana hao waliwahenyesha wapinzani waoMtibwa. 
Edward  Christopher ndiye alianza kuiandikia Simba bao la kwanza katika dakika ya 12 alipoitendea haki pasi ya Haruna Athuman  na kumuuza kipa wa Mtwiba, Shaban Kado langoni mwake. 
Dakika ya 32 Shaban Kisiga aliisawazishia  Mtibwa kwa bao la mkwaju wa penalty  ambapo mwamuzi Hashim Abdallah kuamuru hivyo kutokana na mchezaji wa Simba  Omary Salum kumchezea vibaya Jamal Mnyate wa Mtibwa.Bao hilo lilidumu hadi timu hizo zibnakwenda mapumziko. 
Kipindi cha pili kilianza kwa timu kucheza kwa umakini huku   Simba wakicheza mpira wa akili na kuwachosha wakata miwa hao wa Mtibwa na kuwafanya  kucheza mpira wa kutumia nguvu. 
Christopher aliiandikia tena Simba bao la pili katika dakika ya 52, akimalizia krosi ya Rashid Ismail, kabla ya Mtibwa kusawazisha katika dakika ya 56 kupitia Kisiga aliyepiga shuti kali nje ya 18 na kumshinda kipa wa Simba. 
Simba ilipachika bao la tatu katika dakika ya 66 likipachikwa na Haruna Athuman mara baada ya kuwatoka mabeki  wa Mtibwa, kabla  Hassan Seif kuitumia safu faulo na kusawasazisha katika dakika ya 73. 
Dakika 90 za mchezo huo ambao ulishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dh.Fenella Mukangara ambaye alikuwa mgeni rasmi,zilimazika kwa timu hiyo kwenda sare ya mabao 3-3 hivyo mwamuzi kuongeza dakika 30. 
Alikuwa ni Christopher tena ambaye aliifungia Simba bao la ushindi katika dakina ya 102 alipomalizia kazi safi ya ia  kazi safi ya Frank Sekule na kufanya bao hilo lidumu hadi dakika ya 120 na kuifanya Simba kushinda kwa mabao 4-3. 
Kwa ushindi huo, Simba imepata milioni 40 pamoja na medali , huku Mtibwa ikiondoka na shilingi mil 20 pamoja na medali. 
Aidha, shujaa wa Simba Christopher alizawadiwa sh milioni mbili kwa kuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao 7, huku kipa wa Simba Abuu Hashim alizawadiwa sh milioni 2.5 kwa kuwa mchezaji bora. 
Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi Agosti 8 na kuzishirikisha pia timu za Simba, Mtibwa Sugar, Azam Fc,Polisi Morogoro kwa upande wa Bara, huku Visiwani iliwakilishwa na  Mafunzo ,Zimamoto, Mtende na  Super Falcon. 
Simba:Abuu Hashim, William Lucian, Omary Salum, Hassan Isihaka, Hassan Hatibu, Said Ndemla, Haruna Athuman, Abdallah Seseme, Rashid Ismail, Edward Christopher na Ramadhan Singano/Fank Sekule. 
Mtibwa Sugar:Shaban Kado, Malika Ndeule, Yusuf Mguya, Salum Swedy, Salvatory Ntebe, Babu Ally, Jamal Mnyate, Awadh Juma, Juma Javu, Shaban Kisiga/Hassan Seif na Vicent Barnabas.
source; mitandao..

Labels: ,

Friday, August 17, 2012

NJIA ZA KUPATA MAFANIKIO MAISHANI..


                   
Kwa kuwa maisha ni kama safari na malengo ndiyo dira, ukianza kuyafanyia kazi malengo yako utagundua unatakiwa kufanya nini ili safari yako ya maisha iwe rahisi. Lazima ufahamu mambo muhimu yatakayokusaidia kurahisisha safari yako kuelekea mafanikio.

Baada ya kuyatambua malengo yako, anza kutathmini kuhusu malengo yako na mahali pakuanzia, yakupasa kutambua kuwa safari yako ina milima na mabonde. Kuna ulazima wa kutafakari kwa kina mambo yanayoambatana na safari yako ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio.
Zingatia mambo yafuatayo:

-Taaluma yako: Haijalishi kama umesoma au la! Jiulize na tafakari mara nyingi juu ya uwezo na taaluma yako. Jielimishe juu ya mambo usiyoyafahamu yanayohusiana na kazi yako na hakikisha una taarifa zote muhimu kuhusu fani/kazi yako.

-Matumizi yako- Jiulize kuhusu uwezo wako kiuchumi. Jiulize kipato chako kwa siku na matumizi yako. Jitahidi kuyafanya matumizi yawe madogo kuliko kipato. Anza kuweka akiba kwa ajili ya matumizi ya siku za baadaye.

-Marafiki – Marafiki zako ni kina nani? Kuna usemi maarufu unaosema: Niambie kuhusu marafiki zako nami nitakwambia wewe ni nani. Marafiki na watu wanaotuzunguka wana ushawishi mkubwa wa kutufanya nasi tukawa kama wao. Kama una nia ya kweli ya kufika kwenye kilele cha mafanikio lazima uambatane na watu wenye mafanikio makubwa kukuzidi.

