Tuesday, August 21, 2012

BI KIDUDE (FATMA BINTI BARAKA) ANA HALI MBAYA


 



Taarifa kutoka Zanzibar zinadai kuwa mwanamuziki mkongwe wa Taarab nchini Bi. Kidude anaumwa na hana msaada wowote.
Inadaiwa kuwa mjukuu wake alizungumza na televisheni ya Zanzibar na kulalamika kuwa bibi yake hana msaada na hivyo kumuuguza kwa shida.
Taarifa zaidi zinasema Bi. Kidude anaumwa tangu wiki iliyopita.na hana mdau hata mmoja wa muziki aliyejitokeza kumsaidia hivyo natoa wito kwa wadau wenye uwezo wajitokeze kumsaidia bi kidude ili apate matibabu na arejee katika hali yake ya kawaida.

Labels: ,

Saturday, August 18, 2012

Roma Mkatoliki,TMK Wanaume Family Jukwaa moja Idd Pili



KWA sasa mambo yanazidi kunoga wakati sikukuu ya Idd El Fitr ikiwa inakaribia, pale kulipoandaliwa burudani ya kufa mtu katika fukwe ya Coco iliyopo Oysterbay, Dar es Salaam siku ya Idd Pili.

Katika burudani hiyo inayoletwa na vinywaji vya Grand Malt na Vita Malt ambavyo havina kilevi, huku wasanii kadhaa wenye majina wakitarajiwa kufanya kweli zaidi.

Kwa mujibu wa Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam alisema, wameamua kuleta burudani hiyo ambayo itakuwa bure kwa kila atakayeshiriki, huku kukiwa na michezo kibao ya kuvutia.

Consolata alisema, wasanii watakaoshiriki katika burudani hiyo ya kufa mtu siku hiyo ni pamoja na Roma Mkatoliki pamoja na kundi za la TMK Wanaume.
Kundi hilo linajulikana kwa jinsi lilivyo na wasanii wakali kama Mheshimiwa Temba, Chege, Aslay, Bibi Cheka na wakali wengine kibao, ambao wote wameapa kutoa burudani ya kufa mtu.

“Unajua vinywaji hivi havina kilevi, hivyo ni vema mtu ukaja na familia yako kwani kutakuwa na michezo ya kila aina pamoja na zawadi kibao,” alisema.

Consolata alisema, burudani hizo za bure zitaanza saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni katika siku hiyo ya Idd Pili.

Labels:

Thursday, August 9, 2012

SHOW MPYA ALIZOFANYA LINAH MAREKANI

Labels:

Wednesday, August 8, 2012

BIFU LA SINTAH NA AGNESS MASOGANGE LAINGIA PART II

 
 
Sintah akiwa katika pozi.
                                                                               
 
 
Mwigizaji  mwenye  mbwembwe nyingi  kutoka ndani ya  tasnia ya filamu Bongo Christina Manongi 'Sintah' amemtaka  video queen wa Bongo Agness Gerald Masogange   kufunga bakuli lake (kunyamza kimya) na kuacha  kumapakazia meneno machafu kwenye vyombo vya  habari.
Akizungumza na mwandishi wetu  mapema leo Sintah amesema kuwa amesikitishwa  sana na kitendo cha  Agness kumtaja yeye (Sintah) kuwa ndiye anahusika na kuisambaza kwenye mitandao video  inayomuonyesha Agness akiwa mtupu huku pia akionekana kufanaya  matendo kadhaa ya kingono.

"Nimemsikia na isitoshe kuna watu wengi wameniambia juu ya hilo la kunitukana na kunitaja redioni kuwa nahusika, mimi  sijui lolote awaulize marafiki zake  ambao mimi naamini ndiyo wanahusika kuzisambaza kwani hata kwenye BBM yangu ni wao ndiyo walinitumia namuomba afunge bakuli  lake la siivyo nitazitoa zaidi kwani ninazo pati wani mpaka 3 na zote nimetumiwa na marafiki zake ambao yeye anacheka nao lakini hajui kama ni ma-sn***ch" alisema Sintah

Akiendelea zaidi Sintah amefunguka kuwa  kamwe hajui lolote kuhusu kamera anayoisma Agnes, kwani binafasi hajawahi kukutana naye  na  alimjua  kupitia   nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva kwa kuwa msichana huyo anapenda kuuza sura  na zaidi hajui hata  anapokaa.

Labels: ,

Tuesday, August 7, 2012

Wema na Diamond wanaumwa ugonjwa mmoja?


