Friday, August 3, 2012

HATIMAYE AMINI NA LINAH KURUDIANA..

                         
MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo, Amini Mwinyimkuu ‘Amini’, amedai kuwa anatarajia kutoa ngoma mpya ambayo atamshirikisha mpenzi wake wa zamani Linah, ingawa bado ngoma hajaipa jina.

Amini na Linah walikuwa wapenzi walioshibana lakini walikuja kuachana kwa amani na upendo, na sababu kubwa za kutengana kwao hakuna anayejua zaidi ya wao wenyewe.

Akizungumza na Bongo Mixx, Amini ambaye kwa sasa yuko bize na ngoma hiyo ili iwe ya kimataifa zaidi, alidai kuwa kutoka na mawazo ya watu kuwa yenye ana chuki na Linah, sasa ameamua kumshirikisha katika ngoma yake ili kuweka wazi na kufuta kauli za watu wenye nia mbaya.

Wakati huo huo Bongo Mixx ilimvutia Linah waya, nakudai kuwa naye alidai kuwa ameamua kufanya ngoma moja na Amini, kwani wao ni wasanii na wanahaki ya kushirikiana ingawa anaamini kuwa kuna watu baadhi ambao wanaamini wao bado ni wapenzi wakati ishu hiyo yamesha isha zamani.
                                     

Labels: , , ,

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home