-Tabia/ Mwenendo- Namna tunavyoishi kwa kuendekeza tabia au mazoea fulani ndivyo tunavyojiweka mbali na mafanikio. Kama wewe ni mlevi uliyepitiliza kiwango au unaendekeza anasa, una kazi ya ziada kuyafikia mafanikio.

Baadhi ya tabia na mazoea yakijenga usugu akilini mwa mtu, humpunguzia uwezo wa kutafakari na kuzingatia malengo yake. Badala ya kuhifadhi pesa kwa ajili ya matumizi ya siku zijazo, hutaona tatizo kuzitumia kustarehe na marafiki zako kwa kunywa pombe na kufanya anasa nyingine. Badili tabia na mwenendo kwa dhati, hakika utafanikiwa.

-Afya yako- Vipi kuhusu afya ya mwili na akili? Ili ufanikiwe ni lazima uwe na afya njema. Kinga ya mwili wako lazima iwe imara na akili ifanye kazi kwa kiwango kinachotakiwa. Endapo afya yako haiko sawa (kimwili au kiakili), hakikisha unatafuta ufumbuzi mapema. Zingatia ulaji wa mlo kamili na kunywa maji mengi kila siku ili kuweka mifumo yote ya mwili wako katika hali ya ufanisi.

-Jamii inayokuzunguka: Unaishi vipi na jamii inayokuzunguka? Unajiona mjuaji wa kila kitu au unajishusha thamani? Unawasikiliza wengine au wewe ndiyo kinara wa kila kitu? Unapokea ushauri wa wengine na kuufanyia kazi? Ni busara kujiuliza maswali haya ili uishi vizuri na jamii inayokuzunguka.

Badala ya kujiona unajua kila kitu, jipe nafasi ya kuwasikiliza wengine, utajifunza mengi. Usifurahie kuona mwenzako anapatwa na matatizo, toa msaada kwa wengine kila inapobidi na hiyo itakuongezea nafasi ya kutimiza malengo yako.

-Ufanisi wako- Wengi wetu tuna uwezo wa kufanya mambo makubwa kwa kiwango kinachotakiwa lakini tunakwamishwa na ufanisi mdogo tunaouonesha. Kama malengo yako ni kuanzisha biashara kubwa ya kuuza duka, lazima uoneshe ufanisi mkubwa hata pale unapokuwa na mtaji mdogo. Usifikirie kuwa ukishapata mtaji mkubwa ndiyo utaweza kutunza mahesabu vizuri na kuzuia hasara. Onesha ufanisi tangu hatua ya awali.

-Jifanyie tathmini- Katika kila unalolifanya, hakikisha kuwa unajifanyia tathmini wewe mwenyewe. Usisubiri mtu wa pembeni akwambie kuwa unafanya makosa kwenye jambo hili au lile. Hakikisha kuwa kila siku kabla ya kulala unatathmini shughuli zote ulizozifanya kwa siku husika.

Ukizingatia kwa makini haya niliyoyaeleza, hakika milango yako kuelekea mafanikio ya kweli itafunguka.


Labels: ,

Rufaa Ya Lema Tarehe 20 Sept



RUFAA ya kupinga kuvuliwa ubunge ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), imepangwa kusikilizwa Septemba 20, mwaka huu, mbele ya majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa; Natalia Kimaro, Mbarouk Salim Mbarouk na Salumu Massati.
Kwa mujibu taarifa za kikao cha Mahakama ya Rufaa cha Arusha, rufaa hiyo iliyofunguliwa na Lema akipinga uamuzi uliotengua ubunge wake kufuatia shauri lililofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, inatarajiwa kusikilizwa kwa siku moja ambapo baada ya hapo itapangwa tarehe kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.

Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.

Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Katika madai mengine, Lema anamlalamikia, Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa, alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Lema anadai kuwa, Jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

Kesi hiyo iliyotengua ubunge wa Lema, ilifunguliwa na wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, wakidai kuwa wakati wa kampeni mbunge huyo alimdhalilisha mgombea mwezake, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.

ANGALIZO
Jaji Mbarouk Salim Mbarouk ni yule aliyeonekana kutajwa kwa namna isiyo nzuri kwenye utetezi wa Tundu Lisu au ni mwingine? na kama ni yeye hiyo haitaleta tena kutoridhika iwapo maamuzi hayatakuwa upande wa Lema na Chadema? nini mawazo yenu katika hili? 
Bush Lawayer

Labels: ,

dahh ni nomaa..


MCHAGA anamdai MPARE hela..huku MSAMBAA akishuhudia
MPARE:nimesema sikupi bora nijiue avaeee
(kwa ubahili wake mpare akajichoma kisu akafa)
MCHAGA:kiruu umejiua mbee sikubali na kufuata huko huko unipe pesa yangu
(kwa kupenda hela mchaga nae akajichoma kisu ili amfuate)
MSAMBAA:tateee nane nane..yaani hawa wanataka kuninyima uhondo wanaenda kudaiana huko ili nisione,walah sikubali nami najichoma
(msambaa kwa umbea tu,na uboya wake nae akajichoma)....

