Sunday, July 8, 2012

WEMA SEPETU NA JACKLINE WOLPER NGOMA DROO..


Lile pambano lililokuwa linasubiliwa kwa hamu kubwa ndani ya tamasha la matumaini ndani ya uwanja wa taifa hatimaye lilifanyika jana na liliwakutanisha adui wawili wa bongo movie kati ya Wema Sepetu na Jackline Wolper. Mpambano huo mkali ambao ulianza kwa mbwembwe nyingi kabla na baada ya mpambano ambapo kila mmoja alikuwa na matambo kuwa atamgalagaza mwenzake vya kutosha. Kama kawaida ya mashabiki wao kazi ilikuwa ni macho kutazama na midomo kupiga makelele kwa shangwe na msisimko mkubwa ndani ya uwanja wa taifa. Mpambano huo ulichukuwa raundi mbili tu tofauti na ilivyotazamiwa ambapo maadui wote wawili walitoka ngoma droo huku kila mmoja akimpiga mwenzake vya kutosha.

Jackline wolper akijiandaa kuingia ndani ya uwanja kupambana na Wema Sepetu jana..



Kocha wa Wema Sepetu, Rashidi Matumla akimpa mbinu Wema sepetu jinsi ya kumpiga Jackline Wolper



Muamuzi akiwaachanisha Wema na Wolper baada ya kutupiana makonde..



Wema Sepetu akila tizi muda mfupi kabla hajaingia kwenye mpambano kati yake na Jackline Wolper

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home