Monday, September 3, 2012

***Play gal – 61 (Revenge)







Ilipoishia..

“..Jerry haiwezekani mwanangu wa damu yangu kabisa eti amchukue Tina anajua tulivyompata..?, embu subiri nakuja sasa hivi..?”
Aisha alionekana kuwa na hasira zaidi kwani aliinuka kwa hasira na kwa shari. Nilichomoka kwa haraka huku nikielekea chumbani kwangu kumuwahi mwanangu Adrian lakini kabla sijafika chumbani Aisha akawa tayari ameshaniona kwa mbali kidogo akaniita kwa sauti ya kupaza na ya ukali..
“..Tinaaaaaaaaaaaaaaa….??????????????”

Sasa endelea…

Nilionesha woga uliochanganyika na kusita sita huku nikibaki njia panda nisielewe nimsubiri Aisha afike karibu au niingie ndani kumchukuwa mwanangu Adrian.
”..aahh..??  liwalo na liwe bwana..?”
Nilijikuta najijaza moyo wa kijasiri huku  nikiingia mpaka chumbani kwa nguvu zote nikimchukuwa mwanangu Adrian ambaye bado alikuwa kapitiwa na usingizi mzito. Nilijitahidi kufanya haraka haraka nikakusanya vitu muhimu ikiwa ni pamoja na mkoba mkubwa uliokuwa na hela kidogo na nguo za mwanangu Adrian. Kadri nilivyokuwa naendelea kupaki kwa haraka haraka ndivyo na sauti ya viatu ilioashiria kuwa Aisha yupo njiani anakuja ilikuwa ikiendelea kunishtua ndani ya fikra zangu. Sasa nikawa Tina sugu haswaa tena yule ambaye hasikii la mkuu. Nilichukuwa khanga nakumfunga mwanangu Adrian mgongoni kisha ule mkoba nikauweka kwapani na baada ya hapo nikafanya ishara ya msalaba huku kichwa na mikono yangu nikikielekezea juu.
“..eeh Mwenyezi Mungu nisaidie nakunilinda..”
Nilijisalia kimoyo moyo nakuanza kutoka huku nikifuatisha mlango ule ule wakutokea. Ile nakata kona ya kutokea kwenye kikorido uso wangu moja kwa moja ukakutana na rafiki yangu Aisha.
“..unakwenda wapi na mwanangu unampkeleka wapi..?”
“..mwanako..? leo hii ndio amekuwa mwanako..? Aisha kipenzi nashukuru kwa wema wako ulionifanyia ila kumbuka huyo Jerry ni muongo kakudanganya kwanza sijawahi kuonana naye toka kipiindi kile tulivyomfanyia mchezo ule..??”
Nilijitahidi kumdanganya Aisha lakini ndio kwanza kama nilikuwa naamsha mishipa yake ya hasira kwani alivimba nakutuna mara mbili ya Aisha yule nimjuaye mimi. Hakutaka kabisa kuniamini hata chembe na alichofanya nikukimbilia moja kwa moja kunivua khanga ile niliyokuwa nimembebea mwanangu Adrian.
“..Aisha niache mbona huni..?”
Kabla sijamalizia kuongea chochote nilishangaa  Aisha kunitupia kibao katika shavu langu nakuanza kujihisi kizunguzungu. Sikutaka kabisa kumlegezea zaidi yakuendelea kuing’ang’ania ile khanga asiweze kuifungua kwani kama angeweza kuifungua ingekuwa rahisi kumchukuwa mwanangu Adrian.
“..Jerryyyy???????? Jerryyy  njoo nisaidie..?”
Maskini Tina mimi nikawa katika vita kubwa yakuteteta  mwanangu Adrian asiweze kuwa mikononi mwa Jerry na huyu Aisha kwani nilishajiwekea dhamira ya kutomwachia na kama nitafanya hivyo maisha yangu yatakuwa mabaya zaidi kwani sina tena kizazi wala uwezo wakuweza kuzaa Tina mimi.  Makelele aliokuwa ameyatoa Aisha yakumuita Jerry  tayari yalikuwa yameshapenyeza katika ngome ya masikio ya Jerry na kwa muda huu nilianza kuhisi sauti za viatu tena ikitembea kwa mwendo wa haraka haraka. Nilichokifanya niliinua mkono wangu nakuudumbukiza moja kwa moja mpaka kwenye mkoba nakuchomoa chupa ya maziwa ya mtoto ambayo ilikuwa bado na maziwa yamoto nakisha kumwagia Aisha usoni. Aisha aliinama chini nakuanza kutapatapa huku mikono yake yote miwili akijiziba usoni na kufikicha kwa yale maumivu niliyokuwa nimempatia. Aisha akiwa bado anagala gala pale chini, nikarudishia lile dumu la maziwa nakisha nikaongoza kuelekea sebuleni. Ilinichukuwa hatua tatu tu uso kwa uso na Jerry mwenyewe na tena safari hii aliweza kuchukuwa mikono yake nakuziba njia ili mnisieweze kutoka Tina mimi.
“..kwanza nahakikisha nakuua..?  na pili namchukuwa huyo mtoto  wangu pumbavu mkubwa wewe..?”
“..hapa tutauana na siyo kuniua na kuhusu mtoto  sahau laba nife naye hapa sasa hivi..? baradhuri wewe usiye na hata huruma kwa binadamu. Umeniharibia shule sawa nimekubali ila kuhusu kumpata huyu mtoto ilo sahau Jerry..?”

Hasira kali ziliendelea kunitawala ndani ya halmashauri ya ubongo wangu. Kwa safari hii mwanangu Adrian alikuwa ameshahamka na tayari alikuwa akilia kwa sauti ya juu. Nilitamani japo nimshike nakumbembeleza lakini sikuweza kwani tayari Jerry alikuwa karibu yangu na alikuwa kaniwekea mikono yake shingoni mwangu. Nilijihisi kutapika kwani Jerry alidhamiria kuninyonga kutokana na mikono yake kushikana vilivyo na shingo yangu.
“..nakufa jamani nioookooeenn..?”
Nilijitahidi labda kutoa sauti   huenda majirani watanisikia lakini wapi ? haikusaidia chochote zaidi ya Jerry kukaza zaidi mikono yake huku nikihishiwa pumzi nakuanza kutapatapa mithili ya wacheza mieleka wakiangushana. Kitendo cha mimi kuishiwa nguvu kilimpa faraja na nguvu ya ajabu Jerry yakuweza kunifungua ile khanga yangu niliokuwa nimembebea mwanangu Adrian na kisha akamchukuwa mwanangu Adrian.
“..twende mwanangu huyu shetani hafai angekuua..?”
Jerry alimwambia mwanangu Adrian huku akimbusu japokuwa alikuwa mdogo sana kwani hakuweza kuelewa chochote zaidi ya kutoa macho.  Jerry alifanikiwa kumchukuwa mawanangu mikononi mwangu na kwa safari hii hakutaka hata kumuaga Aisha kwani bado Aisha alikuwa anatapatapa huku akiendelea kufikicha macho yake yaliokuwa nimeyamwagia maziwa ya moto ya mtoto.
Nilijiona sijielewi elewi kwani kila nikitaka kuinuka bado nguvu ziliniishia kabisa na pia shingoni kwangu kulikuwa kunauma sana. Taryari nilianza kuvuta taswira siku niliomchukuwa Adrian pale Ubungo nakutokomea zangu nakufananisha lile tukio kama tukio hili alilonifanyia Jerry leo hii. Mawazo mengi yalikuwa yanaendelea kutawala akili yangu huku nikiwa kama mtu aliyepigwa na bumbuwazi kwani nilijihisi mwanangu Adrian yupo tu kuwa hii ni ndoto lakini jibu lilibaki pale pale kila nilipomwangalia Aisha akiendelea kutapatapa.
“..dada twende nimeshamaliza kazi..?”
Nilikuwa kama sijiamini amini kwani ndani ya muda mfupi nilimshuhudia mfanyakazi wa ndani wa Aisha akiwa kambebelea mwanagu Adrian huku kamzungushia khanga zile zile alizonipora nazo Jerry pamoja na mtoto.
“..unasemaje..? na Jerry yuko wapi..?”
Bado nilikuwa sijiamini amini kama mwanangu Adrian amerudi mikononi mwangu tena. Nilitoka haraka mpaka eneo alipokuwa amesimama yule mfanyakazi. Nilipata furaha ya ajabu kwani kiukweli sikuweza kuamini kama kweli mwanangu Adrian amenusurika kuwa mikononi mwa Jerry.
“..embu niambie umemfanyaje Jerry mpaka umempata huyu mtoto..?”
“..wewe mwenyewe si unamuona huyo Jerry hapo chini alivyo..?”
Niligeuka tena kwa mara ya pili nakumuangalia Jerry vizuri lakini bado alionekana akitapatapata huku pembeni kukiwa na sufuria kubwa.
“yaan bado sijaelewa chochote..?”
“..ujue nini dada..?”
“eeh niambie..?”
“..wakati mnagombana kuhusu mtoto hapo kwenye korido nilikuwa nikiwasikia tu kwa muda mrefu huku nikiendelea kumtayarishia dada Aisha maji ya kuoga. Kadri mlivyokuwa mnaendelea kugombana na maji ndivyo yalikuwa yanazidi kuchemka. Nilipomaliza ile natoka tu nije kumwambia kuwa maji tayari nashangaa nakuona wewe ukiwa chini unatapatapa vivyo hivyo na kwa dada Aisha. Kwa hiyo nilichoamua nikuchukuwa sufuria hivyo hivyo likiwa na maji ya moto nakumwagia jerry ambaye alikuwa kamchukuwa mtoto na kumwagia mgongoni mwake kisha nikamuhai kumchukuwa mtoto. Na nilipoimchukuwa mtoto nilimmalizia kumwagia Jerry yale maji ya moto sana mpaka eneo lote la usoni mwake kwani niliona yeye ndiye chanzo cha matatizo ya kumgombea huyu mtoto hapa..”
“..ohh ahsante sana kwa kunisaidia nakumsaidia huyu mtoto..?”
“..usijari Anti.. ila hapa mie kama nitakamatwa nitafungwa tu..?? hivyo nakuomba tutoroke wote samahani Anti twende kabla majirani wala mlinzi hajatokea hapa..??”
Kwakuwa huyu Dada alikuwa ameshanisaidia kumpata mwanangu  Adrian na pia alinisaidia kmteketeza Jerry hivyo haikuwa na budi kumchukuwa. Nilimpa mwanangu Adrian na kisha nikamfuata Jerry pale chini nakuanza kumsachi mifukoni mwake ili nitafute funguo za gari lake niweze kutoroka. Nillifanikiwa kuzipata ndani ya muda mfupi.
“..chumbani kwa Aisha wapi..?”
Nilimuuliza yule mfanyakazi akanionesha.
“..nipe huyo mtoto na nakupa dakika mbili tu uingie usachi anapoweka hela zake kisha kwa haraka urudi tutoroke kabla mambo hayajawa makubwa hapa.”
Yule mfanyakazi alifanya kama nilivyomuelekeza na ndani ya muda mchache tayari alikuwa amerudi kashikilia bahasha ndogo ilioonesha ndani yake patakuwa na kile nilichomuagiza.
“..haya twende haraka haraka na tukifika hapo nje usioneshe kuwa na haraka haraka mlinzi atatugundua sawa..?”
“..sawa nimekuelewa Anti..?”
Nilimchukuwa mwanangu Adrian na kisha nikatoka na yule mfanyakazi huku nikimsihi mlinzi afungue geti nimuwaishe mwanangu hospitali anaumwa ghafla. Aliniuliza kuhusu Jerry na Aisha wako wapi hivyo nikamjibu kuwa wako chumbani kwao wametuachia ufunguo wa gari hivyo tunaenda hospitali hapo jirani nakurudi na huyu mfanyakazi wameniambia niende naye anisaidie.
Ndani ya dakika chache tayari tulikuwa nje ya geti huku nikiendesha gari la Jerry. Pembeni yangu alikuwa yule mfanyakazi huku mwanangu Adrian akiwa anatoa tu macho pembeni yetu. Giza lilikuwa limeanza kuwa tororo kwani saa ya kwenye gari ilionesha tayari imeshatimu saa sita kasoro. Hata magari tuliopishana nayo hayakuwa mengi sana kwa usiku huu. Tulikuwa hatujielewi tunaelekea wapi lakini wazo likanijia la kuwa tuna pesa tulizozichukuwa chumbani kwa Aisha.
“..ile bahasha uliochukuwa si unayo hapo..?”
Nilimuuliza yule mfanyakazi niliokuwa nimetoroka naye.
“..ninayo tena wala haiko mbali hapa..?”
“..ni kiasi gani cha pesa ulichochukuwa..?”
“..sijui ila ngoja niangalie vizuri..”
Yule mfanyakazi aliichukuwa ile bahasha ambayo ilikuwa imetuna vilivyo kuashilia kuwa amechukuwa hela nyingi sana. Kadri alivyokuwa anaingiza mkono kwenye ile bahasha ndivyo nayeye alikuwa akibadilika sura nakutetemeka nakuwa kama mtu mwenye hasira sana. Ilinibidi kulipaki gari pembeni nakumuuliza.
“..vipi embu toa ni shilingi ngapi zipo hapo..?”
Maskini tina mimi nilikuwa nimeshaingia tena matatizoni kwani alivyochomoa ile bahasha haikuwa na pesa yeyote zaidi yakutoa bastola na kisha kunielekezea kwenye paji langu la uso.
“..samahani najua huna hatia ila inanibidi kufanya hivi..?”
“..jamani kwani imekuwaje..??  nimekufanyaje wee binti..?”
“..Anti..? wala hujanifanya chiochote ila ninachotaka kusema namtaka mwanangu na wewe shuka chini sasa hivi kabla sijakufyatua..?”
“mwanako..? yupi..?  huyu hapa Adrian…?”
“..ndio ni mwanangu kabisa  wa damu na mimi ndio niliokuwa nimemzaa. Siri kubwa ilioko ni ya mimi na dada Aisha kuhusu huyu mtoto. Dada Aisha pale unapomuona hawezi kupata ujauzito kwani ameharibika kizazi kwa kutoa sana mimba ovyo kipindi cha nyuma. Na Jerry alikuwa akihitaji mtoto kwa udi na uvumba lakini kwa Aisha ikawa haiwezekani na ndipo wakaamua kunishirikisha mimi nilale na mlinzi wa pale ili nishike mimba niwazailie mtoto ambaye ndiye huyu uliokuwa umempora kutoka kwao.
Inaniuma sana huyu mtoto kumuona akihangaika kwani nilijifungua kwa operesheni na hapa unaponiona bado nyuzi hazijakaza vizuri katika maumbile yangu ya sehemu za siri. Sasa sina jinsi zaidi ya kumrudisha mwanangu mikononi mwanangu na wewe sihitaji kukuua ila shuka mwenyewe niache na mwanangu nitajua nitakapoelekea..?”





