Leo katika tasfiri
zetu nitaanza na tafsiri ya Umuhimu wa Mawasiliano katika mahusiano ambao ni
msingi mkuu katika misingi mitano ya mahusiano ama ndoa bora.
Mawasiliano
mazuri katika mahusiano ni moja ya suala muhimu sana linaloweza kusaidia
mahusiano yenu yawe na mafanikio.
Siyo kila mtu
anajua namna bora na makini ya kuwasiliana kwa kuzaliwa nayo, hata hivyo
tunaweza kujifunza. Basi kama una matatizo ya mawasiliano mazuri katika
mahusiano yako unaweza kujifunza kwa kusoma makala hii.
Ukijifunza mbinu za
kuwasiliana kila inapobidi na kwa namna inayotakiwa utaweza kusaidia mahusiano
yako kuwa bora na yenye furaha na kuepuka kubaki katika mashaka ya ndoa yako
kuingia katika orodha ya ndoa zilizovunjika.
Mawasiliano
hayana maana ya kuongea tu. Kipengele muhimu sana katika mawasiliano ni uwezo wa
kuwa msikivu. Wakati mwingine ni hilo tu linahitajika, kusikiliza
tu!
Mwenzako anaweza
akawa anahitaji kusikilizwa tu ili kuweza kutatua tatizo ama kuondoa mashaka
yaliyokuwapo. Kama utahitajika kujibu ama kuelezea kuhusu jambo fulani basi
baada ya kumsikiliza mwenzako kwa umakini mkubwa wote wawili kwa pamoja mnapaswa
kujaribu kujadiliana na kufikia muafaka wa tatizo
husika.
Mawasiliano ni
suala pana kwa ujumla, ni pamoja na maneno ya kutamkwa na mambo ambayo si ya
kutamkwa-matendo ama ishara. Mbinu za mawasiliano makini katika mahusiano
zinajumuisha namna zote mbili za kuwasiliana na kuziainisha kwa
uhakika.Tuchukue
mfano, kama mpenzi ana hasira, anaweza akakaa amefumbata mikono kimya
akikutizama tu bila kusema neno. Hali kama hiyo ni jambo ambalo linahitaji
umakini wako wa haraka. Kama utanyamaza na kumwacha bila ya kufanya chochote
utasababisha ajisikie kususwa, kutohitajika na kupelekea mambo kuwa mabaya
zaidi. Kusoma sura na matendo ya mwenzako ni kipaji ambacho
unapaswa kufanyia kazi vyema. Kinakuwezesha kuelewa mambo mengi sana kuhusu
mwenzako anavyojisikia kwa wakati fulani na kugundua hata kama
anadanganya.Kama wewe ni mtu
makini na mwerevu basi unaweza kugundua mbinu mbalimbali za mawasiliano makini
kwa kutilia maanani tu mambo yanayoendelea katika mazingira uliyopo. Ni vyema
kama unahitaji msaada zaidi ili kuelewa mbinu mbalimbali za mawasiliano mazuri
ukahudhuria mafunzo maalumu au kusoma vitabu mbalimbali kuhusu jambo hilo. Hii
inaweza ikakugharimu kidogo lakini thamani yake itakuwa kama dhahabu pale ambapo
itaweza kukusaidia kuokoa ndoa ama mahusiano
yako.Mawasiliano mazuri
ni pamoja na kutoa kipaumbele hata kwa mambo madogo madogo na kumwonyesha
mwenzako kwamba anathaminiwa. Kumwambia asante mpenzi wako isiwe ni jambo gumu.
Kuonyesha kuridhishwa na jambo fulani ni ukarimu wa kawaida katika
maisha.Usichoke
ama kukata tamaa kutamka, “NAKUPENDA”, ama “ASANTE” au “POLE” ama muhimu zaidi
"SAMAHANI". Maneno haya ni vyema yakawa sehemu muhimu sana ya
mahusiano yenu. Kila mtu anahitaji kujisikia
anathaminiwa.
Uelewa ama
maelewano ni sehemu nyingine muhimu katika mawasiliano ambayo imeachwa bila
kufanyiwa kazi. Tukisema bila kufanyiwa kazi ina maanaisha kwamba mara nyingi
katika mazingira mbalimbali ya mahusiano, hayaulizwi maswali ya kutosha kuweza
kuweka mambo bayana. Tunadhania kwamba tunajua kile ambacho wenzetu
wanakiongelea bila kutaka kueleweshwa vizuri zaidi. Kudhania mara
nyingi kutakupeleka katika matatizo. Hivyo hakikisha unaelewa kwa
uhakika ni nini kinaongelewa. Kama huelewi, uliza maswali hadi pale kila kitu
kitakapokuwa wazi na kueleweka.
Ushauri
bora kwa suala hili ni kujifunza, kujaribu, kujaribu na kujaribu.
Jifunze mbinu za mawasiliano bora na makini katika mahusiano na kufanyia
majaribio kila siku. Baada ya muda yatakuwa kama asili yako na hutapata tabu
tena ya kufikiria namna ya kuwasiliana.
Kumbuka, bila
juhudi na kujitolea kuwa na mawasiliano makini na bora katika mahusiano,
mahusiano hayo ni sawa na mahusiano-mfu!
Anza
sasa kuwasiliana ipasavyo… na jenga mahusiano/ndoa
bora!