*** Play gal – 56 (Revenge)
Ilipoishia…
“..ama nife mimi Tina..!, au Jerry..! sitamrudisha huyu mtoto
kamwe..!!”
Nilijisemea kwa sauti ya chini chini huku nikitokomea mpaka
kwenye geti la nje kabisa na nilipofika nje kabisa ndipo kwa mbaali nikasikia
tangazo kuwa kuna dada ametoroka na mtoto na amevaa suruali ya jinsi akiwa na
mkoba mweupe. Eti akamatwe popote alipo humu ndani ya stendi..
“..It’s too late Jerry..!! (Jerry umeshachelewa..!!)”
Niliongea kwa kujidai huku nikipanda dalaladala yakuelekea
Mbagala na nisijue naenda kwa nani na wala itakuwaje huko nieandapo na huyu
mtoto..
Sasa endelea…
Ile hali ya woga na kutetemeka ilishaanza kutoweka ndani ya akili na mwili wangu kwa
ujumla. Na sasa akili yote nilikuwa
nimeielekeza ni jinsi gani nitaishi na huyu mtoto huko niendako. Nilijiona mtu
tofauti sana kutokana na kuwa na mtoto japo si wakwangu lakini kwa jinsi
nilivyokuwa nambembeleza akilia hata akicheka. Nilikuwa nacheka naye kila
abiria allikuwa akinishangaa nakuona ni jinsi gani nilivyokuwa na kipenzi na mtoto
wangu japo ukweli si mtoto wa kumzaa mimi. Ilinichukuwa kama lisaa mpaka kufika
Temeke. Japo daladala ilikuwa inaelekea mbagala lakini kwa upande wangu
kutokana na kuchoka sana mwili na pia mtoto
alikuwa kashajisaidia hivyo nilitakiwa nimbadilishe nguo nikaamua kushukia
Temeke nakutafuta gesti ya bei nafuu uswahilini.
*******
‘Mji mwema guest house’ ndio gesti niliokuwa nimefikia Tina
mimi na huyu mtoto wa Jerry niliomuiba. Kwa sasa alikuwa amelala hivyo
nilipoingia tu chumbani nilimvua nguo zote kisha nikaifungasha vizuri ile
pampasi yake iliyokuwa imejaa kinyesi pamoja na mkojo nakuiweka katika mfuko wa
rambo nakuvitupia kwa pembeni. Nilipomaliza kumsafisha nilichukuwa pampasi ya
akiba ambayo ilikuwa katika huu mkoba mkubwa niliouchukuwa kwa mama yake na
huyu mtoto.
Usingizi ulikuwa wa shida sana kwangu nadhani hii yote ni
kutokana na kuchoka sana mwili na hata akili yangu. Mawazo mengi niliokuwa nayo
na mipangilio yangu ya baadaye kuhusu huyu mtoto ni kati ya vitu ambavyo bado
vilisumbua sana katika halmashauri ya kichwa changu. Nilifanikiwa kuupata
usingizi kwa tabu sana na nilipokuja kushtuka usiku wa manane napo sikuwa na
saa wala simu hivyo sikuweza kugundua imetimia muda gani lakini giza bado
lilikuwa ni tororo. Mtoto alikuwa anakoroma kuashiria kuwa alikuwa na usingizi
sana. Nilitamani japo kupata tena usingizi kwa mara ya pili lakini bado kichwa
changu kikaendelea kuwa na mawazo mgando ya kumuwaza Jerry kwa vitendo
alivyowahi kunifanyia kipindi cha nyuma.
“..Piga ua.! Lazima nije kumtafuta Jerry na nimuue kabisa
kwani adhabu ya kumchukulia huyu mtoto wake haitoshi.. yeye ndio aliofanya
mpaka nimepoteza ramani ya maisha yangu kwa ujumla..”
Nilijikuta naropoka mwenyewe kitandani nakufanya mpaka mtoto
ashtuke nakuanza kulia. Nilimtoa pale kitandani nakuanza kumbembekleza lakini
haikusaidia kitu zaidi ya kuzidisha kulia zaidi. Nilimchukulia japo ile nyonyo
yake ya kunyonyea maziwa ambapo ilibakiwa na vimaziwa kidogo alivyokuwa
amevihifadhi mama yake kwenye mkoba lakini bado haikusaidia kitu chochote.
Machozi yalikuwa mengi sana nakunisisimua mwili mzima kila nilipokuwa nikimwangalia
huyu mtoto. Alibadilika mwili nakuwa mwekundu kutokana na kulia kwa muda mrefu.
Nilijitahidi kumbembeleza hata kwa kutoa maziwa yangu nakumdanganyishia kama
namnyonyesha ndipo akanyamaza nakuanza
kunyonya maziwa yangu ambayo kiukweli hayakuwa yakitoa chochote.
“..Sasa huuuuyu mtoto nimuite jina gani..?”
Nilibaki nimeduwaa mwenyewe huku nikijisikia raha kwa
kunyonywa maziwa yasiotoka na kale katoto mpaka akapitiwa tena na usingizi.
Nilijiuliza maswali mengi sana juu ya jina la huyu mtoto kwani Jerry mara ya
mwisho alimuita Mama yake na huyu mtoto ‘Mama Brayan’ hivyo moja kwa moja huyu mtoto
ndio atakuwa ‘Brayan’. Lakini kwa upande wangu inanibidi nimbadilishe jina huyu
motto haraka iwezekanavyo.
“..Adrian..!!, Adrian..!! yeees..! nitamwita Adrian tu haina
hata ulazima wa kumuita jina la nyumbani kwetu kwani mtoto si damu yangu..?”
Niliongea kimoyomoyo huku nikijitandikia vizuri shuka
nakujilaza tena kitandani tayari kwa kuutafuta usingizi kwa mara ya pili.
~ BAADA YA WIKI TATU ~
Mtoto Adrian nilishamzoea na nilishamchukulia kama moja ya mtoto
wangu wa kumzaa. Pale gesti wahudumu wote wakajua ni mtoto wangu na hata
wakanipa jina la Mama Adrian. Uchangamfu wangu wa kuongea na kila mtu ni kati
ya vitu ambavyo viliwavutia wengi. Zile hela ambazo nilizichukuwa kwa Mchungaji
James nilipomuua kwa sasa zikawa zimeniishia, si kwa kula tu bali hata kwa
matumizi ya huyu Adrian. Ilifika kipindi natumia hadi elfu kumi na tano kwa
ajili ya matumizi ya mtoto tu. Ilinibidi kila siku niwe na pampasi tatu hadi
nne na kopo zima la maziwa ya ng’ombe kwa ajili ya kumnywesha. Sikutaka
kujihusisha na marafiki wa mbali nahii gesti kwani niliamini ndipo kujulikana
kwangu mpaka kwa Jerry. Habari za nyumbani kwa Baba na Mama yangu sasa nikawa
nimezisahau kabisa. Nilianza maisha ya kujitegemea mimi kama mimi tena bila ya
kuwa na msaada wowote huku asililimia mia nikiamini endapo baba au mama yangu
akagundua kuwa sipo chuoni muda mrefu ataumia sana. Sasa akili yangu yote
nikaielekeza katika kufanya mapenzi na watu tofauti tofauti ili tu nipate
chochote cha kuniwezesha kujikimu mimi na huyu Adrian. Kuna kipindi nilikubali
hata kuingiliwa kinyume na maumbile ili mradi tu nipate chochote na hata
wanaume wengine walikuwa wananiingia hivi hivi bila hata ya kutumia kondomu na
hata kunilipa.
Siri kubwa tatu ndizo zilikuwa zimekaa kichwani mwangu kama sheria
na kiapo cha kutokumwambia mtu yeyote
mpaka mwisho wa uhai wangu. Siri ya kwanza ni juu ya huyu mtoto si wangu ila
wote wanatambua kuwa ni wangu. Siri ya pili ni kuwa hapa nilipo nimejificha na nilishawahi
kufanya mauaji hivyo ni wazi natafutwa huko Mwanza na pia natafutwa na Jerry na
mkewe juu ya huyu mtoto wao niliotoroka naye. Na siri ya mwisho inayoniumiza
sana akili yangu ni juu ya ugonjwa huu wa ukimwi. Ni kweli nimeathirika
japokuwa dalili zake sijazipata bado lakini mara ya mwisho niliambiwa hospitali
kuwa nimeathirika. Na ndio siri iliyonifanya hata nishindwe kuendelea na masomo
kwa kuchanganyikiwa na pia hata niwafiche ndugu, wazazi hata na marafiki zangu
wote wanaonifahamu.
“..Binti leo nina buku tano tu..”
“..Twende tu haina shida ila tunatumia kondomu..”
“..aanhaa..!!, kondomu ya nini..?”
“..hheee..!!, we vipi..? basi niongezee ziwe elfu kumi
twende bila kondomu..”
Alikuwa ni mzee mzima kabisa ambaye ana uwezo hata wa
kunizaa, na kwa muda huu alikuwa meshazoea kuja kufanya mapenzi na mimi kwa
kutumia kondomu sasa leo naona kaja kivingine kabisa na anataka twende naye
bila kutumia kinga. Tulikubaliana naye nakuelekea mpaka chumbani kwangu nilipopanga
ambapo nilimchukuwa Brayani nakumlaza chini kisha nikapanda kitandani nakuvua
nguo zangu zote nakubakiwa na shanga tu kiuononi kwa ajili ya kuwadanganyishia
wanaume wapenda ngono.
“.. haya nipe changu kabla..?, huna navaa nguo hakuna
kufanya chochote..?”
“..hilo tu..! ondoa shaka..!!”
Yule mzee hakuwa mbishi, alichomoa noti ya shilingi elfu
kumi nakunipatia. Niliichukuwa nakuiweka kwenye nguo za Adriani pale chini
kisha nikamfuata huyu mzee mpaka kitandani. Nilianza kwa kumchezea kifuani
kwake. Hakutaka kuchezewa sana kwani haja yake nikufanya tu mapenzi na mimi hivyo akajiandaa tayari kwa kufanya
mapenzi. Akiwa kishavua nguo zote mara tukasikia mlio wa simu yake ikiita..
“.embu naomba simu yangu hapo kwenye suruali..”
Alinituma nimtolee simu yake. Haraka haraka nikainuka na
kwenda kumtolea na kisha kumkabidhi.. ile nampa tu simu ikakatika. Akaiangalia
namba nakuizima kabisa kisha akanigeukia kwa tabasamu nakuanza kufanya mapenzi
na mimi. Nilimuonea huruma sana kwakuwa nimeshaathirika hivyo nilimuona kuwa
naye anapoelekea ni huko huko. Kutokana na tamaa zangu za pesa hata sikutaka
kumzuia alifanya atakavyo na alipomaliza tu cha kwanza.
“..unataka kuongeza..?”
Nilimwambia kwa sauti ya taratibu na ya kimahaba huku nikimrembulia
macho. Yule mzee alitaka tena hivyo akachukuwa suruali yake akaniongeza elfu
kumi nyingine napo tukaanza tena kufanya mapenzi kwa mara ya pili. Tukiwa
katikati ya mapenzi mara mwanangu Adrian akaanza kulia kwa sauti yake ya juu.
Sikutaka kumbembeleza mpaka nimalizane kwanza na huyu mzee. Hivyo tukaendelea
tena lakini kwa safari hii mwanangu Adriani ni kama alikuwa amezidisha kulia
kwa sauti ya juu. Bado sikutaka kwenda kumbembeleza. Tukiwa tupo katikati ya
mahaba mara tukasikia hodi inapigwa
Mlangoni kwangu. Ilipiga kwa nguvu kuashiria kuwa mtu anahasira au anataka kitu
cha haraka. Hakukuwa na sauti nyingine yeyote zaidi ya kulia sana kwa mwanangu
Adrian na yule mtu kuendelea kupiga hodi kwa nguvu. Nilichokifanya nilimfanyia
yule mzee ishara ya kumnyamazisha kwa kutumia kidole changu kukiweka mdomoni,
kisha nikamchukua mwanangu Adriani hivyo hivyo akiwa analia nakumtupia uvunguni
mwa kitanda na baada ya hapo nikaelekea moja kwa moja mpaka mlangoni tena kwa
kujiamini huku nimejifunika khanga nakuufungua mlangu nusu.
“eenhe unasemaje..?”
Uso wangu kwa sasa ukawa umekutana moja kwa moja na Mmama
ambaye sura yake si ngeni kabisa machoni mwangu huku akibubujikwa na machozi
yalioambatana na kwikwi na nilipomuuliza tu kuwa anasemaje. Pale pale
alinisukuma nakuingia mpaka chumbani kwangu kwa nguvu…
*** Unavyodhani huyo Mama nii yupi..? Na Tina atafanyaje..?
*** Nini hatma ya Tina kimaisha..?
*** Usithubutu kusimuliwa story hii ndio kwanza imeanza kunoga
kwani mwisho wa hii ya 56 ni mwanzo wa
57..
**Jiandae kujua kilichompata Tina ndani ya Play gal – 57
~~~ Itaendelea~~~
Labels: andy ryn stories
1 Comments:
embu tupia comments zako hapa, unaonaje kitackachotokea hapo? ni mama yupi huyoo??
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home