PENDA KULA MBOGA ZA MAJANI NA UONE FAIDA ZAKE..
Baada ya utambulisho wa umuhimu na faida ya kula matunda na mboga kwani
kila mboga na kila tunda vina nafasi tofauti ya kujenga na kulinda
mwili. Watoto wengi wanasumbua sana kwenye kula hasa mboga majani
asilimia kubwa sio wapenzi angalu upande wa matunda watoto wengi hupenda
matunda lakini kwa kuchagua sio matunda yote watapenda kula tabia hii
hujitokeza kwa kila mtoto hakuna aliekamilika nakumbuka hata mimi
nilipokua mtoto nilikua nasumbua sana kula kiasi ikapelekea kua na afya
dhaifu wakati wa kukua kwangu mpaka nilipobadili tabia na kuanza kula
bila ya kufatiliwa.
Unaweza badilisha tabia ya mtoto wako au mtu yeyote unaeishi nae nyumba moja asiyependa kula mboga majani au matunda kwa kubadilisha muonekano wa chakula hicho au tunda hilo kwa kulinakshi kwa mtindo wowote ule ilimradi kionekane kitu tofauti na kinachovutia hii itakua njia rahisi sana kumvutia mtoto au mkubwa chakula kizuri au upambaji wa chakula sio mpaka hotelini hata nyumbani unaweza fanya sanaa hii na wala haiitaji muda mrefu wa maandalizi muonekano bora wa chakula hutia hamasa kwa mlaji leo tutaangalia utengenezaji wa salad na kuipamba na uandaaji wa mboga ktk muonekano wa kuvutia upande wa kuchonga matunda tutaangalia wakati ujao fata maelezo jinsi ya kutengeneza salad yenye mchanganyiko wa mboga mboga hapo chini.
KWA
KUFATILIA MAELEZO HAYA YOTE UTAKUA UMEFANIKIWA KUMREKEBISHA KAMA NI MUME
AU MTOTO ASIEPENDA KULA MBOGA ZA MAJANI AU MATUNDA IKIWA UMESHAFAHAMU
PIA UMUHIMU WA VYAKULA HIVYO KWA BINADAMU
Unaweza badilisha tabia ya mtoto wako au mtu yeyote unaeishi nae nyumba moja asiyependa kula mboga majani au matunda kwa kubadilisha muonekano wa chakula hicho au tunda hilo kwa kulinakshi kwa mtindo wowote ule ilimradi kionekane kitu tofauti na kinachovutia hii itakua njia rahisi sana kumvutia mtoto au mkubwa chakula kizuri au upambaji wa chakula sio mpaka hotelini hata nyumbani unaweza fanya sanaa hii na wala haiitaji muda mrefu wa maandalizi muonekano bora wa chakula hutia hamasa kwa mlaji leo tutaangalia utengenezaji wa salad na kuipamba na uandaaji wa mboga ktk muonekano wa kuvutia upande wa kuchonga matunda tutaangalia wakati ujao fata maelezo jinsi ya kutengeneza salad yenye mchanganyiko wa mboga mboga hapo chini.
Hili
ni jokofu la kutunzia mchanganyiko wa mboga katika nyuzi joto 4 hadi 5
tu kwa hali ya usalama sana kwa manufaa na afya ya mlaji tukianzia juu
kushoto ni mahindi mabichi ya njano kabla huifadhiwa katika kopo tayari
kwa matumizi, karoti iliyokwaruzwa, Lime stone lettuce, chicory, Radish
iliyokwaruzwa, zucchin iliyokwaruzwa, rollo nyekundu, rollo ya kijani,
matango yaliyokatwa, celeriac salad, curly endive, chicory nyekundu.
Katika
sahani yako anza kupanga mboga ambazo zimekatwakatwa ambazo ni karoti,
matango, mahindi machanga ya njano, celeriac salad na radish nyeupe
Chota kidogo kidogo kila moja panga kwa mtindo wa duara nusu sahani tu kama mduara wa nusu mwezi kati kati acha nafasi kiasi.
Baada
ya hapo chukua jani la salad moja moja toka kila aina ya salad pagange
sambamba majani hayo kisha zungusha yabane kama unataka kuyafunga kamba
kisha kata kiasi upande wa chini utakua umepata kitako safi utakua
umetengeneza kama uwa rozi.
Kisha
liweke juu ya zile mboga mboga pembei yake kata kipande cha tikiti maji
rangi yeyote ile kama ni la kijani, jekundu au rangi ya chungwa pamba
kama invyoonekana katika picha.
Kisha
kata slice nyembamba ya chungwa katikati yake weka tunda lolote dogo la
mviringo kama zabibu au strawbery chomeka toothpick ili ishikilie
chungwa juu ya tikiti maji.
