JIFUNZE KUPIKA PANCAKE YA MBOGA MAJANI
MAHITAJI
480 gram unga wa ngano
120 gram maziwa ya maji
5 gram chumvi
50 gram sukari
2 mayai ya kuku
50 gram mafuta ya maji
1 kitunguu kikubwa katakata vipande vidogo
1 nyanya kubwa katakata vipande vidogo toa mbegu za ndani2 pili pili mbichi kata kata vipande vidogo (sio lazima)
majani ya gili gilani kwajili ya kupambia
JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO NA PICHA HAPO CHINI
Muda wa kuandaa : Dakika 15
Muda wa kupika : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 2
Idadi ya pancake : Kiasi cha 4 mpaka 6
Chukua
unga, sukari, chumvi, maziwa, na mafuta ya maji pamoja na mayai
changanya kwa pamoja kwa kutumia mchapo kisha weka pembeni unga wako,
Kisha katakata pilipili, nyanya na kitunguu kama uonavyo katika picha.
Chukua
kikaango kisha weka mafuta kiasi na sambaza vizuri kisha pata moto
mimina kati kati ya kikaango unga wako na usambaze uenee kwenye kikaango
chote.
Hakikisha
unga ni wakutosha katika kikaango ili pancake yako iweze kua nene na
mboga majani ziweze kutosha iache iive kwa dakika 3 kwa moto wa wastani,
Ikishaanza tu kutoa kama mapovu kwa juu kuonyesha dalili ya kua itakua
imeiva chini na inaendelea kuchemka kwa juu basi tupia vipande vya
nyanya, korienda na kitunguu kisha geuza chini kuwe juu.
Baada
ya kuigeuza utaona rangi ya kahawia upande ule uliokua chini inamaa
imeshaiva upande wa kwanza pia upande wa pili ambao unamboga pika kwa
dakika 3 na kisha toa itakua imeiva pia unaweza mwagia mafuta kiasi kw
apembeni ili yaingie chini ya pancake yako na isiweze kuungua na kushika
katika kikaango.
Baada ya dakika 3 itoe itakua imeiva na itakua na harufu safi sana ya kuvutia hakikisha unamapatia mlaji ikiwa yamoto.
Pancake hii unaweza kunywa na chai asubuhi au jioni saa 10 kama kitafunwa tu cha kawaida. Pia unaweza kula kama mlo kamili kwa mchana au usiku pamoja na chuzi wa nyama samaki au hata maharage ya nazi na familia ikafurahia sana sana.
Labels: ~ Mapishi ~
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home