*** Najua play gal haiwezi kuisha utamu hata siku moja na mwisho wa hii ni **Play gal – 80


***Ki blog nawaombeni sana tuishie hapa na punde kitabu kikiwa tayari muda wowote kuanzia hivi sasa nitawajulisha..


**Kama unakihitaji ni inbox ili nikuweke katika orodha ya watakaokipata au andika jina lako unalotumia facebook then kikiwa tayari nitakushtua..
By admin..
Andrew Carlos Andrew (Andy Ryn)
Executive director,
Rusago  entertainment company ltd.
+255 713 133633,
 Facebook; Andy Ryn

Labels:

Monday, August 27, 2012

***Play gal - 60 (Revenge)



Ilipoishia…

Chumba kilikuwa nikikubwa sana ambapo ndani yake kulikuwa na kila kitu. Kuanzia choo na bafu. Kitanda kikubwa. Nilimvua mwanangu Adrian nguo zake nakumpeleka bafuni ambapo nilimuogesha nakisha nikambadilisha pampasi, baada ya hapo nikaoga na nilipotoka kuoga tu Aisha tayari alikuwa chumbani kwangu kitandani na Adrian ananisubiri nitoke kuoga.
“..Tina nimekuletea nguo hizi hapa, mie huwa zinanibana sana si unajua kunenepa kwangu ovyo tena..!!”
“..Ooh..!!, ahsante Aisha..”
“..ila kuna kitu nahitaji ujue…

Endelea….

Mwili wote ukanisisimka kwa haraka na ghafla kuanzia kichwani mpaka miguuni. Kutokana na kule kutetemeka nilijikuta kuishiwa nguvu mwilini nakuhisi kama kojo linaanza kunidondoka mtu mzima huku akilini nikiwa na shauku kubwa ya kujua ni kitu gani hicho anachotaka kuniambia Aisha.
“…Eennhee shosti..!!  kitu gani tena hicho mbona waniacha roho juu na njia panda mwenzako....??”
“..njoo kwanza mpaka hapa kitandani.., halafu ukiwa katika kujifuta vizuri na kubadilisha nguo mimi nitakuwa nikikusimulia, sawa shosti wangu Tina..?”
“..ni sawa tu hamna neno, au mtoko nini jamani..?”
“..mbona una haraka kiasi hicho jamani hata sijakwambia ni kitu gani..?, siyo mtoko wala nini..??”
“..Sasa ni kitu gani hicho cha kunitia roho juu mwenzangu, wangwi wangwi hadi umeninyima raha na kunipa karaha kwa muda..?”
Muda wote Aisha ailionekana kama mtu wa masihara masihara kwani ni kweli alionesha kuna kitu anataka kuniambia, lakini hakuwa siriazi kwani alikuwa akicheka cheka huku akinipa mkono kwa kugonga.
“..hivi yule mchumba wako wa zamani ‘Jerry’ ushawahi kumuona..?”
Mapigo yangu ya moyo yalibadilisha uelekeo pale aliponitajia jina la ‘jerry’. Sikutaka kabisa kumsikikia Jerry  masikioni mwangu Tina mimi na hata sura yake kwani yeye ndio chanzo cha mimi kuishi maisha haya ya shida nakutangatanga mpaka hivi sasa.
“..kiukweli shosti wangu Aisha. Huyo ‘Jerry’ ndio kwanza nakusikia unamtaja wewe leo hii, kwani toka enzi hizo sikumtia machoni na si unakumbuka alichonifanyiaga kipindi cha nyuma mpaka tukamfanyizia nakumkata kata nanihii yake kwa kutumia viwembe si unakumbuka..?”
“”..hehe heee..!!, halooo!!! Nakumbuka shosti..!!, lakini nadhani yale yalishapita siku nyingi sana, ila kuna jipya nataka nikujuze shosti wangu Tina ambalo hulijui..?”
Sasa nikatuliza pumzi zangu huku nikimtolea macho Aisha aniambie ni kitu gani hicho..
“..haya niambie shosti kwani amekuwaje huyo Jerry..?”
“ni stori ndefu sana Tina lakini maadam upo nitakusimulia kila kitu na utajua nakuelewa tu huyo Jerry. Kwanza kabisa unajua kipindi kile tumemfanyizia  kwanza hakututambua kama ni sisi ndio tulimfanyia ule unyama wa kumkatakata nanii yake kwa viwembe hadi kumpelekea kuharibika njia ya kutolea mbegu za uzazi. Tina..?”
“nakusikia endelea tu..?”
“..najua hutaweza kuamini lakini inakubidi tu uanzae kuamini kwani Jerry kwa sasa amekuwa ni mtu wa karibu sana na mimi..?”
“..bado sijakuelewa elewa Aisha , unamaanisha nini haswa..?”
“..nimekuwa msaada mkubwa sana kwa Jerry katika maisha yake.. Kuna siku moja nilikuwa naelekea kufanya ‘shopping’ zangu pale Mlimani city na kwa bahati nikakutana nae uso kwa uso. Kwa kuwa nilikuwa katika kipindi kigumu sana cha chuo si unajua tena bumu likiisha tunavyotaabika sisi..?”
“..ni kweli..?”
“..basi nikajikomba Aisha mimi kwa Jerry nakujifanya namjua kuliko. Kwa kuwa siku hiyo alikuwa peke yake ikawa ni rahisi sana kumshawishi. Jerry alionesha yuko tofauti sana kwani alikuwa ni mtu mwenye msimamo haswaa. Lakini akaniambia yuko tayari kunigharamia kiasi chochote cha pesa endapo tu nitamtekelezea mambo mawili makubwa kwake..?”
“..hee makubwa..!!, mambo gani tena..??”
Akili yangu sasa ikawa kama imenivurugika huku nikibaki njia panda na nisielewe ni kitu gani hicho ambacho aisha ameambiwa na Jerry. Mawazo yangu yote yakanirudisha mpaka siku niliyoota kuwa nachukuliwa mwanangu na Aisha wakisaidiana na Jerry na kisha nikabakwa na vijana nisioweza kuwatambua..
“..inawezekana ile ndoto ikawa kweli na leo hii ikanitokea ‘live’..?”
Nilijisemea kimoyo moyo huku sura ikinibadilika nakumuangalia mwanangu Adrian pembeni. Hasira kali iliyoamsha misuli pembezoni mwa uso wangu huku ikihamasisha dukuduku kali moyoni. Japo alikuwa hajamalizia kuongea lakini akili yangu ikawa imeshabadilika kwa kiasi kikubwa nakuona huenda nitatekwa tu. kuwa hapa hapanifai hata kidogo tena.
“..ennhee Aisha ikawaje sasa ni mambo gani hayo mawili aliokuwa amekuomba huyo Jerry”..
“..aliniweka wazi kuwa yeye hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, amesumbuka sana kwa madaktari na mpaka kwa waganga wa kienyeji  lakini imeshindikana. Hivyo akaamua aoe na kuishi na mwanamke ambaye yuko sawa nayeye ambaye hana uwezo wa kuzaa ‘mgumba’. Basi akaoa lakini mtafaruku umekuja kwa wazazi wa pande zote mbili wanataka wajukuu.. kilichofanyika Jerry akaniomba kwanza nimtunzie siri na aibu hii kubwa ambayo amehangaika nayo kwa muda mrefu sana bila ya kuwa na mtoto. Pili akaniomba apandikize mbegu zake kwangu kutokea hospitalini ili nishike mimba nakumzalia.
“..hee.., halafu..?”
“..kama nitashika mimba atakuwa bega kwa bega na mimi mpaka nitakapojifungua. Atahakikisha amenijengea jumba kubwa nakuniwekewa kila kitu ndani nitakachokihitaji. Pia mkewe atamsafirisha nje ya nchi kwa siri siri bila ya ndugu kujua chochote na atakaporudi atakuta nimeshajifungua hivyo atamchukuwa mtoto nakumlea. Tulijaribu mbegu zake karibu mara tano lakini ikashindikana mimi kushika mimba kwa kutumia mbegu za Jerry. Kwa kuwa tayari nilishaingia tamaa ya hela na makazi kama alivyoniahidi Jerry. Nikapanga dili na dokta kisha nikasafiri mpaka Morogoro kwa mpenzi wangu Almeida akanipa ujauzito hivyo nikamsakizia Jerry kuwa tumeshafanikiwa kushika mimba. Jerry alifurahi sana kwa kuwa nilikuwa katika kipindi kigumu. Ilinibidi nisimamishe kwanza mambo yangu ya chuo kwa muda wa miezi tisa huku na ujauzito. Nikatafutiwa mfanyakazi wa ndani ambapo hata hivyo haikuwa ikipita siku bila Jerry kunipigia simu au kuniletea vitu mbalimbali vya kuniliwaza..”
“..kwa hiyo sasa huyo mtoto ukajifungua au ikawaje sasa..?”
“tina..? yani mtoto nilijifungua salama bonge la toto  mzuri kama huyo wa kwako. Hii nyumba na gari unavyoviona ameninunulia Jerry. Na mkewe ni rafiki yangu wa karibu sana na haipiti siku bila kunitembelea ama kunipigia simu na hivi nimeshamaliza chuo kabisa utamuona hapa kila siku..”
Mapigo yangu ya moyo yakaishiwa nguvu na kwa sasa yakawa kama yamepigwa ganzi ama kumwagiwa maji tena yale ya barafu ambayo hutoa kama moshi. Kichwa kilianza kunigonga huku nisielewe nianzie wapi. Sikuwa na hamu tena ya kukaa hapa japo ndio kwanza ilikuwa siku ya kwanza. Tukiwa bado kwenye maongezi na Aisha mara tukasikia sauti ya gari ikipiga honi huko nje. Hatujakaa sawa mara tena Simu ya Aisha ikaita, akapokea..
“..yeahh honey mambooo..!!! Ni wewe karibu namimi ndio kwanza nimemaliza chuo leo vipi upo peke yako ama..?”
“..sikuweza kutambua vizuri kuwa Aisha anaongea na nani zaidi yakuniaga kwa ishara huku akiniacha chumbani nakuelekea sebuleni..”
Mawazo mengi bado yaliendelea kunitawala ndani ya halmashauri ya ubongo wangu. Sikuweza kujitambua Tina mimi. Nilihisi kama ndoto. Nilivaa nguo kwa kutetemeka mithili ya mtu mwenye ukoma au yule anayeumwa malaria kali sana. Midomo yangu ilikuwa ikitetemeka kwa haraka haraka mithili ya maji yanapochemka katika sufuria. Nilibaki nimeduwaa peke yangu huku nikiwa sipati jibu wala ufafanuzi wa hili jambo. Nilichokifanya niliiinuka taaratibu kisha nikamweka mwanangu Adriani vizuri kitandani nakuanza kunyatanyata kuelekea sebuleni huku mwanangu Adrian nikimuacha akiwa amelala fofofo.  Niliendelea kunyata kimya kimya. Sauti za taratibu na za kimahaba kuashiria sebuleni kuna mtu na mume wake ndizo zilikuwa zikinivuta zaidi. Nilipokaribia nilifunua pazia la kuingilia sebuleni kwa utaratibu huku nikifumba jicho langu la upande wa kulia nakuliachia jicho la upande wa kushoto likifanya kazi yake ya kuangaza nakushuhudia tukio zima huku masikio yangu yakiwa sambamba na hilo tukio.
“..Jerry..?? Jerry..? oohh…!! Nooo…!!! Aisha noo..??”
Maskini Tina mie alikuwa ni Jerry katika himaya hii. Na kwasasa alionesha sura ya ukali huku akimuhadithia Aisha tukio zima nililomfanyia pale stendi miezi michache iliyopita. Alikuwa akimuomba sana Aisha msaada wa kunitafuta popote pale nilipo ili ampate mtoto wake. Jerry alikuwa akitoa machozi kama mtoto mdogo vile huku akimbembeleza Aisha wawe kitu kimoja kuhakikisha huyo mtoto anapatikana. Nikiwa bado nashuhudia Jerry akimbembeleza Aisha mara Aisha akainuka pale nakutoka huku akielekea sehemu ambapo nipo..
“..Jerry haiwezekani mwanagu wa damu yangu kabisa eti amchukue Tina anajua tulivyompata..?, embu subiri nakuja sasa hivi..?”
Aisha alionekana kuwa na hasira zaidi kwani aliinuka kwa hasira na kwa shari. Nilichomoka kwa haraka huku nikielekea chumbani kwangu kumuwahi mwanangu Adrian lakini kabla sijafika chumbani Aisha akawa tayari ameshaniona kwa mbali kidogo akaniita kwa sauti ya kupaza na ya ukali..
“..Tinaaaaaaaaaaaaaaa….??????????????”






*** Najua bado unatamani sana kujua kitakachompata Tina, hii sio ndoto ni ukweli kabisa, je unavyodhani ndio utakuwa mwisho wa **Play gal..? nini hatma ya Tina..?


*** kwanini mikosi haimuishi Tina kila kukicha..?


*** utamu ndio kwanza unazidi kunoga, chonde chonde usikubali kusimuliwa **Play gal ittakayofuata kwani ni nzuri zaidi ya hapa.  Jiandae kwa kumshuhudia tena Tina kilichompata ndani ya   ***Play gal – 61



***itaendelea>>>>>>>>>

Labels:

Thursday, August 16, 2012

**** Play gal - 59 (Revenge)



Ilipoishia…

Aisha aliongea kwenye simu kwa sauti ya ukali na yakikatili kisha ndani ya dakika chache mlango wa gari kwa upande wangu ukafunguliwa. Tochi zilinimulika kisha nikashikwa na watu nisiowafahamu halafu kwenye gari nikamshuhudia Jerry kiingia kisha akambeba yule mtoto na kuondoka zao na Aisha huku wakiniacha nimekumbatiwa na watu nisiowafahamu.
“..mnampeleka wapi mwanangu..??, mrudisheni..??”
Nilitoa makelele ya nguvu lakini haikusaidia chochote zaidi ya ile gari kutokomea huku wale wavulana waliokuwa wamenishika kwa kunikumbatia wakianza kunivua nguo zangu na zao tayari kwa kunibaka kwa zamu…

 Sasa endelea..


Walinigombania huku kila mmoja akinivuta huku na kule. Nilijitahidi japo kutoa sauti za makelele lakini haikusaidia kitu zaidi ya wale vijana kunipiga vibao na kisha kuniburuta mpaka eneo la kichakani kwenye giza totoro. Mwili wangu wote ukawa hauna thamani tena. Hawakuwa watu wazuri hata kidogo kwani walinifanya kwa nguvu na baada ya hapo wakachukuwa majiti nakunisokomeza ambapo walinisababishia maumivu makubwa na makali sana mwilini mwangu na haswa upande wa matiti yangu kwani walikuwa wakiyavuta na kuyafinya kwa kucha zao ndefu  na hata wengine kuyauma kwa kutumia meno. Ndani ya kama nusu saa walikuwa wameshaniharibu sana na pia walikuwa wameshatawanyika kila mmoja. Uwezo wa kusimama sikuwa nao zaidi ya kujiburuta chini chini huku nikitafuta japo barabara kuu ya kuweza kutokea. Tumbo nalo lilianza kuniuma sana tena kule kuuma kwa kuvuta maeneo ya chini ya kitovu.
“..nimekukosea nini eeh Mungu wangu..? Niangalie ninavyoteseka..? Weka japo mikono yako uniangaze na kunipa nguvu eeh  Baba..?”
Nilianza kumlaumu mwenyezi Mungu aliyeniumba nakujiona nimetengwa kabisa katika ulimwengu huu uliojaa mateso. Mikono yangu miwili ndio ilikuwa kama miguu kwa kujisukumia taratibu. Hatimaye baada ya mwendo kidogo nikaona gari kwa mbali linapita. Nilijaribu japo kutoa sauti ya ukali kwa makelele lakini ilishindikana kwani sikuwa na sauti kubwa tena na hata hivyo lile gari lilikuwa katika mwendo kasi hivyo halikuweza hata kuniona wala kusimama. Akili yangu sasa ikawa inamfikiria mwanangu Adrian niliyeporwa na rafiki yangu kipenzi Aisha akishirikiana na Jerry.
“..na lazima niwatafute na kuwaua kabisa..?”
Hasira yangu kwa sasa ikawa imefika kikomo kwani nilijihisi kutokwa na mishipa pembezoni mwa paji la uso wangu.  Nilijikuta nimepata nguvu za ajabu tena zile za ghafla. Niliweza kuinuka na kwa sasa nikawa natembea haraka  haraka mithili ya wanajeshi wakiwa katika mazoezi yao ya kwenda vitani. Haikunichukuwa  mwendo sana mara kwa mbele yangu kidogo nikakutana na dalaldala pamoja na teksi teksi zikiwa zimepaki huku eneo lile kukiwa na watu wakifanya shughuli zao mbali mbali. Hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi haraka nakutambua kuwa pale patakuwa ni kituo cha daladala na pia ni maeneo ya makazi ya watu. Mwili wangu sasa ukaondoka na hofu ya kuwa bado porini. Furaha yote nikaihamishia ndani ya lile eneo huku nikilisogelea kwa tabasamu ya hapa na pale. Nilipofika tu pale kwenye mwanga kila mmoja akaanza kunishangaa. Nilijiangalia mwili wote kisha.
“..Mamaaaaa..!!!!!, Mamaaaaaa…!!!”
Maskini Tina mimi kumbe nilikuwa sijavaa hata nguo. Nilikuwa uchi wa mnyama na mwili wangu kwa sasa ulikuwa umegandia damu damu ambazo zilikuwepo maeneo yote ya kuzunguka mapajani, tumboni mpaka kwenye maziwa yangu. Aibu kubwa niliipata lakini sikuwa na jinsi zaidi ya akili yangu kunituma nirudi kule machakani nilipobakwa nikazichukuwe nguo zangu. Kwa mwendo wa haraka niligeuka nyuma nakuanza kuondoka zangu. Hatua mbili tatu mara uso kwa uso nikakutana na gari.
“..Mamaa nakufaaa..!!”
Mwili wangu wote ulikuwa uvunguni mwa gari lilikokuwa linapita njia na kwasasa lilikaribia kunigonga. Ni breki tu ndizo zilisaidia. Yule aliyekuwa akiendesha gari alishuka huku anaongea maneno kwa ukali. Kadri alivyonisogelea na ile sauti ilivyokuwa ikitikisa ngome ya masikio yangu ndivyo nilivyokuwa nikisisimka nakupata na wasiwasi kama namfahamu. Aliponifikia karibu tu.
“..haa Aisha niwewe…? Kwanini unanifanyia hivi jamani..??, umenitumia vijana wanibake sawa…? Ukaona haitoshi ukanipora na mwanagu Adrian ukampa Jerry kisa pesa Aisha….??. Haya sasa si unataka unigonge..??, nigonge kabisa ili ndoto zako ziwe zimetimia si ndio..?”
Niliongea kwa jazba sana baada yakugundua kuwa kumbe aliyetaka kunigonga alikuwa ni rafiki yangu kipenzi Aisha na kwa muda huu alishuka nakuniongelesha kwa hasira zake. Nikiwa bado nipo uvunguni mwa gari huku Aisha akiniongelesha mara nikasikia sauti ya mtoto wangu akilia ndani ya gari.
“..Aisha mwanagu Adrian yuko wapi nasikia analia..??, nasikia analia.., yuko wapi..?”
Hasira kali nilizoinuka nazo pale chini zilinifanya nimsukume Aisha nakuongoza moja kwa moja mpaka kwenye mlango wa gari lake bila kugeuka nyuma. Nilifungua mlango ule kwa hasira zote nakumshuhudia mwanangu Adrian akiwa anatapika ovyo huku kafungwa fungwa ovyo na makamba shingoni mwake. Nilianza kumfungua haraka haraka lakini kitendo cha kumalizia kumfungua tu zile kamba nikahisi kimya kwa mwanagu Adrian. Nikamtingisha bado kimya. Nikamgusa na kuegemeza kichwa changu kifuani mwake japo nisikie mapigo yake ya moyo napo kimya. Akili yangu moja kwa moja ikanituma kuwa mwanangu Adrian sinaye tena yaani ameshafariki..
“Adrriiiiiiiiiaaaaaaaaaaaaaaaaaaannnnnnn….???????, Adriiiiiiiiiiiiiiaaaaaaaaan…..??”
Bado nilimuinua nakumtingisha tingisha lakini ndio kama nilikuwa najifurahisha na mdori kwani alishafariki muda mrefu.
“..Aisha..?? Aisha…??, Aishaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa..??”
Nilishtuka kutoka usingizini huku jasho likinitiririka mithili ya maji ya chemu chemu yakifuata mkondo wake huku kwikwi kali sana ya hasira na maji kwa ujumla vikinishika vilivyo. Kizunguzungu cha ghafla kilichonishika nilijihisi naona kama ukungu mbeleni mwangu kwani macho yangu yalikuwa yameishiwa nguvu ya kuona vizuri. Nilishusha pumzi nakupikicha macho yangu huku nisiamini kama vile vyote vilivyonitokea kuwa ilikuwa ni ndoto. Eti mpaka rafiki yangu Aisha akanigeuka nakumchukua mwanangu Adrian. Haraka haraka nikageuka pembeni yangu nakumwangalia mwanagu Adrian ambaye alikuwa bado amelala. Nilimuinua nakumbusu kwenye paji lake la uso.
“..inaonekana unampenda sana mwanao Adrian…?”
Aliniongelesha rafiki yangu Aisha ambaye kwa muda huu tulikuwa bado tupo njiani kuelekea nyumbani kwake na alikuwa akiendesha gari. Nilijilaumu sana kuota ndoto ya ajabu kiasi kile lakini haina jinsi kwani ndoto haipangwi. Nilimgeukia rafiki yangu Aisha mara mbili mbili huku nikioneshwa kutetemeka kwa uwoga nakudhani huenda nilichokuwa nakiota kikanitokea muda wowote.
“..ahh..!! itakuwa mandoto tu..!!, kwanza hawezi kunifanyia hivyo rafiki yangu kipenzi Aisha….”
Nilijikuta najifariji kwa kuongea kimoyo moyo huku nikiachia tabasamu kwa kumwangalia Aisha.
“..daah..!!, kumbe hujaacha kulala lala enhh..??”
“..ennhh..!!  shosti wangu kwa jinsi ninavyopenda kulala Tina mimi..? Yani ni kama ugonjwa kwangu toka kipindi kile tupo wote chuoni.., si unakumbuka hata darasani nilikuwa siingii ama nachelewa kisa usingizi..?”
“.. ni kweli.., ila umelala sana, yani tokea tunatokea pale chuoni CBE umelala tu na mwanako wote. Tumepita kwenye mafoleni pale Morocco, Kijitonyama hadi Mwenge kote bado umelala tu Tina..?”
“ndio hivyo..!!, wanasema usingizi mwanaharamu ukikushika. Lakini bado tu hatujafika aisha..?”
“ujue ni vijifoleni tu vya hapa na pale ndivyo vinafanya hivi, lakini isingekuwa hivi..? tungekuwa nyumbani muda mrefu sana.. lakini hatuna muda mrefu tunafika..”
Niliendelea kupiga  stori mbili tatu na rafiki yangu kipenzi Aisha japo bado kale ka uwoga ka ndoto kalikuwa kakinitawala ndani ya halmashauri yangu ya ubongo. Ndani ya dakika kama kumi hivi tulikuwa tunatazamana na geti kubwa  jekundu lililopambwa na nakshi nakshi za silva. Aisha alipiga honi kama mara mbili na punde akatoka kijana aliyekuwa amevaa kofia kuashiria kuwa huenda alikuwa ni mlinzi wa Aisha. Alitufungulia nakuingia mpaka ndani.
“..Tina karibu na jisikie uko nyumbani. Hapa ndipo ninapoishi na mume wangu niliyekwambia kuwa kwa sasa ni mfanyabiashara na wala si mtu wa kukaaa sana hapa bongo kwani huwa anakuja na kuondoka siku hiyo hiyo au anakaa hata siku moja mbili anaondoka zake. Karibu ndani kipenzi changu..”
Aisha alinikaribisha kwa ukarimu sana. Tuliingia mpaka ndani na akanikabidhi chumba kimoja.
“..hiki kitakuwa chumba chako kuanzia sasa Tina. Jisikie uko nyumbani na jisikie upo kwako rafiki yangu kipenzi Tina..”
“..haa..!!, sijui hata nikushukuru vipi mpenzi..!! Ahsante sana na ubarikiwe uendelee kuwa na moyo huo huo Aisha..”
Chumba kilikuwa nikikubwa sana ambapo ndani yake kulikuwa na kila kitu. Kuanzia choo na bafu. Kitanda kikubwa. Nilimvua mwanangu Adrian nguo zake nakumpeleka bafuni ambapo nilimuogesha nakisha nikambadilisha pampasi, baada ya hapo nikaoga na nilipotoka kuoga tu Aisha tayari alikuwa chumbani kwangu kitandani na Adrian ananisubiri nitoke kuoga.
“..Tina nimekuletea nguo hizi hapa, mie huwa zinanibana sana si unajua kunenepa kwangu ovyo tena..!!”
“..Ooh..!!, ahsante Aisha..”
“..ila kuna kitu nahitaji ujue…





*** je unavyodhani ni kitu gani hicho Aisha anachotaka kusema..?

*** Aisha ataishi vizuri na Tina kweli..? na nini hatma ya Tina katika story hii..?

*** stori ndio kwanza kama inaanza upya.. usithubutu uikose wala kusimuliwa inayofuata, ***Play gal 60

Labels:

Monday, August 13, 2012

***Play gal - 58 (Revenge)


                                                 






http://bossip.files.wordpress.com/2012/05/black-woman-crying.jpg?w=366
*** Play gal – 58 (Revenge)

Ilipoishia…
Niliumia sana moyoni kwa maneno aliokuwa akinitolea yule meneja nakujiona kuwa sifai na sina hata haja ya kuishi hapa duniani.
“..Adrian..? najua wewe huna hatia lakini sina jinsi inabidi nikuhifadhi nakukulea mpaka utakapokuwa kwa hali yeyote ile. Kubali vitu vyote utakavyokutana navyo ukiwa na mimi mpaka utakapokuwa mkubwa..?”
“Nilijikuta naongea na mwanangu Adrian japo alikuwa haelewi ninachokiongea kwakuwa bado mchanga sana lakini alitoa tabasamu nakunifanya nimbusu paji la usoni mwake nakuelekea kituo cha dala dala huku nisielewe ninapoelekea.
Sasa endelea…

“..nitaishi tu, Mungu ndio ajuaye..!”
Nilijikuta naongea peke yangu huku mwanangu Adrian nikimuweka vizuri kwani alikuwa ameshalala. Ilinichukuwa zaidi ya dakika karibu kumi nzima nikiwa nimezubaa peke yangu kituo cha daladala huku nikifikiria nitaelekea wapi na huyu mtoto. Akili yangu ikawa si ya Tina yule wa zamani bali ni ya Tina mlezi tena yule wa mlezi wa katoto kachanga ‘Adrian. Hatimaye nikaingia kwenye daladala iendayo mwananyamala na bado nilikuwa sijielewielewi.
“…Sitakuacha na wala sintokuwa msaliti kwako mwanangu Adrian..!!”
Bado niliongea peke yangu nilipoingia kwenye daladala. Baadhi ya abiria karibu wote ndani ya daladala walikuwa wakinishangaa sana na nadhani nikutokana na kuonesha sura ya huzuni na kuchanganyikiwa kwa mawazo juu ya mwanangu Adrian. Safari ya kutokea Temeke na kuelekea Mwananyamala ilianza. Njia nzima nilikuwa mtu wa mawazo tu haswa ni jinsi gani nitaishi huko niendako. Kuna wakati nilifikiria hata kwenda pale chuo kwa rafiki yangu Aisha japo anipe ushauri wa huyu mtoto na maisha yangu kwa ujumla lakini nikaogopa kwanza kuchekwa na pili mara ya mwisho nilipata uchizi nikiwa pale chuo hivyo kama wataniona na mtoto mdogo watanishangaaa sana na kunicheka kwa dharau.
“ahh..!! liwalo na liwe bwana…!!, konda nishushe hapo magomeni hospitali..?”
Nilijikuta naghairi kufika Mwananyamala ambapo ndio mwisho wa daladala hii na ndio malengo yangu kwa ujumla japo sikujua naenda kwa nani. Hivyo akili na mwawazo yangu ya ghafla yakabadilisha mwelekeo mzima wa safari yangu. Na kwa sasa nikashuka pale magomeni hospitali na mizigo yangu kisha nikaelekea upande wa pili nakupanda daladala ziendazo Posta kwa lengo la kushukia pale chuo cha biashara CBE ambapo ndipo nilipokuwa nasoma chuo na rafiki yangu kipenzi Aisha. Saa ya kwenye daladala ilikuwa jibu tosha kuwa inaelekea saa kumi na moja ya jioni. Haikunichukuwa muda sana kwani mwendo wa kutoka Magomeni hospitali mpaka chuo cha biashara CBE ni kama dakika saba hivyo nilishuka huku nambembeleza mwanangu Adrian mgongoni.
“..twende mwanangu.., hapa ndipo nilipokuwa nasoma..??”
Tayari akili yangu ilikuwa ni sawa na ya mwanangu Adrian kwani kuna kipindi nilikuwa nikiongea naye utadhani kuwa ananielewa nakunisikia kwa ninachokiongea. Mshipa wangu wa aibu niliuweka pembeni kwa muda nakuvaa sura ya mbuzi tena yule beberu kabisa. Nilijitwisha fuko langu la lambo kichwani huku kwenye kwapa nikiuweka mkoba wangu vilivyo na mgongoni nikimbeba mwanangu Adrian tena akiwa amepitiwa na usingizi.
“..embuuu…!! embuu…!!, hivi tulikuwa tunakaa nae bweni lipi tena..?? ok..!!  ok, nimeshakumbuka ghorofa  G namba 13..”
Chuo chote cha biashara CBE kilikuwa kimya sana na najua tu ikiwa hali kama hii ni dhahiri kuwa wanafunzi wote wanakuwa katika mitihani tena ile ya kumaliza chuo. Pale getini hakukuwa na mlinzi yeyote hivyo niliingia bila ya kuulizwa na mtu yeyote. Nilipishana na baadhi ya wanafunzi wachache sana tena wale masista duu na wengine mabrazameni bila ya kujali wala kujiogopa nilipishana nao huku akili yangu yote nikulifikia jengo G namba 13.
“..samahani Anti.. eti namba 13 kuna watu…”
Nilimuuliza mdada mmoja alioonesha sura yake ni ngeni kabisa machoni mwangu kwanza hata alikuwa hanifahamu kwani hakuonesha mshtuko wowote..
“..kwani wewe unamtaka nani..? Maana wanafunzi karibu wote wanafanya mitihani kasoro wale wa mwaka wa kwanza walioingia juzi juzi ndio wapo wapo humu mabwenini..”
“..sawa..!!, unamfahamu Aisha.., anakaa chumba hicho hapo juu namba 13..?”
“..Aisha..? Aisha..??, mhhh..!! Namfahamu wewe ni nani yake labda..?”
“..rafiki yake wakaribu na nimesoma naye hapa hapa chuoni..”
“””haloooo…!!! Eti rafiki yake wa karibu nimesoma naye..??, unahadhi wewe yakutembea na Aisha..? mwenye hipsi.., shepu shepu sio la mchina.. wakutembea na  ‘Verosa’ sio daladala, bajaji wala teksi..?  
Alinitolea maneno ya umbea na yakuumiza sana roho tena kwa pozi huku mdomo akiyumbisha kana kwamba sina hadhi yakuongea naye yeye wala huyo Aisha.
“..subiri hapo hapo nikakuangalizie maana nahisi utakuwa umekosea njia kwani Aisha nimjuaye mimi hawezi kuwa na mtu kama wewe ambaye hujui hata kujipodoa wala kuoga, mwenye kunuka makwapa na hilo toto sijui ndio kojo au lijimavi limeshajinyea..?”
Aliondoka huku akiendelea kuongea maneno yake machafu na kwenda kumuita Aisha. Niliumia sana moyoni nakutamani hata kumrukia na kumpiga lakini niiliogopa kufanya vurugu yeyote katika maeneo ya hapa chuoni. Kwani niliamini nitakamatwa na tena ikijulikana nilikuwa nasoma hapa ndio nitaharibu kila kitu.hivyo nikawa mpole tena mjinga haswaa huku nimejibanza nakumsubiri huyo alieenda kumuita Aisha. Ilinichukuwa dakika kama nne nzima peke yangu. Harufu kali ya marashi ya ‘adorable’ ilioambatana na sauti ya viatu ndio ilinifanya nianze kutoa mchozi kwani ndio marashi niliokuwa nayapenda kutumia na rafiki yangu kipenzi Aisha tulipokuwa wote chuo kipindi kile.
“..Aishaaaaa..?? Aisha rafiki yangu..?”
Nilishusha fuko langu chini nakumkimbilia aisha huku nikitaka kumkumbatia lakini nilipofika karibu yake tu akanikwepa nakunifyonza huku macho akiyatoa vilivyo.
“..wee chizi vipi..?”
“..jamani Aisha embu niangalie vizuri..? umeshanikumbuka rafiki yangu kipenzi..?”
“..sauti siyo ngeni.., embu nikumbushe unatokea wapi wewe..?”
Maskini Aisha alikuwa ameshanisahau kabisa japo mimi nilishamtambua. Kuharibika kwangu sura na nyele zangu za kipindi kile vilitosha kunibadilisha nakuwa Tina feki. Hata nilipomwambia Aisha kuwa naitwa Christina ama Tina bado alikataa nakusema kuwa Tina yule wazamani alishakuwaga chizi wa mitaani na siwezi kuwa mimi. Nilitumia dakika kama kumi nzima za kumulelewesha hadi akanitambua.
“..niwewe Tina..? hata bado siamini kipenzi changu kwanini umekuwa hivyo jamani..??, shetani gani aliokutembelea Tina ukabadilika kiasi kile..?? Ona sasa mwenzako nimetoka kumalizia mtihani wa mwisho.., si tungekuwa tumemaliza wote sasa hivi Tina..?”
Aisha aliongea na mimi kwa uchungu wa hali ya juu huku akitaoa machozi kama vile mtoto mdogo. Alinitoa mule chuoni ndani nakunipeleka mpaka nje. Tukatafuta sehemu nzuri ya baa nakukaa kisha nikaanza kumsimulia yote yalionikuta kipindi sipo naye. Aliona na kufananisha maisha yangu kama vile sinema tena ile ya tamthiliya ambayo ya muda mrefu sana. Nilimuelezea kuanzia tulipoanza naye mpaka nilipomucha chuo nakuanza kufanya umalaya wangu tena kwa kumficha mambo mengi. Kuhusu kuathirika kwangu nilimficha lakini kuhusu huyu mtoto nilimdanganya kuwa ni mtoto wangu ambaye nilizaa na mchungaji yupo Mwanza kaniacha na kunitelekeza na mtoto.
“..pole sana rafiki yangu Tina, ndio maisha jinsi yalivyo. Enhee kwa hiyo unaishi wapi kwa sasa..?”
“Aisha..? hapa unaponiona sina mbele wala nyuma na naishi peke yangu na huyu mtoto wangu tena kwa kutangatanga..”
Tukiwa bado tunaongea mara mwanangu Adrian akashtuka kutoka usingizini nakuanza kulia kwa sauti ya juu. Nilimfunua vizuri nakuanza kumbembeleza huku nikimtolea maziwa kwenye chupa..
“..mtoto wako mzuri sana Tina.., anaitwa nani..?”
“..anaitwa Adrian. Kwa hiyo sasa hivi Aisha umeolewa au maana nakuona na pete ya uchumba shosti..?”
Nilimbadilishia mada asiendelee kuniuliza juu ya huyu mtoto. Alikuwa amevalishwa pete lakini hakuniweka wazi kuhusu bwana anayeishi naye ila aliniambia tu ni mfanyabiashara tena wakimataifa hivyo si mtu wakukaa sana nayeye hivyo ni kama anaishi yeye na mfanyakazi tu. Alinichukuwa pale nakuelekea mpaka eneo aliokuwa amepaki gari lake na safari ya kuelekea kwake ikaanza kwani aliniahidi kuishi na mie mpaka mtoto atakapokuwa mkubwa ama mimi nitakapopata kazi yakueleweka nakujitegemea mwenyewe.
“..Aisha..?, wewe ni rafiki wangu wa milele.., na sina rafiki kama wewe..?”
Niliongea kwa kusisimka huku uso wangu ukitawaliwa kwa machozi ya furaha. Gari lake lilikuwa zuri sana na lenye vioo vyeusi vya kumfanya mtu wanje asiweze kuwaona. Mwanangu Adrian nilikuwa nimeshamshusha mgongoni nakumlaza siti ya pembeni yangu. Muda wote Aisha alikuwa akitabasamu nakucheka na mimi karibu njia nzima na hata tulipofika kwenye foleni alikuwa akinipigisha stori za chuo nilivyoacha gumzo kwa kila anayenijua na hata kitendo cha wazazi wangu kuja kunitafuta chuoni. Kifupi nilifarijika sana nakujiona mtu mwenye bahati ya mara nyingine tena bahati ya mtende.
“..kumbe Aisha unaishi mbali hiivi…??, enhee..!! ni wapi hivi shosti maana hiyo safari hatufiki tu..”
“..weee unafikiri mbali basi..?? ni hapo bunju tu.., tukivuka aka kapori tu tumeshafika..”
Gari ilitembea kama alivyoniahidi kuwa tukivuka tu kapori tumeshafika. Giza nalo lilikuwa limeshatanda. Nilihakikisha mwanagu Adriani nimemfunika vizuri kwa ajili ya baridi ya mule ndani ya gari. Tukiwa bado tupo eneo la kale kapori mara Aisha akasimamisha gari kisha akaanza kufungua droo za mbele ya gari yake kana kwamba kuna kitu amekisahau au anakitafuta amekikumbuka. Ghafla akatoa bastola ndogo nakunielekezea kichwani mwangu..
“..hapo hapo ulipo Tina..??, usitingishike wala kuongea chochote na nitakufyatua usipotii amri hii..??”
Mapigo yangu ya moyo yakabadilika nakuanza kutemeka huku kojo likichukuwa nafasi yake kunitiririka. Nikawa siamini kwa kilichonitokea. Nilibaki kimya kama alivyoniambia Aisha huku ile bastola iking’ang’ana katika paji langu la uso vilivyo tayari kwa kufyatuka. Sikuweza kujipindua zaidi ya kusikia tu Aisha akiongea na mtu kwenye simu.
“..kazi yenu tayari haya sasa mko wapi mnipe changu..?”
Aisha aliongea kwenye simu kwa sauti ya ukali na yakikatili kisha ndani ya dakika chache mlango wa gari kwa upande wangu ukafunguliwa. Tochi zilinimulika kisha nikashikwa na watu nisiowafahamu halafu kwenye gari nikamshuhudia Jerry kiingia kisha akambeba yule mtoto na kuondoka zao na Aisha huku wakiniacha nimekumbatiwa na watu nisiowafahamu.
“..mnampeleka wapi mwanangu..??, mrudisheni..??”
Nilitoa makelele ya nguvu lakini haikusaidia chochote zaidi ya ile gari kutokomea huku wale wavulana waliokuwa wamenishika kwa kunikumbatia wakianza kunivua nguo zangu na zao tayari kwa kunibaka kwa zamu…






*** kila siku stori inazidi kunoga je Tina atalipizaje kisasi kwa Aisha..?


*** Inamaana Jerry alishampanga Aisha kuwa kama Tina atatokea chuoni basi wamchukue mtoto halafu watalipana pesa..?? nini hatma ya Tina..?


******* hii ndio play gal (Revenge).., usithubutu kuhadithiwa hata inayofuata kwani ni kali sana zaidi ya hapa.


*** endelea kuwa nami kwa msisimko zaidi wa hadithi hii yenye ukweli ndani yake ya play gal 59

Labels:

Tuesday, August 7, 2012

***Play gal – 57 (Revenge)


Ilipoishia….

Nilichokifanya nilimfanyia yule mzee ishara ya kumnyamazisha kwa kutumia kidole changu kukiweka mdomoni, kisha nikamchukua mwanangu Adriani hivyo hivyo akiwa analia nakumtupia uvunguni mwa kitanda na baada ya hapo nikaelekea moja kwa moja mpaka mlangoni tena kwa kujiamini huku nimejifunika khanga nakuufungua mlangu nusu.
“eenhe unasemaje..?”
Uso wangu kwa sasa ukawa umekutana moja kwa moja na Mmama ambaye sura yake si ngeni kabisa machoni mwangu huku akibubujikwa na machozi yalioambatana na kwikwi na nilipomuuliza tu kuwa anasemaje. Pale pale alinisukuma nakuingia mpaka chumbani kwangu kwa nguvu…

Sasa endelea….

“...Hivi jamani nikupe nini ili uridhike mwanaume wewe..? eti Baba Jose..? Kwanini unanifanyia mimi hivi..? kitu gani hujaridhika kutoka kwangu..? kitu gani sikupi mie..?”
Nilishusha pumzi chini huku macho yangu nikiyatoa kwa tahamaki nikiendelea kumshuhudia yule Mama akilalama. Kumbe yule mzee niliokuwa nafanya nae mapenzi alikuwa ni mume wake wa ndoa. Na kwa sasa alikuwa kama kishamfumania akiwa na mimi. Aliendelea kumlalamikia sana mume wake huku akimshika shingoni vilivyo.
“..Lakini mama Jose..?”
“..lakini nini..? hivi kweli baba Jose ndio mchezo wako huo unaofanyaga..? lini utakuwa mume wangu..? kama ni watoto tunao wanne, badala tupange ni jinsi gani tutawatunza na kuwasomesha we ndio kwanza unahangaika nakutangatanga na visichana vidogo.. embu inuka twende nyumbani huko..?”
Bado yule Mama alionekana kuwa na hasira iliyoambatana na kwikwi kali kwani kila muda alikuwa akihema kwa shida huku akiishiwa pumzi kwa hasira ambayo alikuwa nayo ya kumfumania mume wake. Akiwa bado anagombana na mume wake mara mwanangu Adrian akaanza kulia pale chini yao.
“..tobaa..!!!, na tena kumbe binti mwenyewe ana mtoto mchanga..? wewe baba Jose nini unafanya jamani..? twende..!!, twende..!!, twende nyumbani nimesema..?
Nilisogea mpaka karibu yao kiuwoga woga huku nanyata mithili ya simba anaponyemelea kitoweo nakumchukuwa mwananagu Adrian nakuanza kumbembeleza huku  nikiwaacha yule Mama na mumewe wakiendelea kuvutana. Waliendelea kuzozana tena kwa sauti ya juu nakusababisha watu waanze kuchungulia madirishanai huku wakipiga kelele za uchochezi. Baada ya muda kama wa dakika tano nzima za ugomvi na kuvutana huku na kule ndipo wakaondoka zao wakiniacha nikiendelea kumbembeleza mwanangu Adrian ambaye kwa muda huu ni kama alikuwa akizidisha kulia.
Baada ya muda kama wa dakika kumi ndipo mwanangu Adrian akaanza kunyamaza nakunifanya nijisikie faraja tele moyoni. Tabasamu aliokuwa akiendelea kulitoa ni wazi kuwa alikuwa mtoto msikivu anapobembelezwa. Niliinua mkono wangu wa kulia nakuanza kumpapasa maeneo ya shingoni, mpaka usoni mwake. Alinishtua sana kwani mwili wake ulionekana wamoto sana. Kamasi za majimaji zilizokuwa zinamtiririka kupitia puani mwake ni wazi zilionesha kuwa anaumwa. Nilimvua nguo zake haraka haraka nakuanza kumuogesha. Nikiwa bado namuogesha mara tena nikasikia kama mtu anabisha hodi. Mwanzo nilionesha kusita lakini kadri nilivyokuwa naendelea kumuogesha mwanangu Adrian ndivyo na yule mtu alizidi kupiga hodi. Nilimtoa kwenye beseni lake la kuogea nakumuweka kitandani nakuelekea mlangoni kujua ni nani alikuwa anapiga hodi.
“Mama  Adrian..? Mambo..? Samahani unahitajika na meneja yupo mapokezi..?”
“..sawa Salma.., mwambie nakuja sasa hivi..?”
Alikuwa ni rafiki yangu wa humu ndani ambaye nayeye ni mfanyakazi na yupo mapokezi na kwa muda huu alikuwa amekuja kuniiita kuwa nahitajika na meneja. Ile hali yangu ya uwoga ilianza kunitawala tena, mwili wangu wote uliishiwa nguvu nakujihisi kama ile hali ya kutetemeka imenianza tena kwani safari hii nilikuwa natetemeka sana maeneo ya mdomoni na nywele kunisisimka. Nilichokifanya nilivaa nguo zangu haraka haraka na kisha kumchukuwa mwanangu Adrian nakuelekea mpaka mapokezi ambapo ndipo alipokuwa meneja akiniita.
“..naam bosi wangu nasikia unaniita..?”
“..ndio nakuita, hivi mama Adrian kwanini unataka kutuchafulia jina hapa mtaani..?”
“..kwani vipi meneja..?”
“ina maana hujui kitu ulichofanya muda si mrefu..?”
“..anhh..!!, unajua meneja ni kwamba..”
Kabla sijaanza kumsimulia meneja. Alinikatiza kuendelea kuongea neno lolote. Sura yake ilikuwa imembadilika na hakuwa kama meneja yule wa awali niliomzoea kwani alionekana dhahiri kuchukizwa na kile kitendo cha mimi kufumaniwa na yule Mzee.
“..sitaweza kuvumilia ujinga unaoendelea kufanya kila siku humu ndani. Katafute gesti nyingine za kufanya huo ujinga hapa kuanzia sasa hatukuitaji na mambo yako ibilisi we..?”
“..Jaribu kunisikiliza na mimi basi meneja..?”
“..hapana..?, hapana nimesema siwezi kukusikiliza tena wala kukuelewa kwa namna yeyote zaidi ya kukuona umeenda huko chumbani nakutoa kila kilicho chako na ufunguo wangu nauhitaji ndani ya dakika kumi, umenisikia na kunielewa..??”
Nilikuwa sina tena ujanja Tina mimi kwani pamoja nakumpigia magoti meneja huku nikitoa machozi ya hapa na pale lakini haikusaidia chochote wala kunielewa. Inaonekana kile kitendo cha mimi kufumaniwa kilimuuma sana nakuona kuwa amechafuliwa jina na atakosa wateja. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuelekea tena chumbani nakukusanya kila kilichokuwa changu. Sikuwa na begi lakuwekea nguo hivyo nilichukuwa nguo zangu na za mwanangu Adrian kisha nikaziweka kwenye fuko kubwa la lambo, na vitu vidogo vidogo kama chupa ya maziwa na vijipodozi niliviweka kwenye ule mkoba wa kipindi kile nilioondoka nao kutoka kwa mama yake na huyu mtoto. Nilirudi mpaka pale eneo la mapokezi nilipomuacha Meneja.
“..funguo wenu huu hapa..?”
“…Nenda huko hatukuhitaji tena hapa Malaya uliokubuhu wee..?”
Niliumia sana moyoni kwa maneno aliokuwa akinitolea yule meneja nakujiona kuwa sifai na sina hata haja ya kuishi hapa duniani.
“..Adrian..? najua wewe huna hatia lakini sina jinsi inabidi nikuhifadhi nakukulea mpaka utakapokuwa kwa hali yeyote ile. Kubali vitu vyote utakavyokutana navyo ukiwa na mimi mpaka utakapokuwa mkubwa..?”
“Nilijikuta naongea na mwanangu Adrian japo alikuwa haelewi ninachokiongea kwakuwa bado mchanga sana lakini alitoa tabasamu nakunifanya nimbusu paji la usoni mwake nakuelekea kituo cha dala dala huku nisielewe ninapoelekea.


*********


*** unavyodhani Tina ataelekea wapi kuishi na tawezaje kuishi na motto Adrian angali mchanga..?

*** Nini hatma ya Tina na nini mwisho wa story hii umeshaujua..?

*** Usikubali usimuliwe endelea kuwa na mimi katika Play gal – 58 kwani ndio kama story inaanza upya….

Labels:

Saturday, August 4, 2012

*** Play gal – 56 (Revenge)



Ilipoishia…

“..ama nife mimi Tina..!, au Jerry..! sitamrudisha huyu mtoto kamwe..!!”
Nilijisemea kwa sauti ya chini chini huku nikitokomea mpaka kwenye geti la nje kabisa na nilipofika nje kabisa ndipo kwa mbaali nikasikia tangazo kuwa kuna dada ametoroka na mtoto na amevaa suruali ya jinsi akiwa na mkoba mweupe. Eti akamatwe popote alipo humu ndani ya stendi..
“..It’s too late Jerry..!! (Jerry umeshachelewa..!!)”
Niliongea kwa kujidai huku nikipanda dalaladala yakuelekea Mbagala na nisijue naenda kwa nani na wala itakuwaje huko nieandapo na huyu mtoto..

Sasa endelea…

Ile hali ya woga na kutetemeka ilishaanza kutoweka  ndani ya akili na mwili wangu kwa ujumla.  Na sasa akili yote nilikuwa nimeielekeza ni jinsi gani nitaishi na huyu mtoto huko niendako. Nilijiona mtu tofauti sana kutokana na kuwa na mtoto japo si wakwangu lakini kwa jinsi nilivyokuwa nambembeleza akilia hata akicheka. Nilikuwa nacheka naye kila abiria allikuwa akinishangaa nakuona ni jinsi gani nilivyokuwa na kipenzi na mtoto wangu japo ukweli si mtoto wa kumzaa mimi. Ilinichukuwa kama lisaa mpaka kufika Temeke. Japo daladala ilikuwa inaelekea mbagala lakini kwa upande wangu kutokana na  kuchoka sana mwili na pia mtoto alikuwa kashajisaidia hivyo nilitakiwa nimbadilishe nguo nikaamua kushukia Temeke nakutafuta gesti ya bei nafuu uswahilini.




*******



‘Mji mwema guest house’ ndio gesti niliokuwa nimefikia Tina mimi na huyu mtoto wa Jerry niliomuiba. Kwa sasa alikuwa amelala hivyo nilipoingia tu chumbani nilimvua nguo zote kisha nikaifungasha vizuri ile pampasi yake iliyokuwa imejaa kinyesi pamoja na mkojo nakuiweka katika mfuko wa rambo nakuvitupia kwa pembeni. Nilipomaliza kumsafisha nilichukuwa pampasi ya akiba ambayo ilikuwa katika huu mkoba mkubwa niliouchukuwa kwa mama yake na huyu mtoto.
Usingizi ulikuwa wa shida sana kwangu nadhani hii yote ni kutokana na kuchoka sana mwili na hata akili yangu. Mawazo mengi niliokuwa nayo na mipangilio yangu ya baadaye kuhusu huyu mtoto ni kati ya vitu ambavyo bado vilisumbua sana katika halmashauri ya kichwa changu. Nilifanikiwa kuupata usingizi kwa tabu sana na nilipokuja kushtuka usiku wa manane napo sikuwa na saa wala simu hivyo sikuweza kugundua imetimia muda gani lakini giza bado lilikuwa ni tororo. Mtoto alikuwa anakoroma kuashiria kuwa alikuwa na usingizi sana. Nilitamani japo kupata tena usingizi kwa mara ya pili lakini bado kichwa changu kikaendelea kuwa na mawazo mgando ya kumuwaza Jerry kwa vitendo alivyowahi kunifanyia kipindi cha nyuma.
“..Piga ua.! Lazima nije kumtafuta Jerry na nimuue kabisa kwani adhabu ya kumchukulia huyu mtoto wake haitoshi.. yeye ndio aliofanya mpaka nimepoteza ramani ya maisha yangu kwa ujumla..”
Nilijikuta naropoka mwenyewe kitandani nakufanya mpaka mtoto ashtuke nakuanza kulia. Nilimtoa pale kitandani nakuanza kumbembekleza lakini haikusaidia kitu zaidi ya kuzidisha kulia zaidi. Nilimchukulia japo ile nyonyo yake ya kunyonyea maziwa ambapo ilibakiwa na vimaziwa kidogo alivyokuwa amevihifadhi mama yake kwenye mkoba lakini bado haikusaidia kitu chochote. Machozi yalikuwa mengi sana nakunisisimua mwili mzima kila nilipokuwa nikimwangalia huyu mtoto. Alibadilika mwili nakuwa mwekundu kutokana na kulia kwa muda mrefu. Nilijitahidi kumbembeleza hata kwa kutoa maziwa yangu nakumdanganyishia kama namnyonyesha  ndipo akanyamaza nakuanza kunyonya maziwa yangu ambayo kiukweli hayakuwa yakitoa chochote.
“..Sasa huuuuyu mtoto nimuite jina gani..?”
Nilibaki nimeduwaa mwenyewe huku nikijisikia raha kwa kunyonywa maziwa yasiotoka na kale katoto mpaka akapitiwa tena na usingizi. Nilijiuliza maswali mengi sana juu ya jina la huyu mtoto kwani Jerry mara ya mwisho alimuita Mama yake na huyu mtoto ‘Mama Brayan’ hivyo moja kwa moja huyu mtoto ndio atakuwa ‘Brayan’. Lakini kwa upande wangu inanibidi nimbadilishe jina huyu motto haraka iwezekanavyo.
“..Adrian..!!, Adrian..!! yeees..! nitamwita Adrian tu haina hata ulazima wa kumuita jina la nyumbani kwetu kwani mtoto si damu yangu..?”
Niliongea kimoyomoyo huku nikijitandikia vizuri shuka nakujilaza tena kitandani tayari kwa kuutafuta usingizi kwa mara ya pili.


~ BAADA YA WIKI TATU ~


Mtoto Adrian nilishamzoea na nilishamchukulia kama moja ya mtoto wangu wa kumzaa. Pale gesti wahudumu wote wakajua ni mtoto wangu na hata wakanipa jina la Mama Adrian. Uchangamfu wangu wa kuongea na kila mtu ni kati ya vitu ambavyo viliwavutia wengi. Zile hela ambazo nilizichukuwa kwa Mchungaji James nilipomuua kwa sasa zikawa zimeniishia, si kwa kula tu bali hata kwa matumizi ya huyu Adrian. Ilifika kipindi natumia hadi elfu kumi na tano kwa ajili ya matumizi ya mtoto tu. Ilinibidi kila siku niwe na pampasi tatu hadi nne na kopo zima la maziwa ya ng’ombe kwa ajili ya kumnywesha. Sikutaka kujihusisha na marafiki wa mbali nahii gesti kwani niliamini ndipo kujulikana kwangu mpaka kwa Jerry. Habari za nyumbani kwa Baba na Mama yangu sasa nikawa nimezisahau kabisa. Nilianza maisha ya kujitegemea mimi kama mimi tena bila ya kuwa na msaada wowote huku asililimia mia nikiamini endapo baba au mama yangu akagundua kuwa sipo chuoni muda mrefu ataumia sana. Sasa akili yangu yote nikaielekeza katika kufanya mapenzi na watu tofauti tofauti ili tu nipate chochote cha kuniwezesha kujikimu mimi na huyu Adrian. Kuna kipindi nilikubali hata kuingiliwa kinyume na maumbile ili mradi tu nipate chochote na hata wanaume wengine walikuwa wananiingia hivi hivi bila hata ya kutumia kondomu na hata kunilipa.
Siri kubwa tatu ndizo zilikuwa zimekaa kichwani mwangu kama sheria na kiapo cha  kutokumwambia mtu yeyote mpaka mwisho wa uhai wangu. Siri ya kwanza ni juu ya huyu mtoto si wangu ila wote wanatambua kuwa ni wangu. Siri ya pili ni kuwa hapa nilipo nimejificha na nilishawahi kufanya mauaji hivyo ni wazi natafutwa huko Mwanza na pia natafutwa na Jerry na mkewe juu ya huyu mtoto wao niliotoroka naye. Na siri ya mwisho inayoniumiza sana akili yangu ni juu ya ugonjwa huu wa ukimwi. Ni kweli nimeathirika japokuwa dalili zake sijazipata bado lakini mara ya mwisho niliambiwa hospitali kuwa nimeathirika. Na ndio siri iliyonifanya hata nishindwe kuendelea na masomo kwa kuchanganyikiwa na pia hata niwafiche ndugu, wazazi hata na marafiki zangu wote wanaonifahamu.
“..Binti leo nina buku tano tu..”
“..Twende tu haina shida ila tunatumia kondomu..”
“..aanhaa..!!, kondomu ya nini..?”
“..hheee..!!, we vipi..? basi niongezee ziwe elfu kumi twende bila kondomu..”
Alikuwa ni mzee mzima kabisa ambaye ana uwezo hata wa kunizaa, na kwa muda huu alikuwa meshazoea kuja kufanya mapenzi na mimi kwa kutumia kondomu sasa leo naona kaja kivingine kabisa na anataka twende naye bila kutumia kinga. Tulikubaliana naye nakuelekea mpaka chumbani kwangu nilipopanga ambapo nilimchukuwa Brayani nakumlaza chini kisha nikapanda kitandani nakuvua nguo zangu zote nakubakiwa na shanga tu kiuononi kwa ajili ya kuwadanganyishia wanaume wapenda ngono.
“.. haya nipe changu kabla..?, huna navaa nguo hakuna kufanya chochote..?”
“..hilo tu..! ondoa shaka..!!”
Yule mzee hakuwa mbishi, alichomoa noti ya shilingi elfu kumi nakunipatia. Niliichukuwa nakuiweka kwenye nguo za Adriani pale chini kisha nikamfuata huyu mzee mpaka kitandani. Nilianza kwa kumchezea kifuani kwake. Hakutaka kuchezewa sana kwani haja yake nikufanya tu mapenzi  na mimi hivyo akajiandaa tayari kwa kufanya mapenzi. Akiwa kishavua nguo zote mara tukasikia mlio wa simu yake ikiita..
“.embu naomba simu yangu hapo kwenye suruali..”
Alinituma nimtolee simu yake. Haraka haraka nikainuka na kwenda kumtolea na kisha kumkabidhi.. ile nampa tu simu ikakatika. Akaiangalia namba nakuizima kabisa kisha akanigeukia kwa tabasamu nakuanza kufanya mapenzi na mimi. Nilimuonea huruma sana kwakuwa nimeshaathirika hivyo nilimuona kuwa naye anapoelekea ni huko huko. Kutokana na tamaa zangu za pesa hata sikutaka kumzuia alifanya atakavyo na alipomaliza tu cha kwanza.
“..unataka kuongeza..?”
Nilimwambia kwa sauti ya taratibu na ya kimahaba huku nikimrembulia macho. Yule mzee alitaka tena hivyo akachukuwa suruali yake akaniongeza elfu kumi nyingine napo tukaanza tena kufanya mapenzi kwa mara ya pili. Tukiwa katikati ya mapenzi mara mwanangu Adrian akaanza kulia kwa sauti yake ya juu. Sikutaka kumbembeleza mpaka nimalizane kwanza na huyu mzee. Hivyo tukaendelea tena lakini kwa safari hii mwanangu Adriani ni kama alikuwa amezidisha kulia kwa sauti ya juu. Bado sikutaka kwenda kumbembeleza. Tukiwa tupo katikati ya mahaba mara  tukasikia hodi inapigwa Mlangoni kwangu. Ilipiga kwa nguvu kuashiria kuwa mtu anahasira au anataka kitu cha haraka. Hakukuwa na sauti nyingine yeyote zaidi ya kulia sana kwa mwanangu Adrian na yule mtu kuendelea kupiga hodi kwa nguvu. Nilichokifanya nilimfanyia yule mzee ishara ya kumnyamazisha kwa kutumia kidole changu kukiweka mdomoni, kisha nikamchukua mwanangu Adriani hivyo hivyo akiwa analia nakumtupia uvunguni mwa kitanda na baada ya hapo nikaelekea moja kwa moja mpaka mlangoni tena kwa kujiamini huku nimejifunika khanga nakuufungua mlangu nusu.
“eenhe unasemaje..?”
Uso wangu kwa sasa ukawa umekutana moja kwa moja na Mmama ambaye sura yake si ngeni kabisa machoni mwangu huku akibubujikwa na machozi yalioambatana na kwikwi na nilipomuuliza tu kuwa anasemaje. Pale pale alinisukuma nakuingia mpaka chumbani kwangu kwa nguvu…




*** Unavyodhani huyo Mama nii yupi..? Na Tina atafanyaje..?


*** Nini hatma ya Tina kimaisha..?

*** Usithubutu kusimuliwa story hii ndio kwanza imeanza kunoga kwani mwisho wa hii ya 56 ni mwanzo wa  57..
**Jiandae kujua kilichompata Tina ndani ya Play gal – 57

~~~ Itaendelea~~~

Labels:

Monday, July 30, 2012

*** Play gal - 55 (Revenge)


Ilipoishia…

Nilihuzunika sana nakuanza kuilaumu nafsi yangu kwa kutokufikiria. Nikiwa bado kwenye mawazo huku watu wakinishangaa mimi na huyu Mama. Mara huyu Mama akatoa sauti ya kuamuru kitu.
“.. jamani mapolisi binti mwenyewe ndio huyu hapa..!!, mchukuweni tumpeleke kituoni..”
Kumbe na mapolisi walikuwa wamenizunguka eneo lote nililokuwa nimezungukwa na watu ambapo walikuwa wamevalia nguo za kiraia. Walinichukuwa nakunipiga pingu huku umati wa watu ukinisikitikia kwa kitendo nilichokifanya cha kumuua mchungaji wao mchungaji James..

Sasa endelea…

“..inuka twende hukoo..!!, husikii..?”
Machozi yangu hayakuwa mbali na uso wangu. Yalianza kunibubujika huku nikijifanya mbishi na king’ang’anizi wa kutokuinuka pale kwenye benchi. Ule umati wa watu ukazidi kuongezeka mara mbili yake nakuanza kupiga makelele ya kuwachochea wale mapolisi huku baadhi yao wakiangua vicheko vya hapa na pale. Sasa Tina mimi nikawa sina ujanja zaidi yakuendelea kushikilia benchi lile la kukalia wageni nikibakiwa na butwaa.
“..jamani, sio mimi niacheni..?, mmenifananisha jamani..?”
“..akufananishe nani mshenzi mkubwa wewe..? na leo ndio utaenda kuozea jela Malaya wewe..?”
Nilijikuta mwili wangu wote unakosa nguvu huku mapolisi wakinibeba juu juu kama vile mzoga wa mnyama tena mnyama mkubwa. Walinipiga kwa ubishi wangu wakugoma kunyanyuka kisha wakaniingiza ndani ya gari yao ya kipolisi huku ule umati wa watu pale stendi ukiwa pamoja nao kunisindikiza kwa makelele na vicheko na baadhi kuhuzunika na nadhani walikuwa wakimpenda sana mchungaji James.
“..kama kufa wacha nife leo leo tu..!  Sitapenda nikaozee jela angali bado kijana hivi..?”
Nilijisemea kwa sauti ya chini chini nikiwa ndani ya ile gari ndogo ya polisi huku baadhi ya polisi wakiwa wamenizunguka chini ya ulinzi mkali na mikono yangu ikishikamana vya kutosha na pingu. Zile nguo zangu zote nilizokuwa nimezivaa nilihisi kama zimelowa tena chapa chapa na si kwa maji bali kwa jasho na kojo lililokuwa likinitoka ovyo kwa woga wa hali ya juu likiendelea kupenyeza ndani ya nguo zangu zoote.
Kila mtu alikuwa akiendelea na shuguli zake. Hakukuwa na baridi sana na wala jua lilichelewa kutoka. Mawingu yaliendelea kuvutana nakuashiria dalili zote za kushuka kwa mvua lakini upepo mkali uliokuwa ukivuma kutoka mashariki kwenda magharibi ndio uliosababisha kukatisha mvua. Makaratasi pamoja na risiti za mabasi zote zilikuwa zimejaa mavumbi yaliosababisha na huu upepo uliojaa vumbi. Milango pamoja na madirisha navyo havikuwa mbali katika kupiga makelele. Kwa sasa macho yangu yalikuwa yamenitoka na niliangaza huku na huku ilikuvuta japo kumbukumbu kujua ni sehemu gani hapa nilipo. Nilijiangalia tena mara mbilimbili nguo zangu kama zimelowa lakini ndio kwanza zilikuwa kavu tena zilizojaa ubaridi.
“..Dada..?, basi limeshafika vipi huendi tena..? basi hilo hapo mbele yako limetokea Kigoma..”
Amani na furaha tele iliniingia ndani ya moyo wangu nakuanza kuamini kuwa kumbe vyote vile nilivyonitokea muda si mrefu haikuwa kweli bali ilikuwa ni ndoto. Eti mpaka mmama mmoja akanijia tena pamoja na mapolisi wakanichukuwa nakuacha umati wa watu ukipiga makelele kwa vicheko. Nilijisachi vizuri mifukoni mwangu kuangalia kama zile hela nilizochukuwa kwa mchungaji James bado zipo. Kwa bahati nzuri zote zilikuwepo. Nilitoa shilingi elfu thelathini nakumkabidhi konda kisha akanikatia tiketi ya kuelekea Dar es salaam.
Njia nzima hadi tunafika Singida bado nilikuwa sijiamini amini Tina mimi. Ndoto niliyokuwa nimeiota ilishanijenga tena vibaya ndani ya halmashauri ya ubongo wangu nakuona sasa nipo katika wakati mgumu. Sikutaka tena kufumba macho kwani niliamini nitaanza tena kuziota zilie zile ndoto mbaya na nitaumbuka humu kwenye basi Tina mie. Siti niliyopata ilikuwa ni ya dirishani na tena nilikuwa peke yangu kutokea Mwanza mpaka tulipofika Dodoma ndipo abiria mwingine akapanda na kukaa pembeni yangu. Alikuwa ni Mmama tu na tena alikuwa na mtoto mdogo anamyonyesha. Mwili wangu wote ukaanza kunisisimka kila nikimwangalia yule mtoto. Alikuwa ni mzuri sana kuanzia macho yake, masikio na hata mdomo wake. Kila mama yake alivyokuwa anambembeleza ndivyo na mie nilikuwa nazidi kusisimka mwili. Hisia kali zilinivuta mpaka nikakumbuka kwa jinsi nilivyoathirika na ukimwi na tena kuhusu kupata mtoto nisahau kabisa milele yote kama alivyoniambia dokta.
“…Jerry..?? Jerry..?? Kwanini Jerry umenifanyia hivi mie..?? Kwanini..?”
Taaratibu wimbi la matone ya machozi likaanza kunidondoka huku nikiendelea kumwangalia Yule mtoto. Ni Jerry ndio alioaharibu maisha yangu yote japo ni tamaa zangu za mwili ila amechangia kwa kiasi kikubwa kuniharibu kimaisha na kimasomo kwa ujumla. Kwanza yeye ndie alieniambukiza ukimwi. Pili ndio alionisababisha mpaka kwa hasira niache masomo nakuanza kudili na ndugu zake nao kuaambukiza.
“..alaaniwe Jerry huko alipo..!! Na ole wake nikifika Dar..?”
Nilijikuta uzalendo umenishinda nakuanza kuropoka ndani ya basi. Kitendo changu cha kuropoka japo kwa sauti ya chini chini kilinifanya nianze kujishtukia lakini kumbe hakukuwa na mtu yeyote aliyeniangalia ama kunishtukia. Hata yule mama ndio kwanza aliendelea kupekuwa pekuwa vitu vya mtoto wake vizuri nakuvipanga. Mwendo wa masaa matano na nusu tulikuwa tumeshapapita Morogoro na kwa muda huu tulikuwa tukiitafuta Chalinze. Akili yangu yote sasa nilikuwa nimeielekeza kwa Jerry ambaye ndio chanzo cha kuharibu maisha yangu kwa ujumla.
”..nitahakikisha nimemuua mmoja mmoja kama nilivyomuua mchungaji James..”
Niliongea kimoyo moyo huku nikiikaza sura yangu kwa hasira ya hali ya juu. Kwa muda huu yule mtoto mchanga aliyekuwa akilia alikuwa ameshapitiwa na usingizi mkali. Yule mama alikuwa kimya akijisomea kitabu  chake huku akihuziunika na kucheka hapo hapo kwa alichokuwa akikisoma.
“..mmhh kwa kweli hii hadithi ni nzuri sana sijawahi kuona..”
Alinigeukia nakuniongelesha huku akiwa kaendelea kushikilia kitabu kile cha hadithi.
“..kwani kikoje..”
“..kinaitwa ‘SITAKI TENA’  yaani hadithi ya humu ndani mhh..”
“..ikoje kama za shigongo..”
“..hapana hii ina muundo fulani hivi lakini inavutia na kuteka hisia zangu. Tangu nimeanza kuisoma nyumbani Dar es salaam bado sijaimaliza na haipiti muda naendelea kuisoma tena, nimekuja huku Dodoma njia nzima bado naendelea tu kuisoma na ndio kwanza bado kurasa kama arobaini ndio niimalize.
“..inaonekana ni ndefu eenhh..?”
“..anhh ndefu sana..!!, ni ‘novo’ kabisa hii. Yaani kuna binti humu ndani anaitwa Levina. Maskini amepata shida toka mdogo mpaka amekuwa bado anaishi katika mazingira magumu tu..”
Kuanzia Chalinze njia nzima ikawa ni yule mama ananihadithia ile hadithi ya Sitaki Tena. Nilianza kutekwa hisia zangu kwani baadhi ya matukio aliyokuwa amefanya yameendana na mimi kabisa.
“..enhee ikawaje sasa huyo Levina..”
“..yaani hadithi inavyoanza Levina akiwa bado mdogo sana anacheza rede na wenzake na kwa bahati mbaya na haraka haraka kimchezo, Levina anaokota jiwe nakumrushia mwenzake huku akidhania ni mpira. Basi lile jiwe linamfikia mwenzake kwa nguvu nakujikuta mwenzake akikata roho pale pale. Sasa hapo ndio hadithi inaanza sasa..”
“ennhh, nipe uhondo japo kidogo..”
“..mkasa unaanzia anapelekwa rumande. Huko mapolisi wa zamu wanambaka na kuharibu usichana wake. Kesi yake ilikuwa inasua sua kwani baba yake alipoteza nguvu ubavu mzima kwa mshtuko hivyo kitendo cha kufuatilia kesi kikawa chini ya mama yake na baadhi ya mawakili waliokuwa wanamsaidia. Mwisho wa siku levina akatumikia kifungo cha maisha gerezani..”
“..Mungu wangu..!!, ikawaje sasa..?”
“..hakukuwa na ujanja tena ikabidi asafilishwe mpaka kwenye gereza la watoto watukutu la mbeya amabapo ndipo maisha yake yakaanza upya..”
“..pliiz..!! pliiz..!!, nakuomba uniazime niendelee kupata uhondo halafu tukifika Dar es salaam nitakuachia, wewe si cha kwako,?..”
“..usijali..!!, chukuwa, endelea hapa nilipomaliza kukuhadithia..”
Akili yangu yote ikawa imebadilika vya kutosha. Mawazo yangu yote nikayahamishia kwenye hii hadithi ya ‘SITAKI TENA’ iliyokuwa imetungwa na mwandishi maarufu na ninayempendaga siku zote ‘ANDY RYN.’ Nilishawahi kusomaga hadithi zake kipindi cha nyuma facebook ila hii sijawahi kuisoma. Mwendo wa masaa mawili na nusu ulinitosha sana kuisoma hadithi robo nzima ya kile kitabu huku nikitamani kujua mbeleni. Sikuwa na ujanja tena kwani tulikuwa tumeshaingia ndani ya hili jiji la Dar es salaam. Giza lilikuwa limeshatanda muda mrefu tu kuashiria kuwa ni usiku japo sikufahamu ni usiku wa saa ngapi. Nilimkabidhi yule mama kitabu chake. Alikuwa na mizigo mingi chini ya basi hivyo akaniomba nimshikie mtoto wake na mkoba wakati wakushuka ili ahakikishe mizigo yake asije akaibiwa. Kwa upande wangu sikuwa na mzigo wowote hivyo nikamsaidia kubebelea mkoba wake na mtoto wake nikambeba kifuani kama mwanangu vile kisha nikaongozana na huyu mama kushuka.
Kitendo cha kutangulia kushuka yule mama akapokelewa na mwanaume huku akikumbatiwa. Halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi haraka haraka nakutambua kuwa inawezekana akawa ndio mumewe. Sikumuona vizuri usoni kwa sasabu ya kukumbatiana na yule mama pia giza giza na mwanga ulikuwepo kidogo tena ile wa ndani ya basi japo kwa sauti zao ndizo ziliweza kupenyeza ndani ya ngome ya masikio yangu.
“..mwanangu Brayan yuko wapi..?”
“..Si huyo hapo amembeba huyo dada..?”
Aliongea yule mwanaume kwa sauti ya ukali naya nguvu akimuuliza mkewe huku akiacha kumkumbatia nakuangaza huku na kule ndipo jicho lake likakutana moja kwa moja na langu.
“…Tinaaa..? wewe si Tina wewe..?”
Alikuwa ni yule yule mvulana niliokuwa nikimchukia maishani mwangu na ndio yule aliyenipotezea malengo yangu ya kimaisha yote. Si mwingine bali alikuwa ni Jerry. Na kumbe huyu alikuwa ni mtoto wake. Nilijiuliza maswali mengi papo hapo japo sikupata jibu kwani ninavyokumbuka kuwa Jerry aliambiwa kuwa hawezi kumzalisha mwanamke kutokana na kwanza kuathirika na ukimwi na pili tulishawahi kumkata kata nanii yake na viwembe mimi na rafiki yangu Aisha na tulihakikisha tumeikata mirija yake yote inayopitisha mbegu za uzazi na hadi akazimia na kuwahishwa hospitali kipindi cha nyuma.
“..Tina mlete mwanangu nimesema..?”
Kwa sasa Jerry alikuwa amebadilika nakuwa mkali sana huku akinisogelea karibu. Mke wake alikuwa akimvuta kana kwamba aniachIe nakuwa mimi ni mtu mzuri tu tangu nimetoka naye safarini. Kila wakijibizana Jerry na mkewe ndipo na mimi nikapata nafasi ya kuwazunguka mpaka kwenye basi jingine nikalizunguka tena basi jingine nakuwatoroka pale pale pale huku nikiwa nimemshikiria mtoto wao.
“..ama nife mimi Tina..!, au Jerry..! sitamrudisha huyu motto kamwe..!!”
Nilijisemea kwa sauti ya chini chini huku nikitokomea mpaka kwenye geti la nje kabisa na nilipofika nje kabisa ndipo kwa mbaali nikasikia tangazo kuwa kuna dada ametoroka na mtoto na amevaa suruali ya jinsi akiwa na mkoba mweupe. Eti akamatwe popote alipo humu ndani ya stendi..
“..It’s too late Jerry..!! (Jerry umeshachelewa..!!)”
Niliongea kwa kujidai huku nikipanda dalaladala yakuelekea Mbagala na nisijue naenda kwa nani na wala itakuwaje huko nieandapo na huyu mtoto..






*** Unavyodhani Tina atakamatwa na Jerry..? Kwanini Tina kaamua hivyo kufanya..?


*** Nini hatma ya Tina kama akikamatwa na Jerry..?


** Hii ndio Play gal (Revenge) , Usithubutu hata kidogo uhadithiwe inayoendelea kwani play gal 56 itakayofuata ni nzuri zaidi ya hapa..



****Itaendelea…****

Labels: