Monday, August 13, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI YA EMBE BICHI

JIFUNZE KUTENGENEZA KINYWAJI HIKI SAFI SANA CHENYE VIUNGO KWA KUTUMIA EMBE BICHI LA KUCHOMA


MAHITAJI


350 grams Embe la kijani, lioshe vizuri
5 pc ice cubes , Mapande ya barafu
1 lita maji safi baridi
 2 kijiko kidogo cha chai Cumin Powder
2 kijiko kidogo cha chai chumvi
1/4 kijiko kidogo cha chai pili pili manga
2 kijiko kidogo cha chai Sukari
majani fresh ya Mint kwa kupambia 

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : Dakika 15

Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 2

Kuna njia 3 za kuandaa juisi hiib ya embe.


 1. Chemsha embe kisha liache lipoe na utoe ngozi ya juu. KIsha toa nyama yote na saga katika mashine kuanzai hapo unafata maelezo kama picha zinavyoonyesha kuanzia step ya saba.

 2. Chukua embe kisha lioshe na umenye katakata na weka katika preasure cooker kwa dakika kumi .Kisha cha lipoe na endelea na maelezo kama picha inavyoonyesha Step ya 7.

Asili ya juisi hii ni kutoka india na kinamama walikua wanachoma maembe kwa mkaa wakiamini hii ndio njia pekee ya kufanya juisi iwe tamu zaidi, Kwasasa technologia imekua unaweza rost embe lako kwa kutumia Oven au gas burner kama inavyoonekana katika picha. Hii ndio njia ya tatu ambayo ninaionyesha leo na juisi inakua na ladha safi sana ya moshi chukua embe lako na weka juu ya gas burner


 
Hakikisha unachoma pande zote mpaka ngozi inakua nyeusi

Kisha weka pembeni lipoe.

Kisha menya ile ngozi yote ya juu.

Kisha toa nyama yote bakisha kokwa tu na nyama weka katika blenda.

Saga iwe laini kabisa.

Kisha chukua ice cubes na weka katika kikombe kikubwa

Kisha chukua lile rojo la embe ulilosaga na weka kwenye vipande vya barafu.

Kisha weka cumin powder, pili pili manga, majani ya minti kidogo na sukari hakikisha unaweka kidogo kidogo mpaka upate ladha halisi unayoipenda wewe.
Kisha ongezea kiasi cha maji na na ukoroge angalia kiasi ya uzito unachopendelea wewe.

Kisha pambia na majani ya mint kwa juu kuongeza harufu nzuri na pia katika juisi yako weka vipande vya barafu zaidi wakati unamapatia mnywaji ili kinywaji hiki kiendelee kua baridi .

Kinywaji hiki anaweza kunywa mtu yeyote yule na kinaongeza sana hamu ya kula hasa kama mtu yeyote yule anaumwa au amepoteza hamu ya kula. Waaandalia familia yako wafurahie. 

Labels:

Tuesday, August 7, 2012

UNAJUA JINSI YA KUTENGENEZA BURGER


WATOTO WENGI SANA WANAPENDA KULA BURGER HATA WATUWAZIMA PIA HUPENDA KULA SIKU MOJA KATIKA CHAKULA CHA MCHANA WATENGENEZEE
FAMILIA WAFURAHI

Kwaujumla napenda sana burger ya kutengeneza nyumbani, na ninapenda kutengeneza mwenyewe au mke wangu lengo ni kuhakikisha viungo na mchanganyikowote unakua sawa. Kwakutmia recipe hii unaweza kutengeneza 8 -10 hamburgers Inategemea utaweka upana gani wa nyama yako.Baada ya kuandaa unaweza kuhifadhi mchanganyiko huo wa nyama kwenye freezer kwa matumizi ya baadae.
MAHITAJI

 1 kg nyama ya kusaga safi 
 240 gram kitunguu kilichokatwa katwa vipande vidogo 
 60 gram bread crumbs ( Unga wa mikate)
 1 kijiko cha chakula Worcestershire sauce
 2 cloves of garlic, peeled and minced
50 gram kitunguu swaumu
 5 gram chumvi
 5 gram pili pili manga
1 lettuce
1 kitunguu
2 nyanya fresh