Labels:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA 17.08.2012

 

CREDIT KWA MJENGWA BLOG
















Labels:

Thursday, August 16, 2012

EXCLUSIVE: "KAMA BUSHOKE AKINIZUNGUA, BASI NAITOA HII MIMBA" - JINI KABULA

Siku chache baada ya kuripotiwa amenasa mimba, mwigizaji anayewakilisha kundi la Scorpion Girls, Mariam Julwa aka JINI Kabula amemtaja mwanaume aitwae Bushoke kama ndio baba wa mtoto wake.

"Hii ni mimba ya miezi minne sasa, kama Bushoke hatakuwa na usumbufu wowote basi nitamzalia mtoto mzuri ambaye atatamba nae mitaani, lakini akinizingua, wakati wowote sikawii kubadilisha mawazo na kuichoropoa"

Labels: ,

HATUA ZA KUMRUDISHA MPENZI WAKO ULIOACHANA / KUGOMBANA NAYE..


Karibuni sana wapendwa katika blog yetu hii ya bongomixx. leo ningependa tuzungumzie jisi ya kumrudisha mpenzi ambaye umeachana naye ama yupo mbali na wewe ama umepoteana naye kwa muda mrefu.
Kugombana ni sehemu ya maisha ya binadamu. Yawezekana kabisa ulikuwa na mwenzi wako ambaye ulimpenda kwa moyo wako wote na sasa mmeachana. Kutengana kuna mambo mengi, wakati mwingine ilikuwa hasira tu.
Siku zote baada ya hasira kuisha, moyo hubaki peke yake katika nafasi yake halisi ya kufanya maamuzi. Hapo ndipo kwenye lengo la mada yetu ya leo. Kwamba kwa msingi huo umegundua kwamba kumbe mpenzi wako uliyeachana naye, bado unampenda.
Kwamba hata makosa aliyokuwa akiyafanya, ulimsababishia au si makubwa kiasi cha kuachana na badala yake mnaweza kukaaa na kuzungumza kiutu uzima na kuyamaliza. Yes! Hilo ndilo ninalotaka kulizungumzia.
 
Upo tayari rafiki? Je, uko katika kundi hilo? Unataka kumrudisha mpenzi wako wa zamani? Kama majibu ni ndiyo, mada hii inakuhusu sana.

JE, NI SAHIHI?
Baadhi ya watu huamini kwamba kurudi kwa mara nyingine kwa mpenzi wa zamani ni kujidhalilisha, kujishusha na kujisalimisha. Kwamba hakuna mwanaume wala mwanamke mwingine yeyote atakayeweza kuwa naye tofauti na huyo anayemrudia.
Jambo hilo si la kweli hata kidogo, kikubwa cha kuzingatia hapa ni moyo; je, unahisi bado unampenda? Ni kweli naye anakupenda? Kama sifa hizi zipo, hayo mambo madogo ambayo mmetofautiana ni ya kawaida kabisa ambayo mnaweza kurekebishana taratibu.
Kwa msingi huo basi, hakuna tatizo lolote katika kurudiana na mpenzi wako wa zamani, maana tayari unakuwa umeshamjua vya kutosha, hivyo kukupa urahisi wa kufanya yale anayoyapenda na kuepuka asiyopenda jambo litakalozidisha umri wa uhusiano wenu, si ajabu mkaingia kwenye ndoa.

UTAFAIDIKA NA NINI?
Utafiti usio rasmi nilioufanya, unaonesha kwamba zipo faida za kurudiana na mpenzi mliyeachana, lakini kikubwa ni awe moyoni mwako.
Hebu msikie Julius Kihesupe wa Uwanja wa Ndege, jijini Dar es Salaam, ambaye alipata kuzungumza nami hivi karibuni akitoa maoni yake kuhusu suala hili: “Si vibaya kurudiana, maana kwanza mnakomaza uhusiano.
“Kumrudia mtu wako wa zamani maana yake ni kwamba umekubaliana na udhaifu wake wote. Unajua anachopenda na anachochukia, hapo lazima mtadumu. Bila kudanganya, mke wangu wakati wa urafiki wetu, tukiwa na miaka miwili kwenye uhusiano tulitibuana tukaachana.
“Kila mmoja alikaa kivyake kwa miezi kama sita hivi, nikakutana naye Dar, nikiwa nimeachana naye Mbeya, nikamwita tukakaa na kuzungumza, miezi minne mbele yake tukafunga ndoa.”

CHUNGUZA ALIPO
Kitu cha kwanza kabisa ambacho unatakiwa kuchunguza ni mahali anapopatikana kwa wakati huo, nasema hivyo kwa sababu yawezekana alihama makazi, kikazi n.k. Kujua anapopatikana ni mwanzo wa kuelekea kwenye mafanikio ya kumkamata katika himaya yako.

ANA HISTORIA GANI?
Lazima ujue kuhusu historia yake kiuhusiano baada ya kuachana na wewe. Hapo unatakiwa kufanya ‘ushushushu’ wako kimyakimya bila yeye kujua. Ikiwa ameshafanya ‘vurugu’ sana, maana yake ni mtu asiye na msimamo na huenda anaongozwa zaidi na tamaa za kimwili na si mapenzi.
Katika kipengele hiki, ni muhimu sana kujua kama muda huo ambao wewe unahitaji kurudi tena mikononi mwake kama ana uhusiano mwingine. Kimsingi kama atakuwa ndani ya uhusiano, itakubidi uhairishe zoezi lako.
Unatakiwa kufanya hivyo kwa sababu kwanza, anaweza kukubali kuwa na wewe wakati akiwa bado hajaachana na mpenzi aliyenaye kwa muda huo, hivyo kuwa kama mwizi tu kwa mwenzako.
Kubwa zaidi ni kwamba, utakuwa katika mapenzi ya kushea, jambo ambalo si zuri kisaikolojia na hata kiafya.

