*** Play gal - 54 ( Revenge)
Ilipoishia…
Nikiwa bado katika hali ya kuongea na dereva teksi na hata
sikuwa nimepanda ile gari wala kupatana naye bei rasmi. Mara kwa ghafla
akatokea mwanamama mnene mrefu kidogo. Alikuwa mweusi huku sura yake
ikikunjamana vilivyo mithili ya mtu anapopigwa jua la utosi. Macho yake
yalionesha kuwa tata kwani mbali na machozi yaliokuwa yakimtoka pia yalikuwa ni
mekundu kama mtu aliyefiwa ama kumpoteza mume au mtoto wa kumzaa.
“..unakwenda wapi Malaya mkubwa wewe..?”
Aliuliza kwa sauti ya jazba. Sikuwa namtambua zaidi
yakumtolea macho mimi pamoja na dereva teksi. Mwili wangu ulikuwa tayari
umeshakata tamaa ya kuishi huku nikihisi kama kojo likiteleza ndani ya suruali
yangu iliyokuwa imenibana…
Sasa endelea….
Uoga uliochanganyikana na kutetemeka mwili mzima ni kati ya
vitu ambavyo vilikuwa bado vinasumbua halmashauri ya kichwa changu huku
nikibaki njia panda nikiendelea kumkodolea macho yule Mmama alioonesha
kunikazia macho vilivyo huku akiendelea kutoa matusi makubwa na mazito.
“...na leo ndio utanitambua vizuri..? yaani siku ya nne leo
huonekani cha nyumbani wala hujui hata watoto wanaishije huko..? Wewe kazi
kuendesha hiki ki teksii chako tena bila hata haya unaongea tu na wanawake
shenzii kabisa wewe mwanaume..!”
Nilishusha pumzi huku nikinyanyua mkono wangu wa kulia
nakushika kifua changu huku nikijihisi mapigo yangu ya moyo yalivyokuwa
yakiendelea kunitoka. Nikatoa kitambaa nakuanza kujifuta futa jasho lilikokuwa
limeshaanza kupenyeza kwenye uso wangu nakupitilizia shingoni. Kumbe yule
dererva teksi niliokuwa naye ndio alikuwa akiongeleshwa na mke wake sijui. Aibu
kubwa ikanijaa ghafla Tina mimi nakufikiri kuwa kumbe ningeumbuka kama ndio
angekuwa mke wa mchungaji James.
“..Naona hapa tena hamna safari..?, embu ngoja nitafute
usafiri mwingine…”
Niliondoka zangu nakuwaacha pale yule dereva teksi na mke
wake wakiendelea kugombana. Nikatafuta teksi nyingine ambapo ilinifikisha mpaka
stendi kubwa ya mabasi. Umati wa watu ulikuwa umefurika ndani ya stendi hii ya
mabasi huku kila mmoja akiwa yuko ‘bize’ si kwa kubeba mizigo yake bali kwa
purukushani za hapa na pale za kugombea tiketi. Nilijisogeza mpaka eneo la
karibu na basi la ‘Mohammedi trans’ ambayo ni mabasi maarufu sana kwa safari
ziiendazo dar es salaam.
“.. Nauli ya hapa mpaka dar shilingi ngapi..?”
“..nauli yake shilingi elfu thelathini na nane tu..”
Nilichomoa hela kwenye suruali tena hela zenyewe zile
nilizokuwa nimeziiba baada ya kufanya mauaji ya mchungaji James. Nikatoa shilingi
elfu arobaini na kumpatia yule mkata tiketi.
“.. nipe tiketi moja..”
“..ya lini..? maana za leo mpaka kesho zote zimejaa…”
“..zimejaa..?”
“..ndio dada. Zimejaa na hapa unavyoona wanafunzi wengi wa
vyuoni haswa wale wa chuo cha Mtakatifu Agustino na chuo cha biashara ndio
wamefunga hivyo tangu juzi mabasi yanawabeba wao wanafunzi tu..”
“..Ooooh Mungu wangu..!! sasa nitafanyaje jamani na
nahitajika Dar es salaamu leo leo hata niingie saa ngapi..?”
“..labda usubiri basi letu jingine linatokea Kigoma litapita
hapa hivyo kaa pale usubiri..”
Kidogo akili yangu ikakaa sawa nakusogea mpaka eneo la kupumzikia
abiria nakuanza kusubiri. Ilinichukuwa kama masaa mawili kusubiri huo usafiri
wa kutokea Kigoma. Bado hakukuwa na dalili zozote wala hata taarifa zinazotia
nguvu juu ya hilo basi litokalo huko kigoma. Jua kali lililochora kivuli
kikubwa chini ilimaanisha dhahiri kuwa itakuwa tayari imetimu mchana tena ule
mchana wakuanzia saa sita nakuendelea maana jua lilikuwa kali sana. Nilikiwa
bado nimezubaa mwenyewe mara ghafla nikahisi kama kuna mtu ananigusa mgongoni
taratibu. Sikutaka hata kugeuka kwani niliamini kwa asilimia zote huenda
atakuwa ni mdudu ama kweli kuna mtu. Nilichukua mkono wangu wa kulia nakuanza
kupapasa papasa kwa nia yakukitoa kitu kinachonigusa kwa begani. Kadri
nilivyozidi kukitoa ndipo kilizidi kunibonyeza kwa nguvu na kwa sasa nikaanza
kuisikia na muambatano wa sauti ya kike kwa mbali.
”..Samahani dada naomba kukuuliza kitu..?”
