Tuesday, August 21, 2012

DR KAFUMU (CCM) AVULIWA UBUNGE NA MAHAKAMA IGUNGA




MAHAKAMA KUU ya Kanda ya Tabora leo imemvua rasmi ubunge, Dk Peter Kafumu, aliyekuwa Mbunge wa Igunga kupitia Tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya mlalamikaji Joseph Kashindye aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Tiketi ya Chadema kufungua kesi dhidi ya Peter Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.
Katika shauri hilo, hoja 15  ziliwasilishwa na wakili wa upande wa mlalamikaji Profesa  Abdalla Safari ikiwamo anayodai kwamba Waziri wa Ujenzi  John Magufuli alifanya mkutano wa kampeni Kata ya Igulubi wilayani Igunga kutumia madaraka yake kuahidi ujenzi wa Daraja la Mbutu kama wananchi hao watampigia kura mgombea wa chama mapinduzi.

Pia Safari anadai waziri huyo aliwatisha wananchi wa kata hiyo kwamba wasipo ichagua CCM daraja hilo halitajengwa na kwamba pia aliwatisha wananchi hao kuwa wasipomchagua Dk Kafumu watashughulikiwa.
Profesa Safari alidai  Baraza la Waislamu (Bakwata) Wilaya ya Igunga liliwakataza waumini wasiipigie kura Chadema  na kwamba naye Rais mstaafu, Benjamini Mkapa alitoa ahadi ya kugawa mahindi kwa wananchi wa Igunga siku moja kabla uchaguzi ili waichague CCM.

Labels: ,

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home