Kumbuka kwamba, unaweza kuwa na mwenzi wako, mkapendana kwa dhati na mkadumu kwa muda mrefu, lakini kwa bahati mbaya mkaachana kwa sababu ambazo mnazifahamu wenyewe.
Katika muda mfupi ambao utakuwa umeachana naye, anaweza kufanya mambo ya ajabu sana. Pamoja na kwamba moyo wako unamhitaji, lakini anaweza kuwa tayari ameshapoteza sifa za kuwa na wewe. Katika hali hiyo, ni sahihi kurudiana naye? Bila shaka jibu hapa ni siyo sahihi.
Wiki iliyopita tulianza kuangalia kama ni sahihi kurudi kwa mwenzi huyo, faida utakazopata kwa kurudiana naye, kuchunguza sehemu anayopatikana na kufuatilia historia yake baada ya kutengana kwenu.
Enheee! Sasa twende kwenye vipengele vingine.



MAWASILIANO

Ukishachunguza mahali alipo na kuridhika na historia yake ya kimapenzi baada ya kuachana na wewe, sasa unatakiwa kutafuta mawasiliano yake. Kupata mawasiliano yake ni hatua ya kwanza, kitakachofuata baada ya hapo ni kujenga mawasiliano. Hapo sasa inategemea na namna mlivyoachana, lakini kama hamkuwa na ugomvi mkubwa sana, basi unaweza kumtumia meseji za kichokozi mara nyingi uwezavyo kwa siku.Majibu yake ndiyo yatakayokupa mwanga wa kuendelea na kipengele kingine. Kikubwa hapa ni kutozungumzia kabisa mambo ya mapenzi, badala yake iwe ni kumjulia hali na utani wa hapa na pale.



MPE MWALIKO


Baada ya kutengeneza mawasiliano naye, sasa unatakiwa kumwalika katika shughuli mbalimbali za kifamilia na binafsi. Mathalani umepata mwaliko wa kwenda kwenye sherehe au hafla fupi ya usiku, omba kampani yake.
Kama mtu mzima atagundua kitu kilichopo moyoni mwako. Hata kama atakuwa mwenye moyo wenye kutu, kutoka naye mbele za watu, kutamfanya akumbuke enzi zenu mlipokuwa mkitoka pamoja, hivyo kufikiria kurudi tena kwako.Ikiwa ataamua kukuambia kwamba anaona mrudiane litakuwa jambo zuri zaidi, maana atakuwa amekurahisishia, lakini akinyamaza, basi njia inayofuata hapa chini ni muafaka kwake.



MVUTE KARIBU YAKO

Sasa unatakiwa kumsogeza karibu zaidi na wewe. Lazima afahamu kwamba, kuna kitu fulani kipo ndani ya moyo wako. Meseji zako zibadilike, kama ulikuwa unamwandikia, “Vp uko poa?” au “Mambo yanaendaje?”, sasa unatakiwa kubadilisha hadi “Niambie sweetie, uko poa?”Meseji za aina hiyo zitamfanya aone tofauti na inawezekana kabisa akagundua kwamba upo kwenye mawindo ya kumrudisha tena kwako. Katika hatua hii katu hutakiwi kufungua mdomo wako kumwambia kuwa unataka kurudiana naye na badala yake unatakiwa kuacha vitendo vizungumze vyenyewe.

OUTING
Kutokana na ukaribu wenu, kumwalika katika mtoko wa chakula cha mchana au usiku, haitakuwa vigumu kwake. Hiyo itakuwa njia nyingine ya kumfanya awe karibu yako zaidi.Mkiwa katika mtoko huna haja ya kuzungumza chochote kuhusu uhusiano wenu, labda kama yeye ataanzisha mjadala huo. Ongelea mambo mengine ambayo ni maarufu zaidi labda katika duru za siasa, sanaa n.k lakini si mambo yanayohusu mapenzi kabisa.Kama kichwani mwake alikuwa amekufanya kama rafiki yake wa kawaida, mtazamo utaanza kubadilika taratibu na kuanza kutamani kurudi tena mikononi mwako. Jaribu kufikiria, kama umetoka naye, akiamini labda unataka kumuomba msamaha na kurudiana naye, wewe unaanza stori za soka! Bila shaka atajiona kama mpumbavu kichwani, si ajabu akaamua kujifunga mwenyewe kwa kuomba urudi tena kwake.



JADILI PENZI LENU
Hatua hii ndiyo muhimu zaidi hapa; sasa unatakiwa kuanza kuzungumzia juu ya uhusiano wenu. Mwambie jinsi ulivyokuwa ukifurahishwa na mapenzi yenu. Msifie alivyokuwa anajua majukumu yake na kukuonesha mapenzi ya dhati.Si vibaya kama utamweleza pia sababu ambazo unahisi zilisababisha wewe na yeye kuachana. Kwa kauli hizo utampa nafasi ya kuchambua/kumjua mwenye makosa na mahali pa kurekebisha.


