TAFF YATOA TAMKO JUU YA MAHARAMIA WA FILAMU
SHIRIKISHO
la Filamu nchini(TAFF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)
pamoja Kampuni za usambazaji wa filamu na kazi za wasanii ‘wameapa’
kupambana na maharamia wote wa kazi hizo ili kulinda maslahi ya
wasanii. Wakizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana,
umoja huo kwa pamoja ulisema umefika wakati tatizo la wizi wa kazi za
wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo ni kero kwa
muda mrefu. Rais wa
Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia aliiomba
Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa kupambana
na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku wakijiamini
kwa kuendelea na kazi hiyo. “Umefika
wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka mbinu
kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa masikini
kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi zao”
“Tuna
imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri, tutaweza
kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii
kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu wachache
ndiyo wananufaika nayo” alisema Mwakifwamba. Naye
Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa inaweza kuwa na
nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato linalochangiwa
na sekta za madini maliasili pamoja na utalii. Alisema
Serikali
inapswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa wizi wa
kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa nchini walioamua
kujitoa mughanga kufanya kazi zao.
Kwa
upande wake Meneja usimamizi kutoka TRA Msafiri Ndimbo alisema Mamlaka
hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari Mwakani
hasa baada ya Serikali kupitia Bunge lake kukubaliana kuweka mikakati
ya kupamba na suala hilo.
Ambapo
wasanii na wasambazaji wa kazi zao wameungana pamoja
kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao zinakwenda kwa haki ili wasanii
na kazi zao
Labels: bongo movie, news updates
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home