MASTAA BONGO MOVIE WADAIWA KUJIUZA BBM
BAADHI
ya mastaa Bongo wanadaiwa kuwa na tabia ya kutumia mtandao wa simu wa BlackBerry
Messenger ‘BBM’ vibaya ikiwa ni pamoja na kujiuza kwa wanaume, Ijumaa
limebaini.
Utafiti
uliofanywa na mapaparazi wetu umeonesha kuwa, wapo ambao wawapo vyumbani kwao
hujipiga picha za utupu na kuzitupia kwenye mtandao huo kisha baada ya muda
huzitoa.
Wakizungumzia
tabia hiyo, baadhi ya wanaume wanaotumia BBM walikiri kukumbana na picha hizo za
ajabu za mastaa huku zikiambatana na maneno ya kujitongozesha kwao.
“Huyu
…(anataja jina la staa maarufu Bongo), juzi usiku mishale ya saa nane alianza
kunitumia ‘sms’ kuniuliza kama niko macho. Nilipomjibu akaniambia kuna zawadi
anataka kunipa, nilivyomkubalia akatupia picha yake akiwa kitandani
mtupu.
“Hazikupita
hata sekunde nyingi, kabla ‘sijai-download’ akaitoa kisha akaniuliza
nimejisikiaje kumuona alivyo. Nilishangaa lakini nikamjibu kwa kifupi kuwa ana
mvuto, basi kuanzia siku hiyo akawa ameniganda,” anasema kijana huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Sule ambaye ni mfanyabiashara jijini
Dar.
Msanii
mwingine wa kiume aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema:
“Mbona
huo ndiyo mchezo wao, yaani ukishamkubalia kuwa rafiki yao basi subiri vituko,
kwa kifupi sasa hivi wengi wanajiuza kupitia BBM.”
Katika
kupata ukweli juu ya habari hiyo, waandishi wetu walizungumza na baadhi ya
mastaa wa Kibongo wanaotumia mtandao huo ambapo walikuwa na haya ya
kusema:
JACQUELINE
PATRICK
Modo
huyo mwenye jina kubwa Bongo alifunguka: “Kwa upande wangu siwezi kukataa kuwa
sijawahi kuweka picha kama hizo, mimi ni mpenzi sana wa picha na ninaupenda sana
mwili wangu hivyo nikipiga picha ya aina yoyote lazima niitupie kwani ‘fansi’
wangu ndiyo wanaoweza kuniambia kama nimenenepa au nimekonda au
kunisifia
“Suala
la kutongoza wanaume naweza nikasema kuwa mimi siweki kwa sababu hiyo kwani
marafiki zangu wote kwenye BBM wana wapenzi wao.”
ZUWENA
MOHAMED ‘SHILOLE’
Mwigizaji
huyo ambaye pia ni mwanamuziki alisema: “Mimi sijawahi kumtongoza mwanaume na
siwezi kwa sababu mila za kwetu zinasema mwanaume ndiye anatakiwa kumtongoza
mwanamke hivyo mwanamke anayemtongoza mwanaume anakosea kwani ataonekana wa bei
rahisi sana.
Labda
wenzangu wanaweza kufanya hivyo kupitia njia hiyo.”
MIRIAM
JOLWA ‘JINI KABULA’
Mwigizaji
huyo alifunguka: “Mimi nina mume wangu, nampenda sana na mara nyingi siingii BBM
ila ninauzisha tu picha zangu kule lakini kuchati na watu siyo kivile na siwezi
kumtongoza mwanaume kwa sababu wanaume wanaopatikana kwa njia hiyo siyo kabisa
labda mastaa wenzangu, lakini mimi sijawahi kumtongoza mwanaume.”
RACHEL
HAULE ‘RECHO’
Staa
huyo wa filamu alisema: “Sijawahi kumtongoza mwanaume ila suala la kutongozwa na
wanaume kwenye BBM ni la kawaida, inategemea na msimamo wa mtu. Najua BBM
tumejiunga kwa ajili ya kujua matukio yanayotokea kwa haraka zaidi na siyo kwa
ajili ya kujiuza.”
ISABELA
MPANDA
Mwigizaji
huyo alitiririka: “Katika orodha ya hao wanaojiuza kupitia mtandano huo, mimi
simo. Nipo BBM ila sijawahi kumtongoza mtu wala kutupia za utupu.”
RUTH
SUKA ‘MAINDA’
Mwigizaji
huyo mkongwe alisema: “Ni kweli nimejiunga BBM lakini kwa sasa nipo ‘shouting’
nicheki baadaye.
Mastaa
wengine waliotajwa kuwepo BBM nja na waigizaji Aunt Ezekiel, Irene Uwoya, Agnes
Gerard ‘Masogange’ na wengineo.
Source: Global publishers
Labels: bongo movie, news updates
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home