Salad
hii unaweza mwagia dresing yeyote ile mfano italian dressing, french
dressing au siki na chumvi inatosha salad hii unaweza kula na kipande
cha kuku, samaki wakuchemsha au wa kukaanga na unakua umekula mlo safi
kabisa bila stach kwa watu wanaofanya dayati hapa ni mahala pake mvuto
na muonekano wa sahani utamfanya mlaji avutie hata kama si mpenzi wa
mboga na matunda.
Hili
ni jokofu la kutunzia mchanganyiko wa mboga katika nyuzi joto 4 hadi 5
tu kwa hali ya usafi sana kwa manufaa na afya ya mlaji tukianzia juu
kushoto ni nanasi iliyopikwa katika sukari, embe mafuta, cappers,
vitunguu vidogo vya kopo, chopped chives, chopped onion, olives nyeusi,
asparagus, matango machanga yaliyosindikwa, olives zakijani, Nyanya
Katika
sahani yako anza kupanga mboga ambazo zimekatwakatwa ambazo ni karoti,
matango, mahindi machanga ya njano, celeriac salad na radish nyeupe.
Chota kidogo kidogo kila moja panga kwa mtindo wa duara kuzunguka sahani yote katikati acha nafasi.
Baada
ya hapo chukua jani la salad moja moja toka kila aina ya salad pagange
sambamba majani hayo kisha zungusha yabane kama unataka kuyafunga kamba
kisha kata kiasi upande wa chi utakua umepata kitako safi utakua
umetengeneza kama uwa rozi.
Kisha
liweke pembeni ya zile mboga mboga katikati ya sahani unaweza weka
mchanganyiko wowote ule wa nyama ya kuku, ngo'mbe, samaki au sausage
iliyochemshwa ikapoa.
Kata saizi ya kuweza kuingia mdomoni kisha changanya na vitunguu vilivyochopiwa safi pamoja chives.
Mchanganyiko
huo unaweza malizia na chaguo lako la dresing yeyote uipendayo kisha
unamwagia kati kati ya sahani mwisho kata nyanya kipande weka pamoja na
tango dogo la kopo na olive moja ya kijani na moja nyeusi kwa kupamba
salad yako.
Kwa upande wa mlo kamili baada ya kupika chakula chako kikaiva kama ni ugali au wali
Chemsha njegere zisiive sana
Kisha kata vitunguu vidogo sana kaanga katika siagi dakika 1 tu
Kisha weka hizo njegere zilizoiva katika sufuria kwa dk 2 usiasahau chumvi kisha zitoe
Chukua nyanya nzuri ngumu iliyokwisha iva kata nusu pia kata kidogo katika kitako ili iweze kukaa katika sahaki
Kisha toa mbegu zote katikati ya nyanya tumia kijiko kuchota na jaza zile njegere kwanye nyanya
Kisha save nyanya hiyo yenye njegere kama mboga majani itakayo ambatana na chakula chako kama ni cha mchana au cha usiku.
Muonekano na mchanganyiko wa rangi inakua kivutio kizuri sana kwa mtu asiependa kula mboga majani.
Sasa hapa ndio utawakamata kweli kweli wasiopenda kula mboga za majani,
Chukua maharage mabichi yachemshe kiasi yasiive sana yabaki na rangi yake nzuri ya kijani
Kisha unachukua bacon slice zipo aina mbili zipo bacon za nguruwe na bacon za ng'ombe chaguo ni lako mlaji.
Kisha chukua maharage hesabu kumi
na tano kisha zungushia bacon katika maharage hayo weka katika ubao wa
kukatia kata ncha za mwisho ili kuweka usawa na muonekano mzuri zaidi.
Ukishamaliza weka kikaango kwenye
jiko la moto wa wastani tu weka mafuta kiasi katika kikaango yakishapata
moto weka maharage yaliyozungushiwa bacon kaanga kiasi tu ili ile
bacona ikauke.
Kisha toa tayari kwa chakula pia
sevu kama mboga majani itakayo ambatana na chakula chako kama ni cha
mchana au cha usiku. Muonekano na mchanganyiko wa rangi inakua kivutio
kizuri sana kwa mtu asiependa kula mboga majani.
Nashukuru sana mdau aliezungumzia
upatikanaji wa bacon ya ng'ombe, nikweli kwa ulaya kupata bacon ya
ng'ombe ni adimu sana ila hapa kwetu Tanzania zinapatikana kwa wingi
ukienda katika supermaket kubwa au maduka makubwa ya nyama utapata.
Endapo umekosa basi chukua mboga
hiyo hapo juu inaitwa leeks kata jani lake lisafishe vizuri kisha
zungushia vizuri maharage yako hatua za upishi ni zile zile unaikaanga
kidogo tu itaiva na italeta harufu nzuri sana kwahiyo kwa asie kula
kabisa nyama atakua nae kafaidika.
Jumapili njema..
endelea kupata uhondo hapa hapa bongomixx
Labels: ~ Mapishi ~
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home