Saturday, August 25, 2012

Hasara 5 za ushauri wa rafiki kimapenzi





Watu wengi wamekuwa wepesi sana kukimbilia kwa rafiki zao ili kuomba msaada wa mawazo ya nini wafanye kwenye mapenzi. Imani iliyojengeka kwa watu wengi katika jamii yetu ni kuwa ushauri ni kitu muhimu sana kwa kila hatua.

Kwa mtazamo wa haraka haraka unaweza kuishia kwenye ukomo huo wa fikra na kuamini juu ya ushauri wa mtu kukufikisha mahali sahihi kwenye mapenzi. Unapokerwa na mpenzi unakimbilia kushauriwa na wakati mwingine hata unapotaka kuoa au kuachana na umpendaye, unamuomba rafiki yako ushauri.
Je, umeshawhi kufikiria hasara za kuomba ushauri wa kimapenzi kwa rafiki yako? Hebu ungana nami wiki hii ili nikumegee kidogo hasara za ushauri.

UTAKUPOTOSHA

Ni wazi kwamba kipimo cha uelewa kinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Ifahamike kuwa, uhodari wa mambo nao hutofautiana, mtu anaweza kuwa mahiri katika siasa na akaaminika kwenye jamii, lakini ukimpelekea suala la mapenzi anakuwa hajui kitu, hivyo ni rahisi kukupotosha.

Uchunguzi unaonyesha kuwa, wapenzi wengi sana hupotoshwa na rafiki zao wasiokuwa na uelewa wa kutosha juu ya tatizo au suala husika la kimapenzi. Ni vema kuwa makini unaposhauriwa.


UTARAHISISHA MAMBO

Mara nyingi washauri huwa si wao wanaokabiliana na mambo, hivyo ni rahisi kwao kupima vitu kwa juu juu tu na kushauri kirahisi rahisi. “Vipi kakupiga namna hii, aaa huyu si mwanaume kwa kweli ni bora ukaachana naye.” Anasema ni bora kuachana naye kwa sababu haumizwi na kuachana, unayeachana ni wewe anayekushauri.

“Mkubali tu bwana unalaza damu, hiyo tabia yake ya uhuni atabadilika, shosti unataka kuacha bahati ipite?” Kwa mshauri ni rahisi kusema hivyo lakini kumbuka ukubwa wa tatizo hatimaye utakabiliana nao wewe. Hii ina maana kwamba, unapofikiria kuhusu ushauri ufikirie pia kuhusu kushauriwa jambo kirahisi, ukiuvaa mkenge mwenye kuumia utakuwa ni wewe.

UTAKUGEUZA

Ulimwenguni kuna aina zaidi ya 1000 za mapenzi na kila mmoja anatajwa kupenda kwa staili zake. Mapenzi ni kama chembe hai nyekundu zilizopo kwenye damu ya mwanadamu ambazo zinaelezwa na wataalamu kuwa hazifanani hata kidogo. Uzoefu unaonyesha kuwa, washauri wengi hushauri kwa uzoefu wao, lakini je ni sahihi uzoefu huo uwe msaada kwa mtu mwingine?

Jibu ni hapana, kinachotokea mara nyingi kwenye ushauri ni mtu kumfanya mwenzake awe kama yeye alivyo, yaani apuuze aamue na apende kama staili yake, jambo ambalo haliwezekani kabisa kwenye mapenzi. Vipi Juma ageuke ghafla awe kama Hassan kwenye suala la mapenzi? Ushauri ni muhimu lakini upime kama unalingana na matakwa yako.

UTAKUONDOLEA UJASIRI

“Kwa maelezo hayo mumeo ni malaya sana, naona itakuwa vigumu kumbadilisha, ni bora ukaanza maisha yako kwa sababu kuna siku hali itakuwa mbaya.”
Huu ni ushauri ambao unaweza kumuondolea mtu ujasiri wa kukabiliana na tabia ya mumewe hadi kufikia hatua ya kumsaidia akaachana na tabia zake mbaya.

Ushauri huondoa ujasiri wa kukabili tatizo hasa pale anayekushauri atakapolipeleka suala lako kwenye njia ngumu isiyokuwa na ufumbuzi. Ikumbukwe kuwa anayeamini kushindwa ni mshauri lakini wewe kama mwanamke unaweza kusimama kutetea penzi lako na kuliweka sawa mpaka jamii ikasema: “Jamani huyu dada kamrekebisha kweli mumewe, hakuwa hivi alikuwa mlevi lakini sasa kaacha pombe.

UTAKUNYIMA FURSA

Kwenye mapenzi kuna fursa nyingi za mafanikio ambazo unaweza usizipate ukiwa mtu wa kusikiliza sana ushauri wa watu. Kuna wakati ambao unatakiwa usimame wewe kuamua kumpenda mtu ambaye jamii inaona kama utapotea.

Labels: ,

cheka kwa picha..

KWA SAHILI HII HAMNA KUIBIA HAPA..

