Saturday, July 7, 2012

Emanuel Okwi mchezaji halali wa Simba kisheria...


MCHEZAJI EMMANUEL OKWI NI MCHEZAJI WA SIMBA KISHERIA


 Makamu mwenyekiti wa timu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu akizungumza na mchezaji wake Emmanuel Okwi kwa njia ya simu  kutoka  nchini Uganda huku waandishi wa habari wakifuatilia mazungumza hayo.
Makamu mwenyekiti wa timu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu akionyesha mktataba wa timu ya Simba na mchezaji Emmanuel Okwi mbele ya waandishi wa habari
WAKATI Mshambuliaji Emmanuel Okwi amekanusha kusaini Yanga, uongozi wa klabu yake, Simba umesikitishwa na habari zilizovumishwa kwenye vyombo vya habari kuhusu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda kujiunga na wapinzani wa jadi, Yanga SC.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makamo makuu ya klabu Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema kwamba habari hizo hazina ukweli wowote, ni kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na zina lengo la kupotosha ukweli na kuwanyima raha wale wote wenye mapenzi mema na Simba.
“Gazeti kama la Spoti STAREHE limekwenda mbali zaidi kwa hatua yake ya kutaka kuufitinisha uongozi na wapenzi na wanachama wake kwa kudai kuwa uongozi unafikiria tu kumuuza Okwi bila ya kuangalia mkataba wake.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, mkataba wa Okwi umemalizika leo na ndiyo maana ameamua kusaini Yanga akiwa mchezaji huru,”alisema Kaburu na kuongeza;.
“Ukweli ulivyo. Emmanuel Okwi alisaini mkataba mpya wa kuichezea Simba mnamo mwaka jana na mkataba huo unamfanya kuwa mchezaji halali wa klabu yetu hadi mwaka 2013. Baada ya mkutano huu, nitawaonyesha waandishi nakala ya mkataba wa Okwi na Simba. Hivyo taarifa kwamba mchezaji huyo hana mkataba na Simba ni za uongo, uongo mtupu,”alisema.
“Hivi ninavyozungumza nanyi, Okwi yuko kwao nchini Uganda akishughulikia viza ya kwenda nchini Italia ambako anatarajiwa kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika moja ya vilabu vya Ligi Kuu ya Italia (Serie A),”alisema Kaburu.

Labels:

Friday, July 6, 2012

Diamond akiri kufundishwa kiingereza na Wema





Mwanamuziki maarufu wa bongo flava nchini Diamond the platnum juzi alikisanua 'live' kwamba kitendo cha yeye kuongea kiingereza vizuri ndani ya mjengo wa Big Brother Africa umetokana na kufundishwa na mpenzi wake waliotemana naye 'Wema Sepetu. Akiendelea kuchanika ndani ya kipindi cha XXL ambacho kinarushwa hewani na  radio ya Cloudz jijini  Dar es salaam, aliulizwa swali la kizushi na mtangazaji B12.