Thursday, July 26, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA MUFFIN YA MATUNDA NA NAFAKA KWA LADHA SAFI KABISA

HAPA CHINI NI MUFFIN YA MATUNDA NA NAFAKA


MAHITAJI

360 gram unga wa ngano

120 gram zabibu kavu
1 kijiko kikubwa cha chakula  Baking Powder
5 gram chumvi
1/2 kijiko cha chai unga wa Cinnamon
3 apple au Pears chop chop vipande vidogo 
60 gram chop chop korosho au walnuts
180 gram ya maziwa ya maji
1 kijiko kidogo cha chai vanila essence
2 kijiko kikubwa cha chakula olive au corn Oil
sukari nyeue ya unga kwajili ya kupambia

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : dakika 30

Muda wa mapishi : dakika 30
 Idadi ya walaji : 4
Idadi ya chakula : 12 muffins


 
Kaanga korosho au walnuts mpaka zinukie kwa dakika 6 hadi 8. Pia unaweza tumia Oven kwa moto wa 350F kwa dakika 5 hadi 6.



Chukua gram 120 za korosho na weka katika blenda kisha ongeza kijikokikubwa cha chakula 4 maji safi baridi na kisha saga na weka pembeni.

 

Katika bakuli safi na kavu weka unga wa ngano, sukari, baking powder, chumvi na cinnamon kisha changanya.



KIsha ongeza zabibu kavu, vipande vya apple au pears pamoja na korosho zote zilizobakia na uendelee kuchanganya mchanganyiko wako uchanganyike vizuri .



Kisha katika bakuli nyingine changanya vanila essence, zile korosho ulizosaga pamoja na maziwa ichanganyike vizuri pamoja na olive oil.




Chukua ule mchanganyiko wenye maziwa na korosho kisha umwagie ndani ya ule mchanganyiko wa unga na uendelee kuchanganya vizuri.

 

Hakikisha unachanganya pole pole mpaka mchanganyiko wako unachanganyika vizuri ( mchanganyiko huu utakua unanasa nasa). usichanganye muda mrefu utaharibu.

 

.Washa oven yako kwa moto wa 400F.Kisha weka karatasi kama zionekanzo kwenye picha ni maalumu kwajili ya kuokea muffin ziwe 12 kisha tumia cooking spray. Kwa kutumia Spray itafanya urahisi wa kutoa wakati ikishaiva kama huna spray basi tumia mafuta ya siagi.




Hakikisha unagawa sawa kwa sawa ili ziweze kutosha vikombe 12 vya muffin.



Nyunyizia kwa juu sukari yakutosha unaweza tumia ya unga au ya kawaida pia inaweza kua nyeupe au ya kahawia ni pendekezo lako tu.



Choma katika oven kwa dakika 20, Au mpaka ukichoma kwa kijiti kati kati kinatoka kisafi bila unga mbichi.



Toa katika pan ya kuokea , kisha zipoze katika wire rack. Maffin yako itakua kavu (crusty)  na crunch nyingi toka kwa korosho kila unapotafuna. Na mapears au apple yanaweka unyevu ndani kwakua ni malaini. Ile korosho ya kusagwa inafanya muffins yako iweze kutafunika kilaini. Hakikisha unampatia mlaji zikiwa zamoto kwani ndio zinapendeza sana kwa ladha pia unaweza kula wakati wa chai ya saa10 jioni au chai ya asubuhi.



Unaweza tengeneza mchanganyiko huu kisha ukahifadhi katika friji kwa matumizi ya kesho asubuhi endapo umeandaa usiku au ukahifadhi kwenye friza kwa matumizi ya mwezi au wiki na ukapata ubora ule ule.



WAANDALIE FAMILIA YAKO KWA KITAFUNWA CHA ASUBUHI ILI WAANZE SIKU KWA FURAHAA.

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home