HATIMAYE BAADA YA KUMTAFUTA SANA SASA TUMESHAMPATA..

NI KWELI IMETOKEA..

MWANAFUNZI MWANAFUNZI TU HATA USIMAMIE VIPI ATAIBIA TU..

JE, UNAHITAJI NA WEWE KUBADILISHA MAZIWA YAKO..??

WHAT'S NEXT..??

BURN CD'S

HUYU NDIYE JUSTIN BIEBER MWENYEWEEEEEEEEEEE...

USISHANGAE SANA HIZI NI MBOGA MBOGA TU..

OTEA ITATOKAJE HII PICHA..??

GOOGLE SEARCH 98%

VIMESHATUA HAPA BONGO HIVII..

USITOE SANA MACHO HILO NI BOGA TU..

WHAT'S NEXT..??

JAMANI TUACHENI NA BONGO YETU TUNAIWEZEA WENYEWE HAMNA CHA AIBU HAPA..

HATA HAPA NI SWIMMING POOL TU..

COMMENTS PLEASEEEEEEEE....

HUJAFA HUJAUMBIKA AU..??  TEH TEH TEH JOKES BHANA...!!!!!!!!!!!

WHAT'S NEXT...??

INGEKUWA BONGO ANGEITWAJE HUYU MTU..???

HAPA KITU CHA TWITTER, FACEBOOK, WHATSUP NA BONGOMIXX UNABURUDIKA UKIWA NDANI YA SHIMOO. HA HA HA HAAAAAAA..!!

Labels:

CHEKA WEEEEE..>!!!!!!!!!!


Mlevi Mmoja Alibatizwa
akazamishwa majini
Mchungaji akasema
tangu sasa hautaitwa
RAHIMU utaitwa Yohana
Umekua kiumbe kipya.
Mlevi alipofika
Nyumbani akachukua
BIA akaitumbukiza
kwenye ndoo ya maji
akasema kuanzia sasa
hutaitwa TUSKER
utaitwa FANTA alafu
akainywa......!!!!!
...!!!!!.tafakari chukua
hatua...ULEVI
NOMAAAA..






MTALII mmoja kaja BONGO akakutana na interpreter mmoja mswahili anaitwa MKUBYA wakaenda hotelini mambo yakawa hivi:

TOURIST:"Do you have vegetables here?"
MKUBYA:"Mnavyo vijimeza hapa?"

WAITER:"Vijimeza vidogo hatuna."
MKUBYA:"No sir,they dont have."

TOURIST:"Ok,fine do you have hotdogs?"
MKUBYA:"Sawa,je mnao mbwa moto?"

WAITER:"Loh! Bwana we hatupiki mbwa hapa!"
MKUBYA"They dont cook here."

TOURIST:"What type of snacks do you have here?"
MKUBYA:"Aina gani ya nyoka munauza hapa?"

WAITER:"We bwana ee hapa hatupiki aina yeyote ya nyoka mwache akale nyumbani kwao."

MKUBYA:"They dont cook any type of snacks here,maybe you can go back and eat at home."

TOURIST:"Ok,atleast give us cocktail juice."
MKUBYA:"Ok,basi tupatie hata juisi ya mkia wa jogoo."

WAITER:"Pumbavu,hebu tokeni na bangi zenu hapa,tena sasa hivi kabla sijakasirika!!"

MKUBYA:"Lets get out of here i think this man is crazy!!"
~Ne~






Saa mbili asubuhi jamaa bado hajarudi nyumbani kwake toka jana.Mke akakerwa sana,mwishowe akaamua kumpigia simu:

WIFE:"Uko wapi we mwanamume ovyo,muhuni mkubwa usiku mzima humkumbuki mkeo kazi kuzurura tu,mi nimechoka mpuuzi wewe unipe talaka yangu! Tena leo.....uko wapi?"

JAMAA:"Unakumbuka lile duka la sonara? Pale ulipoona ule mkufu wa dhahabu ukaupenda sana?"

WIFE:{akaanza kuwa mpole} "Ndio
mume wangu mpenzi,napakumbuka.Kumbe darling uko nje unatafuta mazuri ili mkeo nipendeze,nisamehe kwa hayo maneno yangu makali.Kwa hivyo ndo uko hapo umeamua kuununua...we nawe unanipenda kweli,asante sana mume wangu,najua umechoka nunua haraka uje unywe chai kabla ya hujaenda ofisini.Mwaaaah♥"

JAMAA:"Hapana sio hivyo nilitaka nikwambie niko kwenye bar karibu na hilo duka....kuna beer za offer nakunywa tokea jana!!"





Shahidi wa tukio la ajali akitoa ushahidi wake mahakamani..na hivi ndivyo ilivyokua:

Mwanasheria: "Ni kweli kwamba uliishuhudia ajali iliyotokea?"

Shahidi: "Ndio niliishuhudia."

Mwanasheria: "Ulikua umbali gani kutoka kwenye tukio la ajali?"

