JIFUNZE KUTENGENEZA BAJIA HII YA MBOGA AINA YA CAULIMAUA
JIFUNZE KUPIKA KITAFUNWA HIKI SAFI KABISA NI RAHISI KINAVUTIA
MAHITAJI
250 gms Cauliflower, kata vipande
120 gram unga wa dengu (chickpea flour)
60 gram unga wa mchele
2 kijiko kikubwa cha chakula unga wa ngano
5 gram chumvi
5 gram unga wa pili pili (Chilli powder)
JINSI YA KUANDAA FUATILIA PICHA NA MAFUNZO
Muda wa maandalizi : Dakika 15
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 4
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 4
Pasha mafuta kwajili ya
kukaangia. Huo ni muonekano safi kabisa wa colimaua za rangi tofauti
ingawa nyumbani Tanzania ni adimu sana kupatikana kwa mchanganyiko huo
wa rangi ya zambarau, orange na kijani ila kwa rangi nyeupe ni maarufu
sana na zinapatikana kila sehemu.
Kisha kata kata coulimaua zote na kisha ziweke pembeni zikauke.
Chukua unga aina zote pamoja na chumvi na pili pili ya unga kisha changanya ichanganyike.
Kisha ongeza kijiko kidogo cha mafuta yamoto pamoja na maji ya uvugu vugu.
Hakikisha unachanganya ili kupata mchanganyiko mzito kama uonekanavyo katika picha.
Ukijaribu kumimina unapata mmiminiko mzito kabisa.
Kisha chukua kipande cha cauliflower chovya kwenye mchangantiko wa unga.
Hakikisha unachovya vizuri ili uweze kuenea sehemu zote.
. Unaweza weka vipande vingi kwa wakati mmoja ili kuokoa muda pia inategemea na ukubwa wa kikaango chako.
Kwa kikaango changu huwa natumia vipande vitatu hadi vinne kukaanga kwa wakati mmoja.
Kaanga kwenye moto wa wastani kwa dakika 2 au 3 mpaka iwe na rangi ya golden au reddish brown.
Ukizikaanga
kwa moto unaotakiwa basi hazita meza mafuta ila kwauhakika zaidi weka
karatasi katika bakuli au sinia kisha ukizitoa katika mafuta ziweke ili
zijichuje mafuta.
Unaweza kula na tomato sauce au ketchup au hata chutney ya ladha yeyote na ukafurahia
Inavutia
sana na itasaiaidia kuhamasisha ulaji wa mboga. Pia
unaweza ukawashawishi watoto nyumbani kupenda kula mboga majani kwakua
umeweza kutengeneza chakula chenye rangi mchanganyiko pia mkaanza mchezo
wa kubahatisha nani kapata rangi gani na usishangae hata watu wazima
wakajiunga kubahatisha nani kapata rangi ipi. hahahaaaaaaaa!
AINA
HII YA MAPISHI UNAWEZA FANYA KWA VIPANDE VYA SAMAHI, NYAMA YA NG'OMBE
HATA NYAMA YA KUKU PAMOJA NA DAGAA. NA FAMILAI IKAFURAHIA SANA SANA
Labels: ~ Mapishi ~
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home