Thursday, July 19, 2012

**** Play gal - 51 (revenge)






Ilipoishia….



Ni taa ya kwenye basi tu ndio ilikuwa imewashwa lakini upande wote wa nje kulikuwa na giza kali. Kila abiria aligeuka nakuniangalia kwa kunishangaa.
"..nipeni maji nasikia kiu.."
Niliropoka kwa sauti ya juu huku nikihema juu juu.
James alitoa maji ya chupa kwenye mfuko wa nailoni kisha akanipa na nilipomaliza kunywa nilipewa na machungwa nikala.
"..haya embu niambie jina lako binti.."
"..naitwa Christina.."
"..ok, Christina huku Mwanza ndio nyumbani ama..?"
"..si nilishakujibu toka mwanzo jamani..?'
"..ok, unakaa sehemu gani kwa huku Mwanza tunapoenda..?"
"..Nyamagana.."
Nilimjibu kwa kujiamini na baada ya hapo James akanisihi nikalale nyumbani kwake anapoishi na mke wake kwa kuwa gari itafika usiku sana hivyo kesho yake atanipeleka mpaka nyumbani kwetu Nyamagana..



Endelea….

“..Christina..??, Christinaaaaaaaaaa…??”
Nilishtuka kutoka usingizini huku nisielewe chochote. Kila mmoja alionekana kuwa busy kumsaidia kumbeba mwenzake. Usiku ulikuwa mnene sana kiasi kwamba ni tochi za simu tu ndio zilikuwa zikiangaza huku na kule kuhakikisha wanaona kinachoendelea mbele ya macho yao. Mikono miwili ilikuwa imeshikilia kichwa changu huku ikiniita kwa jina langu la Christina. Kila nikijitahidi kuvuta kumbukumbu bado ilikuwa ni vigumu. Vilio vya watu ndivyo vilizidi kuchanganya zaidi masikio yangu nakujiona kuwa sina tena bahati ya kuishi.
“..wee Christina..? mzima lakini..?”
“wewe nani..?”
Nilimuuliza kwa sauti ya ukali huku nikimkunjia uso vilivyo, jasho kali lilikuwa likitiririka kupitia usoni mpaka shingoni mwangu. Japo alikuwa ni mwanaume lakini alionekana kulia kama mwanamke tena yule ambaye ameshikwa na uchungu wa kujifungua watoto mapacha.
“.. embu amka, mimi mchungaji James..”
“..mchungaji James..? wa wapi..? unataka nini kwangu..?”
“Kwa uwezo wa mwenyezi mungu aliyetuumba nafarijika kukuona umekuwa mzima wa bukheri. Ulikuwa umepitiwa sana na usingizi huku ukiweweseka kwa mawazo njia nzima. Basi likaanza kuyumba huku likipoteza uelekeo. Abiria wote wakaanza kupiga makelele huku wengine wakimlaani dereva kwa kitendo cha kuendesha gari vibaya.  Nilijitahidi kusali sala zangu zote ili tu ninusuru ajali hii lakini kama unavyoona yaliyopangwa na mwenyezi mungu hakika kwa binadamu hawezi kutenganisha. Tumepata ajari kubwa sana na hii yote imesababishwa na lori lililokuwa limepaki vibaya..”
“lori..?”
Nilishusha pumzi nakurudiwa nakumbukumbu vizuri yakuwa nilikuwa naelekea Mwanza nyumbani kwetu. Nikayapindua macho yangu vizuri huku na kule kwa kutumia mwanga ule ule wa tochi za simu nakuona watu wakilia na wengine wakibebwa. Mwili wangu ulinisisimka ghafla sambamba na kichwa kuniuma huku mchozi ukinidondoka nakujiona laiti kama ningekuwa mimi ndio majeruhi ama maiti.
“..kweli mwenyezi  Mungu bado ananipenda nakujali..”
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikimuangalia mchungaji james mara mbili mbili.
“..ahsante mchungaji, umeokoa maisha yangu..!”
Aliniinuka pale chini nakuelekea nje kabisa ya basi, sijui alienda kufanyaje lakini baada ya muda mfupi alirudi mpaka eneo niliokuwa nimejilaza. Maiti nyingi zilikuwa zimepangwa huku nyingi zikiwa hazina viungo vya mwili. Kuna ambazo hazikuwa na shingo, mikono hata nyingine hazikuwa na miguu. Hakukuwa na msaada wowote kutoka hospitalini zaidi ya wale waliokuwa wazima kuwasaidia wale wenye unafuu kidogo na kuendelea kutoa maiti nakuzipanga kwa nje.
“..Kwani hapa mpaka Mwanza ni mbali..?”
Nilimuuliza mchungaji james huku nikimuegemea begani mwake kana kwamba mume wangu ama baba yangu na bila yakuogopa kama ni mtu wa mungu.
“wala hata siyo mbali sana kwani umbali wake ni sawa na kibamba mpaka kariakoo..”
“..twaweza kutembea..?”
“..wala tusiwe na haraka kiasi hicho. Kwanza tuhakikishe hawa ndugu zetu wanapata matibabu ya huduma ya kwanza. Pili lazima mawasiliano yafanyike na wote tuje kuchukuliwa na basi jingine wala usiwe na wasiwasi Christina..”
Maneno yale yaliniingia sana kichwani nakunitia nguvu nakumuona kuwa mchungaji James ni mtu mzuri, anayejali na kuheshimu watu na hata pia ni msamalia mwema. Aliniinua pale nilipokuwepo.
“..mizigo yako unakumbuka ulipokuwa umeiweka..?”
“..hapana, wala usihangaike kwani sikuwa na mzigo wowote..!”
Kwa muda mfupi tayari gari za polisi wakishirikiana na wanakijiji wa hili eneo walikuwa wakizunguka nakupakiza zile maiti zilizokuwa zimepangwa pembeni ya macho yangu. Sikuwahi kushuhudia maiti zikiwa nyingi kiasi kile zaidi yakuonaga kwenye televisheni tena kwenye taarifa ya habari ama filamu. Machozi yangu yalikuwa karibu sana nakujikuta nikiendelea kububujikwa na machozi huku nikiushikilia kikamilifu mkono wa mchungaji James nakuelekea kwenye basi dogo lililokuwa limekuja kuokoa majeruhi.
“…Hapana, sisi ni wazima tunamshukuru mwenyezi mungu tumenusulika, hivyo tupelekeni mpaka kituo cha mabasi  ‘Nyegezi’ hapo tutajua jinsi yakufika makwetu..”
Aliongea mchungaji James huku akimsisitizia dereva wa hii gari. Safari yakuelekea stendi kubwa ya mabasi ya Mwanza ‘Nyegezi’ ilianza huku akili yangu yote nikiituliza nakumuachia James kwani alishaniahidi kuwa atahakikisha amenipeleka mpaka nyumbani. Mwendo wa nusu saa ulitosha sana kutufikisha Nyegezi. Hali ya hewa ilikuwa imebadilika sana japo hakukuwa na joto sana wala baridi sana. Mchungaji James muda wote alikuwa amepitiwa na usingizi nadhani hakupata usingizi kabisa zaidi ya njia nzima kushikilia biblia yake nakulichambua neno  la Mungu.
“..James..?, mchungaji James..?? amka tumefika.!!.”
Nilimuamsha kwa kumtikisa lakini bado alionekana mzito kuamka. Baada ya kuendelea kumuamsha zaidi ndipo akaamka.
“..haya niambie tunaelekea wapi sasa..?”
“..naona kumekucha kabisa, sasa kwa hapa inatubidi tuchukuwe taksi mpaka nyumbani kwangu mtaa wa pili kule halafu tutajua sasa namna yaw ewe kukupeleka kwenu Nyamagana..”
Tulichukuwa taksi nakuelekea mpaka nyumbani kwake. Mchungaji James aliuwa na nyumba kubwa sana tena yenye uzio wa ukuta.
“..Mama yuko wapi..!”
“..Mama, mama hayupo..!!”
“..kaenda wapi..?”
“..kaenda kanisani..”
Mchungaji james alimuuliza mtoto wake baada tu yakupokelewa mizigo.  Uchovu niliokuwa nao ukichanganyia na usingizi ni kati ya vitu vilivyokuwa vimeuchosha sana mwili wangu. Tulipoingia tu sebuleni, mchungaji James aliongoza moja kwa moja mpaka chumbani kwake kisha akarudi akiwa kabadilisha nguo.
“..samahani Christina. Unaweza kwenda bafuni ukaoga mlango ule, mimi nitaogea chumbani kwangu. Na kwa kubadilisha nguo binti wa kazi huyo hapo atakuelekeza..”
“..sawa, wala usiwe na hofu nitaelekea tu  kuoga..”
Kwa namna alivyokuwa amekuja mchungaji James alinifanya mwili wangu wote ujisikie vibaya kwa kusisimka ovyo. Japo alivaa ‘singlendi’ lakini macho yangu yaliweza kuhakisi nakushuhudia nywele nyingi sana zikiwa zimemjaa kifuani mwake. Hata ile hamu yakuelekea bafuni nikaikosa nakutamani kwenda kuoga naye tena nimuogeshe mimi. Kila nikifikiria kuwa ni mlokole nabaki naumia nakuvunjika moyo.
“..lakini mie ndio Tina..!!, tena Tina aliyepinda toka zamani..”
Nilijikuta uzalendo unanishinda Tina mie nakutokwa na udenda  uliochanganyikwa na hamu ya kutaka kufanya mapenzi na mchungaji.  Nilikuwa bado nimezubaa pale sebuleni huku pembeni yangu akiwa mfanyakazi wa ndani akiangalia televisheni. Nikajisachi mifukoni mwangu nakutoa noti shilingi elfu moja kisha nikampa Yule mfanyakazi wa ndani.
“..nenda duka la madawa lolote kaninunulie sabuni ya detto, nashindwaga kutumia sabuni nyingine, sawa..?”
Yule binti wa watu aliinuka nakuondoka kwenda dukani haraka haraka.
“..wafanyakazi kama hawa ndio dawa yao..”
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikihakikisha Yule mtoto wa James aliyetupokea yupo nje. Nikauloki ule mlango wa sebuleni nakisha nikazivua nguo zangu nakubakiwa mtupu kama nilivyozaliwa, nikazishikilia mkononi nakuongoza mpaka chumbani kwa mchungaji james huku nikijitingisha makalio yangu…











*** Mchungaji  James kafanya usamaria mwema kwa Tina na sasa yanataka kumtokea puani. Je mchungaji James atamfanyaje Tina..?


*** kuhusu Tina kufika kwao atafanikiwa..? na nini hatma ya Tina..?

*** story bado kali na nzuri kupita kiasi huko mbeleni, sasa nipo nawewe karibu kuhakikisha unapata burudani ya kutosha..

** Majukumu ndio yalikuwa yamenibana kwani mbali nakuumwa nilikuwa safarini. Lakini kwa sasa niko huru kuendelea kutoa burudani. Nawapenda sana nakuwajali..



*** usikose Play gal 52 (Revenge)


******************itaendelea*****************

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home