Wema Sepetu akichukua vipimo
Diamond alipokuwa hospitali baada ya kuugua ghafla
Pengine huu si muda wa kuendelea kuspeculate tena iwapo Wema Sepetu na Diamond wamerudiana. Kuna mambo mengi yanayoonesha dalili kuwa wapenzi hawa wa zamani wamerudiana. Hawajasema hadharani lakini picha za hivi karibuni zinaweka wazi. 

Kuanzia zile picha za Kigoma kwenye video ya Leka Dutigite na zingine. Lakini inaonekana kama vile Diamond na Wema Sepetu wanaumwa ugonjwa mmoja. 

Wiki iliyopita Diamond alionekana kwenye picha akiwa amelala kwenye kitanda cha wagonjwa na akichukuliwa vipimo na daktari. Na sasa kuna picha ya Wema akiwa kwenye kitanda hicho hicho na akichukuliwa vipimo vilevile kama Diamond. 

Daktari ni yule yule japo anaonekana akiwa na nguo tofauti. Swali ni je wapenzi hawa wanaumwa ugonjwa mmoja? Ama kuna kamchezo kaitwako 'Public Stunt' wanakacheza?

Labels: ,

BONGO MOVIE: Ney wa mitego naamin kabisa unatafuta jina lipande kupitia "Bongo Movie" tunaomba uwataje wahusika

Ney wa mitego akiwa katika pozi



            Msanii wa maarufu wa bongo movie nchini 'Divanesh aidan' kama anavyojulikana kwa jina la Nesh ambaye hivi sasa anatamba kwenye filamu mpya ya 'Glory of Ramadhan' aliyoshilikishwa na Ray. ameibuka juu nakumchana live' Mwanamuziki wa bongo flava nchini Ney wa mitego. Kitendo cha ney kuikashifu sanaa ya bongo movie nchini imechukizwa na wengi wana bongo movie akiwemo Nesh ambaye uvumilivu ulimshinda nakujikuta akimchana live' kupitia mtandao wa kijamii wa 'facebook alinukuliwa akisema.
         "Ney wa mitego naamin kabisa unatafuta jina lipande kupitia "Bongo Movie" tunaomba uwataje wahusika" Baada ya habari hizi kusikika Bongomixx iliamua kunyanyua waya nakumtafuta Ney mwenyewe aeleze lakini jitihada zilishindikana baada ya simu yake kuita muda mrefu bila kupokelewa.

Nesh 'kushoto akiwa na Ray
                                                             
                                            
                                                               
                                                                                                     

Labels: , ,

Mke: BABY MADAHA KANIPORA MUME WANGU..

                                    
Mke wa mwigizaji wa bongo movie 'Khadija kushoto. kulia ni Huyo mume akijirusha na Baby madaha
                                                            

MKE wa mwigizaji wa filamu Bongo, Slim Omar, Khadija Amir ‘Kay’  amemfungukia msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ kuwa amempora mume.

Akizungumza na mtandao huu  hivi karibuni nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar, Khadija alidai kuwa alimwagwa na Slim huku akiwa mjamzito na kwenda kupiga kambi kwa Baby Madaha.


“Mimi nalia na Baby Madaha jamani. Amenipora mume wangu, Slim. Mbaya zaidi aliniacha nikiwa na ujauzito kama hivi mnavyonioa. Lakini sijali kwa sababu naamini kama sikupangiwa niishi na Slim hata nikifanya nini haitasaidia.


“Nashangaa sana kufanyiwa kitu kama hicho na mtu ambaye ni rafiki yangu wa siku nyingi, bora angefanya mwingine lakini si Baby Madaha,” alisema Khadija ambaye ni Miss Shinyanga 2009.


Baby Madaha anayelalamikiwa kwa ‘wizi’ wa mume, alipopatikana kwa njia ya simu alisema yeye hayupo tayari kuzungumzia mambo yasiyo na msingi zaidi ya kutafuta fedha.


“Slim kweli namjua, nafanya naye kazi. Juzi tu hapa nilikuwa nashuti naye wimbo wangu mpya, ghafla ndiyo huyo mwanamke (Khadija) akaanza kunitukana na kudai nimemuibia mumewe.


“Sasa kama anadai wameachana anachokitafuta tena ni nini? Si amuache Slim awe huru kutafuta mtu mwingine?” alisema Baby Madaha pasipo kuweka wazi kama wanatoka na mwanaume huyo au vipi.


Jitihada za kumpata Slim ili kufafanua juu ya msimamo wake kwa wanawake hao hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Labels: , ,

HATIMAYEMKALI WA BONGO FLEVA CHIKU KETTO AOLEWA..

Mkali wa miondoko ya bongo flava Chiku Ketto akiwa kwenye vazi la harusi.
                                                                            
Walisema haolewi mbona kaolewa? Ni Chiku Omary Keto, 28, ambaye jana alionekana kwenye picha alizoziweka kwenye page ya Facebook zikimwonesha akiwa amevaa shela kama Bibi Harusi.

Picha hizo ziliwafanya marafiki zake wa Facebook washangae iweje ameolewa kimya kimya hivyo kama inavyoonekana hapo chini.


Hata hivyo baada ya kumuuliza kuhusiana na picha hiyo alisema ni picha za video ya wimbo wake mpya. Umenipata msomaji wa bongomixx..?
                                                     

Labels: , ,

Saturday, August 4, 2012

ROMA APATA AJALI MBAYA AKIELEKEA MORO KWENYE SHOW..

Muda mchache uliopita msanii wa kizazi kipya kwenye bongo hip hop ROMA amepata ajali mbaya barabara ya Morogoro. Roma anasema alikuwa yupo kwenye mwendo wakawaida ndio tairi la mbele lilipopata pancha na ndipo gari likaacha njia yake na kwenda kugongana uso kwa uso na fuso ambalo lilikuwa upande wa pili na gari hilo dogo alilokuwa akiendesha Roma kurudi lilipotokea.
Roma ananiambia kwa sasa anaelekea Hospital kwa check up zaidi ila aliokuwa nao kwenye gari hakuna aliyeumia wote ni wazima.

Roma akimwelezea police wa usalama barabarani kilichotokea mpaka kupata ajali hiyo mbaya.

Huyu ni mmoja kati ya marafiki wa Roma aliyekuwa nae kwenye gari wakielekea Morogoro kwenye show




                                                                               

Labels:

Friday, August 3, 2012

HATIMAYE AMINI NA LINAH KURUDIANA..

                         
MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo, Amini Mwinyimkuu ‘Amini’, amedai kuwa anatarajia kutoa ngoma mpya ambayo atamshirikisha mpenzi wake wa zamani Linah, ingawa bado ngoma hajaipa jina.

Amini na Linah walikuwa wapenzi walioshibana lakini walikuja kuachana kwa amani na upendo, na sababu kubwa za kutengana kwao hakuna anayejua zaidi ya wao wenyewe.

Akizungumza na Bongo Mixx, Amini ambaye kwa sasa yuko bize na ngoma hiyo ili iwe ya kimataifa zaidi, alidai kuwa kutoka na mawazo ya watu kuwa yenye ana chuki na Linah, sasa ameamua kumshirikisha katika ngoma yake ili kuweka wazi na kufuta kauli za watu wenye nia mbaya.

Wakati huo huo Bongo Mixx ilimvutia Linah waya, nakudai kuwa naye alidai kuwa ameamua kufanya ngoma moja na Amini, kwani wao ni wasanii na wanahaki ya kushirikiana ingawa anaamini kuwa kuna watu baadhi ambao wanaamini wao bado ni wapenzi wakati ishu hiyo yamesha isha zamani.
                                     

Labels: , , ,

Tuesday, July 24, 2012

HIVI NDIVYO MH: ZITO ZUBERI KABWE ANAVYODAIWA KUREJESHA PENZI LA DIAMOND NA WEMA SEPETU

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ametajwa kuwa kichocheo cha kurejea kwa penzi la vijana wenye umaarufu mkubwa nchini kwa sasa, Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’ na Wema Isaac Sepetu.

Uwazi, lina mkanda wa video, unaowaonesha Diamond na Wema pamoja kwa mara ya kwanza, baada ya muda mrefu wa kutupiana maneno mengi ya kashfa, huku kila upande ukimshusha hadhi mwenzake.
Diamond na Wema, walinaswa kwenye Tamasha la Kigoma All Stars, lililoandaliwa na Zitto kisha kufanyika Julai 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Shukurani kwa Zitto, kwani kupitia tamasha hilo, Diamond na Wema, waliweza kudhihirisha kwa kila mtu kwamba uhusiano wao sasa umerejea upya kwa kuambatana kimahaba ndani ya Mkoa wa Kigoma.

SAFARI ILIVYOKUWA TAMU
Watu wengi wakijua kwamba kuna uhasama mkubwa kati ya Wema na Diamond, Julai 17, mwaka huu, ilikuwa ni mshangao wa aina yake kwa waliokuwepo Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Kigoma, baada ya vijana hao kushuka wakiwa wameongozana.

