AZAM WAMTIMUA KOCHA WAO..
Aliyekuwa kocha wa timu ya Azam Fc Stewart Hall |
Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa kuwa mkataba wake na
kocha Stewart John Hall kutoka nchini uingereza ulisitishwa rasmi jana Tarehe
31/07/2012 kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Klabu ya Azam FC inajivunia mafanikio ya kocha Stewart Hall,
na inampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya katika muda wote aliofanya kazi kama
kocha mkuu na mkurugenzi wa ufundi.
Chini ya Stewart Hall, Azam FC ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa
Mapinduzi Cup, Kushika nafasi ya pili katika ligi kuu, Mashindano ya Urafiki na
Kombe la kagame. Haya ni mafaniko ambayo hayajawahi kufikiwa na makocha wote
waliotangulia na ni mafaniko ya kihistoria katika klabu ya Azam FC.
Azam FC inamtakia kocha Stewart Hall kila la heri, na
inatarajia kuwa ipo siku katika siku za usoni kocha Stewart atarudi tena
kufanya kazi na Azam FC.
Stewart Hall anaacha changamoto kubwa sana kwa mrithi wake
ambaye atatangazwa hapo baadaye lakini kizuri ni kuwa, mrithi wa Stewart Hall
atakuwa ni mwalimu anayefuata mfumo ule ule wa uchezaji ulioachwa na Stewart
Hall kwani hiyo ndiyo (Playing Philosophy ya Azam FC)
Kwa sasa timu itakuwa chini ya Vivek Nagul na Kally Ongala
Imetolewa na Utawala
Azam FC
Labels: michezo
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home