Tuesday, August 7, 2012

Makutano show ya Fina yageuka gumzo la jiji


Orest Kawau akimkaribisha Fina Mango katika studio za Magic FM kwa ajili ya kuanza kuendesha kipindi chake kipya cha Makutano 

Kipindi cha kwanza cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango kilianza rasmi jumamosi ya wiki iliyopita. Huu ni ujio mpya wa Fina Mango baada ya kupotea kwenye redio toka wakati akiwa Clouds FM.

Katika kipindi cha Jumamosi Fina alianza kwa kuichambua sheria mpya ya mafao iliyopigiwa kelele na Watanzania wengi ambapo mwanasheria aliichambua na kuielezea ni kwa nini imepingwa na watu wengi kifungu kwa kifungu.
Fina Mango katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Zitto Kabwe na Lawrence Masha ambao kabla ya kufanya nao mahojiano kwenye kipindi ambapo walielezea masuala mbalimbali ndani na nje ya siasa.
Mheshimiwa Zitto Kabwe akiongea katika kipindi cha Makutano na kujibu na maswali ya wasikilizaji yaliyotumwa kupitia mitandao jamii
Baada ya hapo Mheshimiwa Zitto Kabwe aliiongea na Fina huku akijibu maswali mengi yaliyotumwa kupitia mitandao ya Twitter, Facebook na Jamii Forums ambayo mengi yalikuwa ya kuhoji kuhusishwa kwake kwenye kashfa ya rushwa, nia yake ya kugombea urais 2015 na uhusiano wake na baadhi ya viongozi ndani ya chama.

Timu ya Makutano Fina Mango, Orest Kawau na Mussa Kipanya katika picha ya pamoja baada ya kipindi.
Mheshimiwa Lawrence Masha akiongea na Fina Mango na kumuelezea mamabo mbalimbali ikiwemo historia yake ya kisiasa.
Wa mwisho kuongea alikuwa Mbunge wa zamani wa Nyamagana na Waziri wa mambo ya ndani Lawrence Masha ambaye alielezea historia yake ya kisiasa na sababu za yeye kushindwa uchaguzi mwaka 2010 kabla hajapewa nafasi ya kuchagua nyimbo 3 anazozipenda na kujibu maswali ya wasikilizaji.

Wengi walionyesha kufurahia ujio mpya wa Fina Mango hasa mjadala uliobaki kwenye mitandao ya kijamii baada ya mahojiano na Zitto Kabwe kumalizika.

Labels: ,

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home