Diamond akiwa amevaa shati jekundu na tai nyeusi, chini akiondokea suruali ya jeans rangi ya bluu iliyopaushwa kimodo, huku Wema akitokelezea kwa koti la rangi ya maziwa, ndani blauzi nyeusi, halafu wote wameyaficha macho yao kwa miwani nyeusi, waliwaka vilivyo ndani ya Ujiji, Kigoma.
Baada ya kuwasili Kigoma, Wema na Diamond walielekea Hoteli ya Tanganyika Beach (ipo ufukweni mwa Ziwa Tanganyika) ambako walipata pumziko walilohitaji kabla ya nyota huyo wa wimbo wa Mbagala, hajaelekea Uwanja wa Lake Tanganyika kwenye Tamasha la Kigoma All Stars a.k.a Leka Dutigite.

WEMA ALIFUATA NINI KIGOMA?
Minong’ono ilitawala kila kona ya Mkoa wa Kigoma kwamba Wema amekwenda kuwakilisha Leka Dutigite, hivyo wakataraji kumuona Uwanja wa Lake Tanganyika, akitoa sapoti yake kwenye tamasha hilo.
Wapo ambao waliacha shughuli zao kwa ajili ya kwenda kumuona Wema tu uwanjani lakini waliambulia patupu, kwani mrembo huyo hakuonekana kabisa.
Kutokana na hali hiyo, wale waliovumisha stori kwamba Wema amekwenda Kigoma a.k.a Lwama, walionekana wazushi wasiofaa kusikilizwa, bila kujua kwamba mtoto alijificha ndani ya Hoteli ya Lake Tanganyika Beach.

HAKIKA WANAPENDANA
Kama ukaribu wao ulisababishwa na tamasha lililoandaliwa na Zitto peke yake, basi wangekuwa na muonekano ‘feki’ sehemu chache wanazopita lakini kinyume chake wao walithibitisha wanapendana haswaa!

Diamond, alishindwa kujichanganya na wasanii wenzake aliokuwa nao kwenye shoo ya Kigoma kama akina Said Juma ‘Chegge’, Peter Msechu, Banana Zorro, Mwasiti Almasi na wengineo, badala yake muda mwingi aliutumia kuwa umbali wa mita sifuri kutoka alipo Wema.
‘Mtundu’ wa nyimbo mbili mpaka sasa, Nai Nai na Baadaye, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ndiye pekee aliyekuwa jirani na vijana hao maarufu, walioamua kurejesha penzi lao kupitia mwavuli wa shoo hiyo.

Kwa upande mwingine, ni kama vile waliamua kwenda kufanya tambiko nyumbani asili kwa mume mtarajiwa, yaani Diamond kwa sababu chimbuko la Wema ni Mkoa wa Tabora, japo baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, amejichimbia Zanzibar kwa miaka mingi.
Mtu mmoja, mwenye hulka ya kutopitwa na mambo, akamueleza ripota wetu kuwa Julai 18, wasanii hao walikwenda Hifadhi za Gombe na Mahale, mkoani humo lakini jioni yake, Diamond aliongozana na Wema mpaka kwa babu yake, eneo la Ujiji Posta, mkoani humo ambako walisomewa dua na Babu Nasibu.

RAHA NDANI YA TILAPIA HOTEL
Safari ya furaha kwa Wema na Diamond, ilihamia ndani ya Jiji la Miamba ya Mawe, Mwanza ‘Rocky City’ kwenye Hoteli ya Tilapia, iliyopo ufukweni mwa Ziwa Victoria, eneo la Capri Point, hiyo ikiwa Julai 19, 2012.

Habari zinapasha kuwa wawili hao, walipumzika kwenye hoteli hiyo kwa muda mfupi, wakati wanasubiri saa ya ndege yao ya kuwatoa Mwanza hadi Dar es Salaam ifike.

Ndege waliyopanda Diamond na Wema kutoka Kigoma, ilitua Mwanza saa 9:30 alasiri, hivyo kuanzia muda huo, waliutumia Tilapia Hotel mpaka saa 2:30 usiku, wakaripoti Uwanja wa Ndege wa Jiji la Miamba ya Mawe, kabla ya saa 3:50 usiku, usafiri huo wa anga, uliitupa mkono ardhi ya Mwanza mpaka Dar es Salaam.

AIR PORT DAR ES SALAAM
Mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra Sammi’, alionekana Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, kuanzia saa 4:45 usiku (Julai 19), hivyo kwa jicho la ripota wetu, ikawa wazi kwamba amekwenda hapo kumpokea mwanaye kipenzi, Diamond ‘Sukari ya Warembo’.

