Kwenye YOU HEARD ya XXL ya Clouds Fm, Soudy Brown amempigia
simu Mpoki kumuuliza kuhusiana na story iliyoandikwa na gazeti la Ijumaa Wikienda
kuhusiana na Masanja Mkandamizaji mwishoni mwa wiki iliyopita kudaiwa
kutandikwa makofi hadharani na polisi baada ya kuingilia msafara wa gari
lililokuwa limebeba fedha.
Katika mahojiano hayo Mpoki amemwambia Gossip Cop kuwa hana
taarifa zozote kuwa Masanja amelazwa kutokana na kichapo hicho na kummshauri
kuwa aende kwanza field ili ajifunze uandishi wa habari kwakuwa hauwezi.
Mpoki amejinadi kuwa yupo kwenye game kwa miaka 12 hivyo
hayumbishwi na kitu.
Habari hiyo iliandikwa:
MCHEKESHAJI wa Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’,
mwishoni mwa wiki iliyopita anadaiwa kutandikwa makofi hadharani na polisi
baada ya kuingilia msafara wa gari lililokuwa limebeba fedha.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilitokea kwenye
njiapanda ya Chalinze mkoani Pwani ambapo msanii huyo alikuwa akitokea Dar
kuelekea Tanga huku akiendesha gari kwa kasi ya ajabu.
Chanzo hicho cha Ijumaa Wikenda kinachopiga kambi maeneo
hayo kilieleza kuwa jamaa huyo alikutwa na kasheshe hilo baada ya ‘kuliovateki’
gari hilo lililokuwa likisindikizwa na polisi ambapo pamoja na kuzuiwa na
wajeda hao, Masanja alijitoa fahamu na kujifanya kichwa ngumu.
Kilisema: “Baada ya ‘kuwaovateki’ wale polisi, ndipo nao
(askari) wakamkimbiza hadi wakamkamata na alipotaka kuleta ‘mbovumbovu’ za
kujifanya staa kama wale wenzake waliopoteza umaarufu na mvuto, ndipo akala
mbata zake safi na soo likahamia kwenye Kituo cha Polisi cha Chalinze Njiapanda
na kumshikilia kwa muda kisha kumuachia baada ya mahojiano.”
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta
Masanja ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kukamatwa na askari
kutokana na makosa ya barabarani kwake ni suala la kawaida huku akikanusha
kupewa kibano.
Labels: gossip, news updates