Shahidi: "umbali wa futi 31 na nchi 6 na robo."
Mwanasheria (akidhani atamtia mtegoni shahidi): "Vizuri, Je unaweza kuiambia Mahakama ulijuaje kama umbali huo uliosema ndo wenyewe haswaa?"

Shahidi: "Kwa sababu ajali ilipotokea nilichukua futi ya kupimia nikapima na nilijua some stupid lawyer would ask me that question."





Kulikuwa na jamaa wawili kipofu na kiziwi waliongozana wakawa wanaenda porini walipofika sehemu moja wakaona matunda wakaamua na apande juu ya mti ikabidi apande yule kiziwi alipofika juu ya mti akakanyaga tawi lililooza akadondoka chini bahati mbaya nguo zikabaki kwenye matawi akamwambia yule mwenzie niangalie kama nimepona yule kipofu akaenda akampapasa akamshika kwenye makalio akasema yayayayaa! Yaani meno yote mdomoni hayamo asijue kuwa ameshika makalio.







Jamaa aktika mizunguko yake kafika mahali akajiskia ana kiu akaenda nyumba iliyokuwa jirani na hapo akaomba maji ya kunywa.. Akaja mtoto na kikombe cha maziwa akampa. Jamaa alipomaliza akaomba aongezwe dogo akamletea tena maziwa.. Jamaa ikabidi aulize, '' vipi mbona mnagawa maziwa kwa wingi namna hiyo?'' dogo akamwambia kuwa panya alindumbukia kwenye maziwa ndio maana wote hapa nyumbani wameyakataa.. duh jamaa kusikia vile kwa mshangao akaachia kikombe chini kikavunjika.. yule dogo akapiga kelele eti '' Yalaaaaaaaaa kile kikombe Bibi anachotemea mate kimevunjikaaaaaaa....






Mchaga alipata ajali alipozinduka pale hospitali akauliza "nipo wapi hapa?" Nesi akajibu,"umepata ajali, hapa upo hospitali. Bahati mbaya umekatika mkono." Mgonjwa: Na je saa yangu ipo wapi ya Rolex? Ipo mzee, nesi alijibu. Nesi: Mkeo na watoto wapo hapa kukufariji. Mgonjwa: Yeuwi... Wamefunga duka?






Jamaa walikuwa
wanacheza mpira. Kwa
bahati mbaya mchezaji
mmoja akaanguka na
kuzimia. Refari alikuwa
mzungu lakini wachezaji wote ni waswahili.
Mchezaji mmoja akataka
kumwambia refari
(Mzungu) kuwa huyu
jamaa kazimia. Akafikiria amwambie nini
refarii kwa sababu refari
hajui kiswahili. Akafikiria
kuwa neno "kazi" ni "Job" kwa kizungu, na neno "mia" ni "hundred" kwa kizungu, akasema sasa
nimejua nini nimwambie
refarii, akamwendea
refarii na kumwabia hivi
"Hello refari this man
kajob handred".







Jamaa1 alitulia beach mara
akapita mzungu
akamuuliza "R U RELAX"
jamaa hajui k2 akajibu
"NO" akapita mwingne
akamuuliza vilevile jamaa
akajibu "NO AM
ALEX"....Akaamua kusogea
mbele akamkuta mzungu
ame2lia akamuu "R U
RELAX"mzungu akajibu
"YEAH!" Jamaa akampiga
bonge la bao
akamwambia "ebo!!!
Wananiangaisha mie 2
kumbe we ndo relax
umejificha huku nenda
uko wenzio wanakutafuta.






KUNA DOGO MMOJA WAKIKE ANARUDI NYUMBANI KWAO NA MADAFU MAWILI MKONONI,MAMA YAKE AKAWA ANAMUULIZAWAKINA JUMA NDIO WAMEKUANGULIA MADAFU? MTOTO AKAJIBU HAPANA MAMA WAMEKATAA KABISA NIMEPANDA MWENYEWE KUANGUA .MAMA AKAANZA KUGOMBA WASHENZI SANA HAWA WAKINA JUMA WALITAKA UPANDE TU WAKUCHUNGULIE CHUPI,,,KISCHANA KIKAJIBU ,,NA MIMI NILIJUA TU NDOMAANA NILIIVUA KABLA YAKUPANDA WAMEZODOKA EEE MAMA,,,,,,,,,,MAMA KABAKI NA MSHANGAO WAAJABU.








Mlevi anarudi na rafiki yake mgeni nyumbani kwake na kuanza kumuelekeza hii ni nyumba yangu na lile ni gari langu, wakaingia ndani wanalikuta njemba limelala na mke wa mlevi bila wasiwasi mlevi akaendelea kuelekeza kile ni kitanda changu, yule ni mke wangu na yule aliyelala naye ni MIMI. .




Labels:

Friday, August 24, 2012

Magazeti Leo Jumamosi Tarehe 25.08.2012












Labels: ,

Wednesday, August 22, 2012

STREET STYLE















Labels: