Tuesday, August 7, 2012

Wema na Diamond wanaumwa ugonjwa mmoja?


Wema Sepetu akichukua vipimo
Diamond alipokuwa hospitali baada ya kuugua ghafla
Pengine huu si muda wa kuendelea kuspeculate tena iwapo Wema Sepetu na Diamond wamerudiana. Kuna mambo mengi yanayoonesha dalili kuwa wapenzi hawa wa zamani wamerudiana. Hawajasema hadharani lakini picha za hivi karibuni zinaweka wazi. 

Kuanzia zile picha za Kigoma kwenye video ya Leka Dutigite na zingine. Lakini inaonekana kama vile Diamond na Wema Sepetu wanaumwa ugonjwa mmoja. 

Wiki iliyopita Diamond alionekana kwenye picha akiwa amelala kwenye kitanda cha wagonjwa na akichukuliwa vipimo na daktari. Na sasa kuna picha ya Wema akiwa kwenye kitanda hicho hicho na akichukuliwa vipimo vilevile kama Diamond. 

Daktari ni yule yule japo anaonekana akiwa na nguo tofauti. Swali ni je wapenzi hawa wanaumwa ugonjwa mmoja? Ama kuna kamchezo kaitwako 'Public Stunt' wanakacheza?

Labels: ,

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home