SASA NI ZAMU YA JB NA MAJUTO NDANI YA MUVI MPYA YANAKWENDA KWA MWANANGU..
King majuto aliyekaa akiwa na Jb huyu aliyesimama.. |
Sikuzote wapenzi wa filamu za bongo walikuwa wanahamu sana kuona Jb akiigiza na Majuto kwenye movi moja. Kwa kulithibitisha hilo bila kuwaacha wapenzi na dukuduku. Wasanii maarufu na wanaoongoza katika soko la filamu hapa bongo Jacob Stephen ama JB na yule nguli namba moja wakuchekesha hapa bongo AMRI ATHUMANI ama king majuto hivi karibuni wameibuka na movi moja kali inayokwenda kwa jina la NAKWENDA KWA MWANANGU. akizungumzia juu ya muvi hiyo, Jb alisema kuwa ameamua kubadilika nakutengeneza seriously comedy. Mbali na muvi hiyo pia Jb na Majuto wanatarajia kuelekea Mwanza kwa ajili ya uzinduzi huo tarehe 30 ya mwezi huu wa 7.
Labels: bongo movie, news updates
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home