KIRI MAKOSA YAKO
kiwa kuna mahali unaamini ulikwenda kinyume na yamkini ndiyo sababu kuu iliyosababisha muachane, kiri makosa yako mbele yake. Mweleze kwamba wewe ndiyo chanzo cha matatizo na huenda kama si kukosea, msingeachana.Kujutia hasa kama uso wako utawakilisha vyema kilicho moyoni mwako, kutamfanya akuone muungwana ambaye unatambua ulipojikwaa na sasa unataka kurekebisha makosa yako. Hapo utakuwa na nafasi kubwa ya kumnasa kwa mara nyingine.


MWELEZE YAKO YA MOYONI
Sasa huna sababu ya kuendelea kujitesa, toa dukuduku lako. Mwambie moja kwa moja kilichopo moyoni mwako. Kwamba unahitaji nafasi nyingine kwake, maana umeshajua makosa yako.
Hii ni nafasi ambayo si rahisi kabisa kuchomoka. Itumie vilivyo. Sauti yako pekee itoshe kumaanisha kile kilichopo moyoni mwako. Lazima atakuelewa.
Kama utakuwa umefuata kwa makini vipengele vyote hapo juu, lazima urudi tena mikononi mwake. Kuna nini tena? Ameshakuwa wako huyo, ila kuwa makini usimpoteze tena.

AKIKATAA JE?
Pamoja na kufuata vipengele vyote hivyo, inawezekana akakataa. Kukataa kwake lazima kuna sababu nyingi. Mwingine anaweza kukuambia moja kwa moja sababu za kukataa kurudiana na wewe wakati mwingine anaweza asiseme chochote.
Huenda akakumbia kwamba tayari ana mtu wake, au hafikirii kurudi mikononi mwako; usihuzunike.
Ni bora sana huyu anayekuambia ukweli, kuliko kurudi halafu ukutane na mateso yale yale.Inawezekana labda hana mapenzi na wewe. Kama ndivyo, kuna sababu gani ya kujikomba? Kubaliana na ukweli, halafu subiri mwingine!
Sikia, subiri mwingine na siyo utafute, maana mwenzi wa kweli huja mwenyewe, hatafutwi!

Labels: ,

Vunja mbavu zako kwa picha..

Bibi mjanja akiingia ndani ya blog yetu ya bvongomixx

Mkisi mchumu mwaaaaaaaa!!!!!!1

sio lazima uende beach hata hapa unabadilisha hali ya hewa tu..

je? unahitaji fundi wa kujenga??

ohh, watoto tu ndio wanaoga kwenye mabeseni, nani kasema?? nenda kenya uone

jamani urembo kaziiiiiiiii...!!

hata hapa ni toilet tu..!!!

wanasoka mmemuona balloteli akizeeka??

hii kitu serious imetokea

kama ungekuwa wewe ungefanyaje hapa..??

dah hizi network za kibongo miyeyusho kweli yaan

je, unajua mapozi ya wachina katika kupiga picha???

kama kawa kama dawa tunawakilisha peoplesssssssssssssssssssssssssssssss!!!!

eeeh, kumbe kwa mbele ndio anamanywele hiviii..!!!

mbwa ana akili huyuuu..!!!

weee endelea kuchat ipo siku utaumbuka wewe????

ooh, eti rooney hajawahi kuuza pipi na biskuti, nani kasema??

hii ndio bongo halisi

kama kweli una gari jaribu kupita kushoto uone

kweli hii picha itatoka full hapa..???

kitu cha DSTV yaani hapa ni full big brother, super sport na ma movie ya kumwaga

Labels:

**** Play gal - 59 (Revenge)



Ilipoishia…

Aisha aliongea kwenye simu kwa sauti ya ukali na yakikatili kisha ndani ya dakika chache mlango wa gari kwa upande wangu ukafunguliwa. Tochi zilinimulika kisha nikashikwa na watu nisiowafahamu halafu kwenye gari nikamshuhudia Jerry kiingia kisha akambeba yule mtoto na kuondoka zao na Aisha huku wakiniacha nimekumbatiwa na watu nisiowafahamu.
“..mnampeleka wapi mwanangu..??, mrudisheni..??”
Nilitoa makelele ya nguvu lakini haikusaidia chochote zaidi ya ile gari kutokomea huku wale wavulana waliokuwa wamenishika kwa kunikumbatia wakianza kunivua nguo zangu na zao tayari kwa kunibaka kwa zamu…

 Sasa endelea..


Walinigombania huku kila mmoja akinivuta huku na kule. Nilijitahidi japo kutoa sauti za makelele lakini haikusaidia kitu zaidi ya wale vijana kunipiga vibao na kisha kuniburuta mpaka eneo la kichakani kwenye giza totoro. Mwili wangu wote ukawa hauna thamani tena. Hawakuwa watu wazuri hata kidogo kwani walinifanya kwa nguvu na baada ya hapo wakachukuwa majiti nakunisokomeza ambapo walinisababishia maumivu makubwa na makali sana mwilini mwangu na haswa upande wa matiti yangu kwani walikuwa wakiyavuta na kuyafinya kwa kucha zao ndefu  na hata wengine kuyauma kwa kutumia meno. Ndani ya kama nusu saa walikuwa wameshaniharibu sana na pia walikuwa wameshatawanyika kila mmoja. Uwezo wa kusimama sikuwa nao zaidi ya kujiburuta chini chini huku nikitafuta japo barabara kuu ya kuweza kutokea. Tumbo nalo lilianza kuniuma sana tena kule kuuma kwa kuvuta maeneo ya chini ya kitovu.
“..nimekukosea nini eeh Mungu wangu..? Niangalie ninavyoteseka..? Weka japo mikono yako uniangaze na kunipa nguvu eeh  Baba..?”
Nilianza kumlaumu mwenyezi Mungu aliyeniumba nakujiona nimetengwa kabisa katika ulimwengu huu uliojaa mateso. Mikono yangu miwili ndio ilikuwa kama miguu kwa kujisukumia taratibu. Hatimaye baada ya mwendo kidogo nikaona gari kwa mbali linapita. Nilijaribu japo kutoa sauti ya ukali kwa makelele lakini ilishindikana kwani sikuwa na sauti kubwa tena na hata hivyo lile gari lilikuwa katika mwendo kasi hivyo halikuweza hata kuniona wala kusimama. Akili yangu sasa ikawa inamfikiria mwanangu Adrian niliyeporwa na rafiki yangu kipenzi Aisha akishirikiana na Jerry.
“..na lazima niwatafute na kuwaua kabisa..?”
Hasira yangu kwa sasa ikawa imefika kikomo kwani nilijihisi kutokwa na mishipa pembezoni mwa paji la uso wangu.  Nilijikuta nimepata nguvu za ajabu tena zile za ghafla. Niliweza kuinuka na kwa sasa nikawa natembea haraka  haraka mithili ya wanajeshi wakiwa katika mazoezi yao ya kwenda vitani. Haikunichukuwa  mwendo sana mara kwa mbele yangu kidogo nikakutana na dalaldala pamoja na teksi teksi zikiwa zimepaki huku eneo lile kukiwa na watu wakifanya shughuli zao mbali mbali. Hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi haraka nakutambua kuwa pale patakuwa ni kituo cha daladala na pia ni maeneo ya makazi ya watu. Mwili wangu sasa ukaondoka na hofu ya kuwa bado porini. Furaha yote nikaihamishia ndani ya lile eneo huku nikilisogelea kwa tabasamu ya hapa na pale. Nilipofika tu pale kwenye mwanga kila mmoja akaanza kunishangaa. Nilijiangalia mwili wote kisha.
“..Mamaaaaa..!!!!!, Mamaaaaaa…!!!”
Maskini Tina mimi kumbe nilikuwa sijavaa hata nguo. Nilikuwa uchi wa mnyama na mwili wangu kwa sasa ulikuwa umegandia damu damu ambazo zilikuwepo maeneo yote ya kuzunguka mapajani, tumboni mpaka kwenye maziwa yangu. Aibu kubwa niliipata lakini sikuwa na jinsi zaidi ya akili yangu kunituma nirudi kule machakani nilipobakwa nikazichukuwe nguo zangu. Kwa mwendo wa haraka niligeuka nyuma nakuanza kuondoka zangu. Hatua mbili tatu mara uso kwa uso nikakutana na gari.
“..Mamaa nakufaaa..!!”
Mwili wangu wote ulikuwa uvunguni mwa gari lilikokuwa linapita njia na kwasasa lilikaribia kunigonga. Ni breki tu ndizo zilisaidia. Yule aliyekuwa akiendesha gari alishuka huku anaongea maneno kwa ukali. Kadri alivyonisogelea na ile sauti ilivyokuwa ikitikisa ngome ya masikio yangu ndivyo nilivyokuwa nikisisimka nakupata na wasiwasi kama namfahamu. Aliponifikia karibu tu.
“..haa Aisha niwewe…? Kwanini unanifanyia hivi jamani..??, umenitumia vijana wanibake sawa…? Ukaona haitoshi ukanipora na mwanagu Adrian ukampa Jerry kisa pesa Aisha….??. Haya sasa si unataka unigonge..??, nigonge kabisa ili ndoto zako ziwe zimetimia si ndio..?”
Niliongea kwa jazba sana baada yakugundua kuwa kumbe aliyetaka kunigonga alikuwa ni rafiki yangu kipenzi Aisha na kwa muda huu alishuka nakuniongelesha kwa hasira zake. Nikiwa bado nipo uvunguni mwa gari huku Aisha akiniongelesha mara nikasikia sauti ya mtoto wangu akilia ndani ya gari.
“..Aisha mwanagu Adrian yuko wapi nasikia analia..??, nasikia analia.., yuko wapi..?”
Hasira kali nilizoinuka nazo pale chini zilinifanya nimsukume Aisha nakuongoza moja kwa moja mpaka kwenye mlango wa gari lake bila kugeuka nyuma. Nilifungua mlango ule kwa hasira zote nakumshuhudia mwanangu Adrian akiwa anatapika ovyo huku kafungwa fungwa ovyo na makamba shingoni mwake. Nilianza kumfungua haraka haraka lakini kitendo cha kumalizia kumfungua tu zile kamba nikahisi kimya kwa mwanagu Adrian. Nikamtingisha bado kimya. Nikamgusa na kuegemeza kichwa changu kifuani mwake japo nisikie mapigo yake ya moyo napo kimya. Akili yangu moja kwa moja ikanituma kuwa mwanangu Adrian sinaye tena yaani ameshafariki..
“Adrriiiiiiiiiaaaaaaaaaaaaaaaaaaannnnnnn….???????, Adriiiiiiiiiiiiiiaaaaaaaaan…..??”
Bado nilimuinua nakumtingisha tingisha lakini ndio kama nilikuwa najifurahisha na mdori kwani alishafariki muda mrefu.
“..Aisha..?? Aisha…??, Aishaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa..??”
Nilishtuka kutoka usingizini huku jasho likinitiririka mithili ya maji ya chemu chemu yakifuata mkondo wake huku kwikwi kali sana ya hasira na maji kwa ujumla vikinishika vilivyo. Kizunguzungu cha ghafla kilichonishika nilijihisi naona kama ukungu mbeleni mwangu kwani macho yangu yalikuwa yameishiwa nguvu ya kuona vizuri. Nilishusha pumzi nakupikicha macho yangu huku nisiamini kama vile vyote vilivyonitokea kuwa ilikuwa ni ndoto. Eti mpaka rafiki yangu Aisha akanigeuka nakumchukua mwanangu Adrian. Haraka haraka nikageuka pembeni yangu nakumwangalia mwanagu Adrian ambaye alikuwa bado amelala. Nilimuinua nakumbusu kwenye paji lake la uso.
“..inaonekana unampenda sana mwanao Adrian…?”
Aliniongelesha rafiki yangu Aisha ambaye kwa muda huu tulikuwa bado tupo njiani kuelekea nyumbani kwake na alikuwa akiendesha gari. Nilijilaumu sana kuota ndoto ya ajabu kiasi kile lakini haina jinsi kwani ndoto haipangwi. Nilimgeukia rafiki yangu Aisha mara mbili mbili huku nikioneshwa kutetemeka kwa uwoga nakudhani huenda nilichokuwa nakiota kikanitokea muda wowote.
“..ahh..!! itakuwa mandoto tu..!!, kwanza hawezi kunifanyia hivyo rafiki yangu kipenzi Aisha….”
Nilijikuta najifariji kwa kuongea kimoyo moyo huku nikiachia tabasamu kwa kumwangalia Aisha.
“..daah..!!, kumbe hujaacha kulala lala enhh..??”
“..ennhh..!!  shosti wangu kwa jinsi ninavyopenda kulala Tina mimi..? Yani ni kama ugonjwa kwangu toka kipindi kile tupo wote chuoni.., si unakumbuka hata darasani nilikuwa siingii ama nachelewa kisa usingizi..?”
“.. ni kweli.., ila umelala sana, yani tokea tunatokea pale chuoni CBE umelala tu na mwanako wote. Tumepita kwenye mafoleni pale Morocco, Kijitonyama hadi Mwenge kote bado umelala tu Tina..?”
“ndio hivyo..!!, wanasema usingizi mwanaharamu ukikushika. Lakini bado tu hatujafika aisha..?”
“ujue ni vijifoleni tu vya hapa na pale ndivyo vinafanya hivi, lakini isingekuwa hivi..? tungekuwa nyumbani muda mrefu sana.. lakini hatuna muda mrefu tunafika..”
Niliendelea kupiga  stori mbili tatu na rafiki yangu kipenzi Aisha japo bado kale ka uwoga ka ndoto kalikuwa kakinitawala ndani ya halmashauri yangu ya ubongo. Ndani ya dakika kama kumi hivi tulikuwa tunatazamana na geti kubwa  jekundu lililopambwa na nakshi nakshi za silva. Aisha alipiga honi kama mara mbili na punde akatoka kijana aliyekuwa amevaa kofia kuashiria kuwa huenda alikuwa ni mlinzi wa Aisha. Alitufungulia nakuingia mpaka ndani.
“..Tina karibu na jisikie uko nyumbani. Hapa ndipo ninapoishi na mume wangu niliyekwambia kuwa kwa sasa ni mfanyabiashara na wala si mtu wa kukaaa sana hapa bongo kwani huwa anakuja na kuondoka siku hiyo hiyo au anakaa hata siku moja mbili anaondoka zake. Karibu ndani kipenzi changu..”
Aisha alinikaribisha kwa ukarimu sana. Tuliingia mpaka ndani na akanikabidhi chumba kimoja.
“..hiki kitakuwa chumba chako kuanzia sasa Tina. Jisikie uko nyumbani na jisikie upo kwako rafiki yangu kipenzi Tina..”
“..haa..!!, sijui hata nikushukuru vipi mpenzi..!! Ahsante sana na ubarikiwe uendelee kuwa na moyo huo huo Aisha..”
Chumba kilikuwa nikikubwa sana ambapo ndani yake kulikuwa na kila kitu. Kuanzia choo na bafu. Kitanda kikubwa. Nilimvua mwanangu Adrian nguo zake nakumpeleka bafuni ambapo nilimuogesha nakisha nikambadilisha pampasi, baada ya hapo nikaoga na nilipotoka kuoga tu Aisha tayari alikuwa chumbani kwangu kitandani na Adrian ananisubiri nitoke kuoga.
“..Tina nimekuletea nguo hizi hapa, mie huwa zinanibana sana si unajua kunenepa kwangu ovyo tena..!!”
“..Ooh..!!, ahsante Aisha..”
“..ila kuna kitu nahitaji ujue…





*** je unavyodhani ni kitu gani hicho Aisha anachotaka kusema..?

*** Aisha ataishi vizuri na Tina kweli..? na nini hatma ya Tina katika story hii..?

*** stori ndio kwanza kama inaanza upya.. usithubutu uikose wala kusimuliwa inayofuata, ***Play gal 60

Labels:

Namna ya kupanga malengo maishani






Baada ya kuanza kujiuliza na kuyatambua malengo yako huku ukiandika kila wazo linalokujia akilini, fuata hatua zifuatazo:

1. JENGA PICHA AKILINI MWAKO
Jenga taswira ya kitu unachokitaka akilini mwako. Picha unayoijenga lazima iwe kubwa. Fikiria jinsi utakavyokuwa na mafanikio makubwa maishani katika kile ulichochagua kukifanya. Jione tayari ukiwa katika mafanikio ambayo ulikuwa ukiyatamani kwa siku nyingi.

Jitazame furaha utakayokuwa nayo na jinsi utakavyoyamudu maisha ya mafanikio. Panga malengo ya muda mrefu. Usifikirie kuwa ulichokiwaza kitatokea kesho, jipe muda hata wa miaka kumi au zaidi, usiogope kufikiria mambo makubwa yanayohitaji muda mrefu kukamilika. Kuanzia hapo, endelea na hatua ya pili.

2. YARAHISISHE MALENGO YAKO
Yawezekana malengo yako ni makubwa sana kiasi cha kukuzidi. Hiyo isikutishe, yarahisishe malengo yako. Kivipi? Kama malengo yako ni kuwa na mafanikio makubwa maishani baada ya miaka kumi, ugawanye muda wako katika sehemu ndogondogo.

Kwa mfano unaweza kuanza kugawanya miaka kumi kwa mbili, yaani baada ya miaka mitano uwe angalau umefikia nusu ya kile ulichokiwaza awali. Baada ya hapo igawanye miaka mitano kupata mwaka mmoja mmoja.

Jiulize kwa kila mwaka utafanya nini ili kuyakaribia mafanikio. Weka ratiba na mipango yako kwa maandishi. Ugawanye mwaka kupata miezi, jiulize utafanya nini mwezi wa kwanza, wa pili hadi mwaka uishe. Hakikisha unaandika kila kinachokujia akilini.

Endelea kurahisisha malengo yako kwa kujiuliza ndani ya miezi sita utakuwa tayari umefanya nini, shuka mpaka miezi mitatu kisha malizia kwa kila mwezi mmoja. Utaona kwamba lengo unalotarajia kulifanikisha kwa kipindi cha miaka kumi umelirahisisha mpaka kwenye mwezi mmoja.

Usiishie hapo, mwezi ugawanye kwenye wiki, kisha malizia kwenye siku. Jiulize kila siku utafanya nini ili kuelekea kwenye lengo lako kubwa unalotaka litimie baada ya miaka kumi. Hapo utaanza kuona umuhimu wa kutumia muda wako vizuri, hakuna muda wa kupoteza.

3. ANZA UTEKELEZAJI
Anza utekelezaji wa malengo yako mara moja. Hakikisha kila saa inayopita umefanya jambo ili kupalilia malengo yako. Hakikisha unafuata ratiba uliyojipangia, usisubiri mtu mwingine aje kukukumbusha kuhusu malengo uliyoyapanga. Tembea na karatasi au kitabu ulichoandika malengo yako na endelea kujikumbusha kila siku juu ya kile unachotaka kitokee.

Mwanasaikolojia mmoja mashuhuri aliwahi kuandika kuwa: Mafanikio siyo tukio unaloweza kulisubiri litokee bali ni hatua unayochukua kuyafikia. Ukianza kufikiria mafanikio, tayari umeanza kufanikiwa, ukiweza kupanga malengo na kuanza kuyafanyia kazi, tayari umo ndani ya mafanikio.

Usisubiri itokee siku ambayo utalala halafu ukiamka asubuhi ukute yale uliyokuwa unayataka yametokea. Malengo yako lazima yakutese usiku na mchana. Watu wote waliofanikiwa hawakufika hapo kwa bahati, walipanga malengo na wakayafanyia kazi.

MAMBO YA KUZINGATIA KUELEKEA MAFANIKIO
Kwa kuwa maisha ni kama safari na malengo ndiyo dira, ukianza kuyafanyia kazi malengo yako utagundua unatakiwa kufanya nini ili safari yako ya maisha iwe rahisi. Lazima ufahamu mambo muhimu yatakayokusaidia kurahisisha safari yako kuelekea mafanikio.

Labels: ,

Tuesday, August 14, 2012

MAGAZETI LEO JUMANNE..

















Labels: