ASPIRINI INAWEZA KUZUIA SARATANI.
ASPIRINI INAWEZA KUZUIA SARATANI
Vidonge vya Asprin |
Kumeza kidonge cha aspirini kila siku inaweza kuzuia na hata kutibu saratani. Taraifa hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya.
Matokeo
ya utafiti huo yalichapishwa na jarida la matibabu la The Lancet, na
hivyo kuzidisha kuonyesha manufaa ya aspirini katika matibabu ya
saratani.
Watu wengi tayari wanatumia Aspirini kama dawa ya maradhi ya moyo.
Lakini
wataalamu wanaonya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuelezea watu
kutumia aspirin ili kuzuia saratani na hata vifo vinavyotokana na
saratani.
Wataalamu hao wanaonya kuwa dawa hiyo inaweza kusababisha athari kubwa kama kuvuja damu tumboni.
Prof
Peter Rothwell,wa chuo kikuu cha Oxford akiwa na wakufunzi wengine
ambao wamefanya utafiti wa hivi karibuni, tayari walikuwa wamehusisha
aspirin na kuzuia aina ya saratani hasa saratani ya matumbo.
Lakini
utafiti wao wa awali, ulipendekeza kuwa watu wanahitaji kutumia dawa
hiyo kwa takriban miaka 10 ili iweze kufanya kazi hiyo.
Sasa
wataalamu wanaamini kuwa uwezo wa dawa hiyo kuzuia saratani, hutokea
mapema mno kati ya miaka mitatu na mitano. Hii ni kwa mujibu wa taarifa
mpya kutoka kwa majaribio 51 yaliyohusisha wagonjwa 77,000.
Na
asprini haionekani tu kuzuia tisho la kuugua aina nyingi ya saratani
bali pia lakini pia inazuia saratani kusambaa kwa sehemu zingine
mwilini.
Hata hivyo majaribio hayo hayakufananisha dawa ya aspirini na dawa zengine zinazoweza kuzuia maradhi ya moyo.
Lakini
wakati kikundi cha wataalamu, kilichoongozwa na Profesa Rothwel
kilidurusu wangapi kati ya watu waliohusika katika utafiti huo walipata
kuugua saratani na hata kufariki kutokana na ugonjwa huo, waligundua
kuwa vifo vilitokana pia na matumizi ya aspirin.
Kuzuia kusambaa kwa Saratani
Kwa
mtu anayetumia kiwango kidogo cha dawa hiyo kila siku, ilionekana
kupunguza idadi ya visa vya saratani kwa robo baada ya miaka mitatu
pekee.
Ni
watu tisa waliogungulika kuwa na saratani katika watu elfu moja kila
mwaka ikilinganishwa na watu kumi na mbili kwa watu elfu moja kwa wale
waliomeza tembe hizo.
Pia ilipunguza idadi ya vifo vilivyookana na saratani kwa asilimia kumi na tano.
source:BBC
Labels: mahusiano
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home