Kutokana na safari hiyo kuwa mguu wa Diamond uliambatana na wa Wema, kwenda kwenye shoo ya kutoa shukurani nyumbani kwao Kigoma, ni wazi Mama Nasibu (Mama Diamond) alikuwa pale pia kwa minajili ya kumlaki mkwe a.k.a Mka Mwana.

PW 415 YAWASILI DAR
Diamond na Wema, walipanda ndege ya Kampuni ya Precision Air, PW415 na ilipotimia saa 5:30 usiku, ilitangazwa kuwa ndiyo inawasili kwenye uwanja huo wa ndege wenye jina la muasisi wa taifa huru la Tanganyika na baadaye Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ‘Baba wa Taifa’.
Milango ya saa 5:52, Diamond na Wema, walipita kwenye mlango wa wanaowasili (arrivals gate), wakiwa sambamba na Ommy Dimpoz, walipokelewa na Mama Nasibu hadi sehemu ya maegesho ya magari uwanjani hapo.

Timu nzima, ilijipakia kwenye gari la Diamond aina Toyota Land Cruiser Prado, rangi ya fedha, wakatoweka eneo la uwanja huo.

DIAMOND KWA WASIWASI
Saa 6:14 usiku (Julai 20), Diamond alimpigia simu ripota wetu, eti akahoji kilichompeleka uwanja wa ndege. Mahojiano yalikuwa hivi;

DIAMOND: Kiongozi nilikuona Air Port, pale ulikuwa unafanya nini?

RIPOTA: Aah, kumbe uliniona? Mlivyojikausha nikadhani hamkuniona. Kuna mzigo
wangu nilikuwa naufuatilia pale.

DIAMOND: Mzigo wapi? Naomba uniambie ukweli.

RIPOTA: Acha hizo dogo, unafikiri mimi nilikufuata wewe? Tena ningejua unafika leo, halafu ujio wenyewe ni huo, ningetega kamera zangu na tuwapige picha za kutosha.

DIAMOND: Aah, usifanye hivyo kiongozi.
Baada ya mazungumzo hayo, Diamond kila alipopigiwa simu hakupokea mpaka gazeti hili linanyanyuka kwenda kiwandani.

UFAFANUZI WA WEMA
Wema alipopigiwa simu na ripota wetu, alijibu kuwa yeye na Diamond hawajarudisha mapenzi, isipokuwa hivi sasa wako karibu kama marafiki wazuri kwa ajili ya kusaidiana mambo mbalimbali.
“Kusema ukweli kwa sasa sijafikiria kurejesha mapenzi na Diamond ila tupo karibu kama marafiki,” alisema Wema.

ZITTO NAYE
Jitihada za kumpata Zitto aweze kuzungumzia kurejea kwa penzi la Wema na Diamond kwenye tamasha aliloliandaa, hazikuzaa matunda. Muda wote naibu huyo wa Kambi ya Upinzania Bungeni, simu yake ilikuwa imezimwa.

WANANCHI WAMPONGEZA
Fununu kuwa Wema na Diamond wamerudiana zilivuma kwa kasi ndani ya mitandao ya kijamii na maoni ya wengi yakaelekeza pongezi kwa Zitto, kwani kabla ya hapo, mastaa hao walikuwa na uhasama mkubwa.

UNAKUMBUKA?
Malumbano yao kwenye vyombo vya habari? Diamond alipomfedhehesha Wema baada ya kukataa kupokea fedha zake alizomtuza kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam Machi mwaka huu? Je, kauli nzito za Mama Wema, Mariam Sepetu kwamba Diamond ni kijana mbaya na hafai?

JIULIZE SASA
Mpaka hapo bado unabisha kwamba mapenzi ni upofu? Unaendelea kukataa kwamba mapenzi hayaulizwi kwa nini? Diamond alipoachana Wema, alitua kwa Miss Tanzania namba mbili 2006-07, Jokate Mwegelo, je, penzi lao limeyeyuka au bado lipo kwa sura gani?


Labels: , , ,

Thursday, July 19, 2012

IZZO BIZNESS NA BELLE9 WAKUTANA FACE 2 FACE.



Rapper anayeiwakilisha vyema Mbeya City,Izzo Bizness amekutana Face 2 Face na Mwimbaji mkali mwenye sauti ya hatari Belle 9 katika Ngoma yake mpya.
Izzo amefunguka na kusema yupo katika harakati za mwisho za ngoma mpya aliyomshirikisha Belle 9 na itatoka mwezi wa 8.
Ngoma hiyo inaitwa UTARUDISHWA. Beat ya ngoma hiyo imetengenezwa na mwana hiphop mkali rapper ONE THE INCREADIBLE, na ameingiza vocal katika studio itwayo Dirty Mode Record chini ya Tris.

Labels: