Monday, August 20, 2012

HATUA SAHIHI YAKUFANYA PALE WAPENDANAO WANAPOTOFAUTIANA



Kamwe usifanye yafuatayo mnapokuwa katika mgogoro baina yako na mpenzi wako:
1. Kamwe msiitane majina yasiyorasmi wala msiyoyatumia kwa kawaida mfano; majina ya wanyama, vitu, majina ya kudharauliana na kushushiana hadhi.
2. Kamwe msitishiane na kupigana mikwara kama vile vitisho vya talaka, kudhuru, au kujidhuru.
3. Kamwe usiwaingize ndugu au wakwe kwenye mjadala usiowahusu au kuwachanganya ili kumuumiza moyo mwenzako.
4. Kamwe msitukanane, kukosoana au kukejili maumbile ya mwenzako.
5. Kamwe msitukanane, kukosoana au kukejeliana kuhusu uwezo wa akili au ufahamu wa mwenzako.
6. Kamwe usimtilie shaka mpenziwako katika yale anayoyawaza au kuyaandika wakati huna uhakika.
7. Kamwe kusiwepo na vurugu za kupigana baina yenu hata kama ni kwa vitisho tu.
8. Kamwe usimuingilie mwenzako wakati anazungumza kitu, msikilize, subiri amalize na wewe useme.
9. Kamwe usipayuke au kutumia sauti yako kubwa au kilio ili tu kutafuta ushindi.
10. Kamwe kusiwepo na viapo visivyo na msingi wala kutupiana laana za maneno.
Daima jitahidi kufanya yafuatayo mnapokuwa katika migogoro:
1. Fanya kila linalowezekana kufikia muafaka kabla ya kumaliza mjadala au tofauti zenu. Kamwe usiondoke, kusitisha au kutoroka katikati ya mjadala au ugomvi wenu wakati haujaisha.
2. Zungumza katika sauti ya kawaida pasipo kupayuka au kuhamaki.
3. Kuwa na mtazamo chanya, usiingie katika ugomvi ukiwa na mtazamo wa kuvunjika kwa uhusiano.
4. Tumia lugha inayokubaliwa pande zote mbili, matusi na kejeli havikubaliki.
5. Weka mipaka ya ugomvi au tofauti zenu, jifunzeni kuzimiliki tofauti zenu na kuzifanya ziwe zenu binafsi. Mara nyingi siyo hekima kila ugomvi wenu ujulikane na kila mtu kuanzia ndugu hadi wapitanjia. Epuka kuzozana mbele ya watoto.
6. Jaribu kuwa muelewa na jitahidi kutilia maanani katika kusikiliza kile ambacho mwenzako anataka kukiwakilisha.
7. Jaribu kukubali kukiri na kushuka badala ya kuwa mkwepa tuhuma ukitumia vijisababu vya kujilinda (defensive mechanisms)
8. Jitahidi na penda kufikia muafaka na siyo kutafuta kuwa mshindi katika tofauti mliyonayo.

Labels: ,

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home