Alikuwa Mmama mwingine na ni
mgeni machoni mwangu kwani hata sikuwahi kumuona maishani mwangu. Sura
yake pana iliyokuwa imeng’arishwa na manukato ya zile losheni zinazopendwa na
baadhi ya kina dada wa uswahilini na waliokuwa na kipato kidogo. Zile zinazojulikana sana kwa kubadilisha sura yako
ya kutoka weusi nakuwa weupe. Wengi wanapenda kuiita ‘carolite’. Na kwa sasa
harufu ile ya carolite ilikuwa inapambana na pua zangu zilizokuwa zimenasa
harufu hiyo kali na inayochukiwa na baadhi ya wanaume wenye pesa zao. Niliendelea
kumtolea macho huku nikijipa maswali mara mbili mbili ndani ya ubongo wangu nakuona
sasa huyu huenda ndio akawa Mke wa mchungaji James kweli. Nilimkazia macho
nakumjibu.
“..uliza tu mama yangu..?”
“..haya..! Ujue nakufahamu sana binti japo wewe huwezi
kunikumbuka mpaka nikukumbushe..?”
“..ni kweli unayosema mama..!”
Woga tayari ulishaninyemelea Tina mimi nakuona sasa haya ni
majaribu haswa ya dunia. Nilikuwa mpole ghafla nakujidai mtakatifu tena Yule wa
kanisani kabisa. Nilijinyenyekeza huku nikimtolea macho na kutega maskio yangu
kwa kumsiliziza kwa umakini mkubwa.
“..nimekufuatilia muda mrefu.., kwanza kabisa pole na matatizo
yaliokukuta kule tuliposafiri wote ikiwa ni pamoja na ajali tuliokuwa tumeipata..”
“..pole ya nini tena Mama. Mbona mimi sijasafiri nina muda
mrefu nahii leo ndio kwanza nasafiri kuelekea Dar..?”
“..wala usitie shaka na mie. Mie nilikuwa mmoja wapo katika
lile basi tulikuwa tumesafiri nalo jana kutoka Dar, na nakumbuka kabisa
ulipandia kijiji fulani hivi japo kwa jina sikikumbuki na hapo ukapata siti
tena kwa bahati nzuri ukakakaa na mchungaji mmoja hivi anaitwa mchungaji
James..”
Akili yangu ikawa haitaki kabisa kukubaliaana na ukweli aliokuwa
anaendelea kuongea huyu Mama. Sura yake kila nikiivutia kumbukumbu bado ilikuwa
ni kazi kuikumbuka. Nilichokifanya niliendelea kumkana kama vile Yuda
alivyomkana Yesu mara tatu..
“..wewe Mama utakuwa umenifananisha mie..?, embu niondokee
hapa..!! Kwanza unavyoendelea kukaa na mimi, hiyo mikarolite yako inazidi kuharibu
pua zangu..?”
Nilijifanya nimekasirika nakumgeuzia kibao yule Mama. Umati wa
watu ukaanza kujaa katika eneo nililokuwa nimekaa na huyu Mama ukinizunguka.
Yule Mama aligeuza macho yake huku na huku kana kwamba kafumaniwa ama ameona
kitu cha ajabu sana kwangu.
“..nakupa dakika moja tu na wala siendelei.. Jibu ndio au
hapana..?”
kwa muda huu yule mama alikuwa amebadilika sura na sauti nakuwa
mbogo kwa muda. Kigugumizi cha ajabu kilichoambatana na kwikwi kali kikaanza
kunishika Tina mimi huku nikiwa sina ujanja tena. Nikiwa bado najiandaa kumjibu
yule Mama akanishika kwa nguvu ile blauzi yangu nakuanza kuropoka.
“..sasa utaeleza vizuri kwanini umemuua mchungaji wetu tena
mchungaji James tuliokuwa tukimpenda sana kwa mahubiri yake..?”
Maskini Tina mimi nilijikuta nimeshaingia matatani tena,
nilijitahidi japo kuzirudisha kumbukumbu kumtambua huyu Mama. Ndipo nikakumbuka
kuwa jana wakati nipo safarini siti moja na marehemu mchungaji James aliniambia
kuwa nilizimia mara mbili wakati ananiombea na tena wakisaidiana kuniombea na
Mmama ambaye alikuwa mtu wa Mungu. Nilihuzunika sana nakuanza kuilaumu nafsi
yangu kwa kutokufikiria. Nikiwa bado kwenye mawazo huku watu wakinishangaa mimi
na huyu Mama. Mara huyu Mama akatoa sauti ya kuamuru kitu.
“.. jamani mapolisi binti mwenyewe ndio huyu hapa..!!,
mchukuweni tumpeleke kituoni..”
Kumbe na mapolisi walikuwa wamenizunguka eneo lote
nililokuwa nimezungukwa na watu ambapo walikuwa wamevalia nguo za kiraia.
Walinichukuwa nakunipiga pingu huku umati wa watu ukinisikitikia kwa kitendo
nilichokifanya cha kumuua mchungaji wao mchungaji James..
*** Inamaana ndio utakuwa mwisho wa safari ya Tina..?
*** Huyo Mama umeshamkumbuka..? na nini hatma ya Tina huko
kituoni..?
*** Utamu wa story hii ndio kwanza unaanza kunoga. Endelea
kufuatilia ujue ** Play gal – 55 itakuwaje..?
*****Itaendelea..*****
Labels: andy ryn stories
1 Comments:
aisee Andy unatisha uhondo ndo kwanza unaanza haya 2naendelea kusubiri.
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home