Katika bakuli kubwa changanya nyama pamoja na kitunguu, bread crumbs, Worcestershire sauce na kitunguu swaumu kisha weka . Kisha changanya safi na gawa katika mafungu 8 au 10 kulingana na ukubwa unaopenda wewe.
JINSI YA KUPIKA

Unaweza ukakaanga kwenye kikaango au ukapika kwa moto wa 160 degrees katika oven. Chukua mkate wa burger kisha kata katika pande mbili kisha paka mayonnaise na tonato  ketchup kwenye mkate upande wa chini, ongezea lettuce, slice kitunguu na nyanya fresh na slice ya tango la kopo. Nyunyizia chumvi kidogo mpatie mlaji ikiwa yamoto


Labels:

JINSI YA KUPIKA BIRIYANI KWA KUTUMIA WALI WA BASMATI NA NYAMA YA KUKU, MBUZI AU NG'OMBE

                                                       MAHITAJI


1 kilo mchele wa basmati mrefu

1 kilo nyama iwe ya kuku au ng'ombe au mbuzi kata katika umbo dogo la kutosha kula kisha ichemshe na tangawizi na kitunguu swaumu, unga wa binzari (turmeric powder) pili pili manga na chumvi ili kuweka ladha nzuri. Ikisha iva itoe iweke pembeni na mchuzi wake uweke pembeni utautumia baadae.
1 kilo ya vitunguu kata slice ( mviringo)
1 kilo nyanya nyekudu zilizoiva, osha vizuri kisha katakata saizi ndogo ndogo sana
240 gram ya Mafuta ya kupikia
240 gram ya samli au mafuta yeyote ya kupikia
2 maggi chicken soup cubes
3 kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili mwekundu
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa binzari (turmeric powder)
3 kijiko kidogo cha chai unga wa girigilani (coriander powder)
2 kijiko kikubwa cha chakula mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu swaumu vilivyosagwa (ginger-garlic paste )
50 gram korosho iliyo kaangwa usizisage zibaki nzima
50 gram majani ya girigilani (fresh coriander leaves, washed and chopped)
8-12 mbegu za nzima ya hiriki (green cardamoms)
4 bay leaves ( sifahamu kiswahili chake)
15 mbegu nzima ya pili pili manga (whole black peppercorns)
30 gram majani mabichi ya minti ( mint leaves )
salt kulingana na ladha yako binafsi
Jinsi ya kuanda

Weka mafuta katika sufuria yako iliyo juu ya moto tayari, kisha kaanga nyama yako iliyokwisha chemshwa mpaka iwe na rangi ya kahawia (golden brown)

Kisha itoe nyama hiyo na ichuje mafuta ili mafuta yanayobaki weka kitunguu na endelea kukaanga kwa dakika 7-10 kisha weka unga wa binzali, unga wa pili pili mwekundu, unga wa girigilani, bay leaves, mbegu za hiriki na nusu ya mbegu za pili pili manga.
Changanya vizuri mpaka utapata mchanganyiko mzuri mkavu miminia humo maji uliyotunza baada ya kuchemshia ile nyama yako na kuiweka pembeni ipoe. kisha weka nyanya fresh ndani ya sufuria yako pika mpaka maji yakauke na mafuta yaanze kuoneka kwa juu ndani ya sufuria.
Kisha weka nyama yako ndani ya sufuria pole pole halafu punguza moto acha ijipike kwa muda mpaka mchuzi wako na nyama vikamate ladha pia usisahau kuweka chumvi kulingana na ladha unayopenda.
Chukua sufuria nyingine weka mafuta ya samli na vitunguu ilivyoslice kisha kaanga na majani ya girigilani, majani ya mint na korosho funika kwa dakika 10 picha inaonyesha hapo chini, kisha weka wali wako mkavu uliokwisha oshwa vizuri na uchanganye vizuri ongeza vikombe 5 vya maji na chumvi kidogo mchele ukishaanza kuchemka funika sufuria lako na punguza moto maji yakisha kauka kiasi weka mchanganyiko wa ile nyama yako nusu tu juu ya wali wa basmati acha wali uive kabisa kisha itakua tayari kula na pakua chakula chako kikiwa cha moto,


Wali wa pishori ( Basmati rice) uliokwisha iva


muonekano wa majani ya girigirani wakati wa kukaangwa


 Wali wa pishori ( Basmati rice) uliokwisha iva ukakaangwa na vitungu na korosho


Nyama ya kuku iliokaangwa vizuri na viungo na nyanya ukapata mchanganyiko mzuri mzito




Muonekano halisi wa biriyani yako baada ya kuiva ikiwa imechanganyikana na nyama pia kumbuka kunamchuzi mzito na nyma ilibaki pembeni mlaji ataweza kujongezea kiasi apendacho.
Furahia chakula hiki pamoja na familia yako.

Labels:

TENGENEZA KEKI YA TUNDA TUFAA ( APPLE)

HII NI KEKI NZURI YA TUFAA AU APPLE SAFI KULA BAADA YA CHAKULA AU UNAWEZA KULA NA CHAI YA SAA 10 JIONI


MAHITAJI

170 gram siagi
170 gram sukari
1/2 kijiko kidogo cha chai kwaruza ganda la limao
4 mayai mabichi sawa na (210 gram)
275 gram unga wa ngano
1 kijiko kikubwa cha chakula baking powder
100 gram maziwa ya maji au cream
ca. 20 lavender leaves
3 au 4 apple kata vipande vidogo vidogo
3 kijiko kikubwa cha chakula
60gram majani ya mchai chai (lemon grass)

JINSI YA KUANDAA

Changanya sukari na siagi kwa uwiano wa uzito sawa ile ya gram 170 mpaka ichanganyike vizuri.

Kisha weka chenga za limao ulizokwaruza pamoja na mayai endelea kuchanganya

Kisha weka unga wa ngano na baking powder enedela kuchanganya kiasi

kisha ongeza maziwa na mchai chai ulikatwa vipande vidogo vidogo

kisha mimina mchanganyiko wako kwenye chombo unachotumia kuokea

kisha chomeka katika mchanganyiko wako vipande vya apple safi vienee

mwisho chukua vile vijiko vitatu vya sukari juu ya mchanganyiko wako

choma katika oven kwa moto wa nyuzi joto 175°C kwa dakika 45 mpaka 55 mpaka iwe rangi ya kahawia safi kisha itoe ipoe tayari kwa kuliwa.



Huu ni muonekano wa mmea wa mchai chai na majani yake


Huu ni muonekano wa shina la mchai chai na ndio inahitajika kwajili ya keki yako kata vipande vidogo vidogo sana kisha tumia katika mchanganyiko wako wa keki kwa harufu na ladha safi

Huu ni muonekano wa rangi nzuri ya juu safi wa keki yako baada ya kuiva



Huu ni muonekano safi kabisa baada ya kuikata keki yako unaona vipande vidogo vidogo vya mchai chai na tunda tufaa au apple. Unaweza kula ikiwa ya moto au ikiwa imepoa yote sawa pia unaweza kuhifadhi katika friji kwa muda wa wiki moja tu.


Labels:

Sunday, August 5, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA PIZZA KAUKAU YENYE CHIIZI JUU NA PEMBENI


PIZA HII NI TAMU SANA NA NIRAHISI KUTENGENEZA KAA TAYARI KWA RECIPE

MAHITAJI

KWAJILI YA UNGA WA KUKANDIA
    Utaweza tengeneza 6 pizza  ( 23-30 upana wa cm ) 
1 kilo ya unga wa ngano 
1 kijiko kikubwa cha chakula chumvi
1 kijiko kidogo cha chai amira ya chenga
60 gram Olive oil au vegetable oil
420 gram maji baridi sana (40° F/4.5° C)
1 kijiko kikubwa cha chakula sukari


KWAJILI YA KUWEKA JUU YA PIZZA

600 gram sauce iliyopikwa kwa nyanya
1 kilo Mozarella cheese ( nusu kata slice na nusu kata umbo la mstatiri kama katika picha)
200 gram slice za nyanya fresh iliyoiva
1 fungu la majani ya basil


JINSI YA KUANDAA FATA MAELEKEZO NA PICHA HAPO CHINI



Katika bakuli weka unga wa ngano, humvi pamoja na amira au kama unatumia mashine basi weka katika mashine.



Kisha weka mafuta ya olive, sukari na maji baridi kisha kanda vizuri. kama unatumia mashine weka speed ndogo. 
 

Kanda kwa kutumia nguvu kiasi baada ya maji kushi unga vizuri ili upate mchanganyiko safi.




Kisha toa mchanganyiko huo wa unga na uweke juu ya meza kanda kwa dakika 5 mpaka 7, mpaka uhakikishe mchanganyiko wako umekua laini kabisa. kama bado limekua tepe tepe, ongeza unga kiasi na uendelee kukanda au kama kavu sana ongeza kijiko 1 au 2 vya maji baridi.



Kama unatumia kukandia mashine kama kwa muda huo huo nilioelekeza ila kwa speed ndogo. Mwaga unga juu ya mea unayokandia. Kisha kata unga wako katika vipande sawa 6 vyenye uzito sawa.  Mi nimekata katika vipande 4 kwakua nilikua nataka pizza kubwa.



Mwagia unga kiasi juu ya mchanganyiko wakow a unga. Hakikisha mikono yano ni mikavu kisha ipake pia unga. Kisha chukua vipande hivyo vya unga na viringisha katika maumbo ya duara.



 Kisha chukua hayo maumbo ya duara na weka katika sinia ulilolipaka mafuta weka na paka mafuta juu ya hiyo miviringi pia.



Kisha chukua plastic foil na funika kwa juu.  Kisha weka mchanganyiko wakow a unga katika friji acha ulale usiku kucha pia kama unataka kula pole pole unaweza hifadhi kwa siku 15 mpaka 30 katika freezer sio friji. kisha ukawa unapika pizza moja moja kila siku na kama umeziweka katika freezer kumbuka siku moja kabla ya kuipika pizza yako toa katika freezer na weka katika friji ili iyeyuke. Kama unataka kupika siku hiyo hiyo basi acha katika friji kwa masaa 3 mapka 4 kisha toa.




Siku ya 2 - siku uliyopanga sasa kula pizza, masaa 2 kabla ya kupika viza yako, Toa idadi ya miviringo ya pizza unazotaka kupika wewe. Kwanza unamwagia unga kisaha unapaka mafuta kiasi kisha weka juu ya meza kwajili ya kukanda tena. Kanda kwa dakika 2 kisha funika na plastic wrap Acha kwa masaa 2 nje.



Kisha chukua maumbo hayo ya mviringo na anza kusukuma upate umbo bapa maalumu kwajili ya pizza.



Kwakutumia rolling pin ( ubao wa kusukumia) zungusha pizza yako katika mpini na uibebe



Kisha weka katika pizza pan ambayo imemwagiwa unga na imemwagiw amafuta kiasi (Hii inasaidia pizza isigandie tyra ya kuchomea)
 


Kisha kwa kutumia mikono yako vuta mpaka ifike mwisho wa sahani



Hakikishs baada ya kuivuta mwisho wa sahani iwe na muonekano kama wa kwenye picha



Hakikisha unaweka chizi iliyo na umbo la mstatiri na uache nafasi kama ionekanavyo katika picha. .



Kisha kusanya mchanganyiko wako tokea nje na unaingiza ndani kwa kufunika cheese yote na ukandamize ili ishike. Hakikisha unakandamiza vizuri. Weka mtindo wa curl kama nilivyofanya mimi, Fanya hivyo kuzunguka pizza yote.



Chumua mchuzi wa nyanya ( tomato sauce) kisha pakaza pizza yako yote kwa juu.


 
Rushi majani ya basil juu ya sauce ya nyanya. Kisha weka slice za nyanya fresh, ziwe nyembamba. Kisha weka slice za fresh mozzarella cheese juu kabisa iwe mwisho.



Choma katika oven iliyokwisha washwa na inamoto wa 450-500F. Choma kwa dakika 15 mpaka 20 inategemea na uwezo wa oven yako. Kwa moto makali sana inaweza chukua hata dakika 10 tu. Hakikisha ikiwa katika oven unaichungulia.



Ikishaiva toa na rushia tena majani ya basil kwa juu. Joto kali toka katikapiza litaunguza majani hayo na kutoa harufu safi sana.
 


Kata katika vipande vidogo inakua rahisi kwa mlaji.



Hakikisha unampatia mlaji ikiwa yamoto. Unaweza rushia kwajuu Parmesan cheese ana pili pili manga kama unapendelea.




HUU NDIO MUONEKANO WA PIZZA YETU SAFI SANA UNAWEZA KUIONGEZEA LADHA KWA KUWEKA CHOCHOTE KILE UKIPENDACHO KAMA NYAMA AINA ZOTE NA UKAFURAHIA NA FAMILIA YAKO.

Labels:

JIFUNZE KUPIKA PILAU SAFI NA RAHISI..


RECIPE SAFI KABISAYA PILAU KWA MSIMU HUU WA SIKU KUU ZA KUFUNGA MWAKA. UNAWEZA PIKA KWA KUTUMIA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI TU AU UKAPIKA KWA AINA YEYOTE YA NYAMA KWA KUTUMIA MTINDO HUU HUU NA IKAPENDEZA SANA SANA.

MAHITAJI

  240 gram za mchele wa basmati au mchele wowote mrefu, Loweka katika maji kwa dakika 20
  1 kijiko kidogo cha chai mbegu za binzali nyembamba ( cumin seed)
   1 kitunguu kikubwa kata kata
  1 Nyanya kubwa kata kata
   3  spring onions ( majani ya kitunguu) 

  1 bay leaf
   3 cloves ( Mbegu za Karafuu )

3 cardamom ( mbegu za hiriki)
  1/2 kijiko cha chai kidogo turmeric powder ( Unga wa manjano)
   5 gram kitunguu swaumu
  1 pili pili mbuzi kata kata
    5 gram unga wa tangawizi au ya kusagwa
    1 kijiko kidogo cha chai garam masala
   600 gram coconut milk (Tui la nazi) sio lazima kama hutumii nazi basi weka maji kawaida
   5 gram chumvi
    1 fungu la giligilani kwajili ya kupambia
  1 jikiko kidogocha chai maji ya limao (sio lazima)




JINSI YA KUANDAA FATILIA HAPO CHINI



  Katika sufuria weka kijiko 1 kikubwa cha chakula mafuta kisha kaanga mbegu za binzali nyembemba, bay leaf, karafuu, mbegu za hiriki, kitunguu swaumu, pili pili mbuzi, tangawizi na chumvi.




 Kitunguu kikashalainika weka nyanya pamoja na unga wa manjano na  garam masala. Kaanga kwa dakika 2.




Pilau hii nimepika sio ya nyama, kwa wale wapenzi wa nyama wakati umeweka vitungu na vile viungo vyote weka pamoja na nyama kaanag vyote kwa pamoja kwa dakika 10 kisha ndio uweke nyanya na viungo vingine vinavyofatia.


Nyama yako ili iwe laini chukua papai lililoiva baada ya kukatakata nyama pondea papai katika bakuli lenye nyama kisha weka chumvi kidogo, soya sauce kidogo, kitunguu swaumu na tangawizi kwa ladha zaidi. Nyama hii iweke kwenye friji kwa dakika 45 tu iwe ndani katika mchanganyiko huu itakua laini sana na utaipika kwa muda mfupi sana na familia watafurahia.




   Kisha ongeza mchele hakikisha unauweka bila maji. Hakikisha una ugeuza geuza mpaka mchele ubadilike rangi na kutoa harufu safi baada ya kuukaanga.





 Kisha ongeza tui la nzai au maji kwa wale wasio tumia nazi endelea kukoroga ichanganyik vizuri.





 Funika na mfuniko kisha pika kwa dakika 10 au mpaka mchele wako utakapo iva na kua wali.






Kisha ugeuze wa chini uje juu na wajuu uende chini. Binafsi huwa napenda kuongezea njegere zilizochemshwa nikahifadhi katika friji mwisho kabisa pilau hii ikishaiva. 
 
 

Kwa kuipendezesha pilau yako sasa mwagia kwa juu majani ya kitungu na majani ya giligilani.  Kisha huwa na mwagia kwa juu maji ya limao kwa sababu kuu mbili. Moja ni kuongeza ladha. Pili inasaidia kupunguza kiwango cha sodium.


Hakikisha unampitia mlaji chakula kikiwa chamoto. Kwa wale wapenda samli unaweza weka kijiko kimoja pia itaongeza harufu na ladha safi katika pilau yako.




HUU NI MUONEKANO SAFI BAADA YA PILAU YETU KUIVA FURAHIA NA FAMILIA YAKO KWA MAPISHI SAAFI NA RAHISI KUANDAA KUMBUKA LIMAO AU PILI PILI SI LAZIMA KUWEKA NI PENDEKEZO LAKO TU HASA KAMA UNAMATATIZO USIWEKE TUMIA VIUNGO VINGINE NA BADO PILAU YAKO ITAPENDEZA SANA.

Labels: