Saturday, August 4, 2012

J.B ; BONGO MOVIE HAIWEZI KUFA KAMWE..


KUNA tetesi kuwa Klabu ya Bongo Movie inayoundwa na baadhi ya mastaa wa filamu Bongo, inaelekea kusambaratika huku mwenyekiti wao, Jacob Steven ‘JB’ akiibuka na kusema umoja huo hauwezi kufa ila unahitaji kuombewa.

Madai ya awali yalisema Bongo Movie inapumulia mashine ikiwa ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na kutokuwa na uongozi bora.

“Mimi naweza kusema kuwa Bongo Movie haiwezi kufa tena inahitaji kuombewa sana kwa sababu sasa hivi ukiwataka wasanii wa filamu unawapata kirahisi kuliko wale wa muziki, pia tunainua vipaji vya chipukizi, nadhani hao wanaosema tumesambaratika washindwe na walegee kabisa,” alisema Jb.



Mwenyekiti wa klabu ya Bongo Movie, Jacob Steven 'JB'
                                                                                 

Labels: ,

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home